Katika ushiriki wa Tanzania hii miaka ya karibuni tumeonesha kupoteza dira kabisa na kila washiriki wanapoenda wanazidi kufanya vituko ambavyo vinaishushia hadhi Tanzania kutokana na ukweli kwamba mataifa ya nje yanahubiri ukarimu,upendo na tabia njema tulizonazo wa-TZ.
Miaka ya mwanzo washiriki wetu walianza vizuri sana na tukajisifu katika hilo lakini miaka hii hakuna mtanzania anaetamani hata kuiangalia Bigbrother kutokana na madudu yanayofanywa na washiriki wetu.Kwa mara ya kwanza alipoingia Mwisho Mwampamba mjengoni alifanya vizuri sana na akawa mshindi wa pili na kuipa shavu kubwa sana Tanzania japo alikuwa na mapungufu ya hapa na pale lakini sio ishu, akaja Richard na yeye akafanya vizuri hatimae kuibuka kidedea katika mashindano hayo na hakika hapo ndipo watanzania tukasema hakuna anaetuweza katika mashindano ya Bigbrother Africa.
Aliyekuwa mshiriki wa TZ na mshindi wa pili katika shindano la Bigbrother Africa I, Mwisho Mwampamba.
Aliyekuwa mshiriki wa Tanzania na kuibuka mshindi katika shindano la BigbrotherAfrica II,Richard Beduizenhout.
Latoya.
Baada ya washiriki waliotangulia kufanya vizuri, waliofuatia wakavimba vichwa na kujiona kwa kuwa wametoka Tanzania basi wao ndio wao au niseme washiriki wetu walipatwa na ule msemo usemao "Mgema ukimsifia Tembo hulitia maji"? kiukweli kabisa ndivyo ilivyo...sasa basi tukaona ngoja tutupe karata na kwa wadada..mama yangu tunajuuuta kuwafahamu na kuwapeleka mjengoni, hakika bora tungekaza uzi wa kupeleka vidume hata wakifanya madudu mwisho wa siku ni kuchanganya mataifa tofauti na madada zetu wanaomwegwa kisela.
Mwaka huu kichefuchefu kimetutokea mdomoni sio puani,tumepeleka wadada wawili..jamani mimi nawalaumu waliowachagua bila kuchanganya na kidume pale mjengoni, hakuna asiejua yaliyotokea baada ya kuwapeleka Bhoke na Lotus..mhhhhh, mmoja mapemaaaa kisa ngumi mkononi halafu bora angekuwa Bhoke tungesema ni walewale vita ni vita mura, lakini hapana ni Lotus kamchapa mshiriki mwenzake Luclay kavukavu mwisho wa siku Out.
Lotus
Akabaki Bhoke..mama yangu akagawa uroda kama biskuti..Ernest akamega kisela live bila chenga kila mtu kajionea kasoro vipofu tu ila na waop minong'ono watakuwa wameisikia. Bhoke nae mwisho wa siku kafungasha mapemaaa yupo home, sasa hatujui jamaa ataendelea kumega au ndio walikutana kimjinimjini?
Bhoke
Sasa watanzania wenzangu washiriki wetu ndio wameshatuangusha sasa tufanye nini ili miaka ijayo turudishe heshima yetu? Mimi nianze kutoa maoni yangu,Moja kuna haja tunapochagua washiriki tupate tabia za mtu tangu utotoni na hivi sasa kuwa anaishi vipi, ili kupata watu wenye maadili ya kitanzania na tusiendelee kujitia aibu, Pili mshiriki aingie mkataba na akubali akirudi tunamuadhibu kulingana na sheria za nchi pale itakapodhihirika ameitia nchi aibu na kuwafedhehesha watanzania kipindi chote alichokuwa ndani ya mjengo. Toeni maoni yenu kupitia Bog hii au mnicheki jiffjeff@yahoo.com .