Wednesday, June 27, 2012

ZITTO ALIA NA SERIKALI UNYAMA ALIOFANYIWA Dkt ULIMBOKA


Dkt. Ulimboka akiwa ktk hali mbaya mara baada yakuokotwa akiwa hajitambui,Habari zilizomwagika hivi punde zinadai kuwa Dkt Ulimboka alitekwa jana usiku mishale ya saa 6 za usiku na Watu ambao hawakuweza kufahamika mara moja,habari za wataalamu wa mambo zinasema Dkt alipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kwa jina moja la Abeid..na wakati akiwa katika juhudi za kuonana na huyo mtu watu wawili"vipande" waliokuwa na silaha walimvamia na kumteka kabla hajaangushiwa kisago cha kufa mtu ambacho kilimuacha akiwa hoi bin taaban katika msitu wa Magwepande..kufuatia kitendo hicho wataalamu wa mambo wamefunguka kuwa wafanyakazi wa chumba cha maiti muhimbili nao wamegoma na kuna tetesi za mgomo kuwa mkubwa zaidi!

Akizungumza baada ya kupata habari hizo ifuatayo ni Taarifa ya Mh Zitto.
Ujumbe amenitumia Daktari yupo pale MOI ‘Kaka Zitto,hali ya Dr.Ulimboka yuko unconscious,multiple ribs fracture na kwenye mikono pia amevunjika pamoja na taya,yuko icu wanamstabilise kwanza kwasababu hapumui vizuri,the situation here is really bad,I agree with you this is outright outrageous’
Nimechukizwa sana na habari za kutekwa, kupigwa na kuumizwa vibaya kwa Dr Ulimboka, Kiongozi wa Madaktari Nchini. Mambo kama haya tumezoea kuyasikia kwenye nchi za kidikteta na kuongozwa kiimla ambapo watawala badala ya kutumia njia ya kidemokrasia na kisheria kushughulikia wanaoamini ni maadui zao katika utawala, hutumia wahuni katika Taasisi za usalama kuteka raia, kuwatesa, kuwafunga na hata kuwaua.
Sitaki kuamini kwamba Tanzania imefikia huko. Nimezungumza na baadhi ya madaktari walio karibu na Dokta Ulimboka na kujulishwa kwamba majeruhi huyu wa vitendo vya hovyo kabisa kutokea hapa nchini alikamatwa jana usiku mnamo saa sita na watu wasiojulikana na kupelekwa katika msitu wa MagwePande na kujeruhiwa vibaya. Habari hizi bado hazijathibitishwa na vyanzo huru lakini ndio zilizopo hadi hivi sasa.
Serikali kama mlinzi wa usalama kwa raia inaWAJIBU kueleza tena kwa haraka ni nini kimetokea kwa kijana huyu msomi na kiongozi wa wataalamu wenzake. Serikali INAWAJIBIKA kueleza katika nyakati kama hizi ambapo kuna mgogoro kati yake na madaktari imekuwa wapi kuhakikisha usalama wa viongozi wa madaktari ili kuepusha watu wanaoitwa ‘agente provocateure‘ kuweza kuhatarisha hali ya amani ya nchi na hata kupelekea kuweka hali ya vitisho kwa madaktari wetu.
Serikali INAWAJIBIKA kueleza kama sasa imeamua kutumia njia za kihuni kumaliza matatizo na wananchi wake.
Nimemuomba Waziri kivuli wa Afya wa CHADEMA kufuatilia suala hili kwa kwa karibu sana ili kuhakikisha kwamba ukweli wote na ukweli mtupu unafahamika. Kamwe hatuwezi kuacha Mtanzania yeyote aonewe, anyanyaswe au akandamizwe eti kwa sababu ya kudai haki yake na za wenzake. ‘An injury to one, injuries to all’
Naomba madaktari wamwangalie kwa karibu daktari mwenzao ili aweze kupata nafuu. Ulinzi uimarishwe ili kuhakikisha usalama wake.

EURO 2012 NUSU FAINALI YA MAFUNDI WANAOJUANA SPAIN Vs URENO


Christiano Ronaldo wa Ureno(Real Madrid)

Xavi Alonso wa Uhispania (Real Madrid)

Miamba ya soka barani Ulaya Ureno na Uhispania leo zitapepetana katika nusu fainali ya kwanza ya michuano ya Ulaya katika dimba la Donbass,Donetsk.
Timu hizo mbili zinakutana zikiwa zimesheheni nyota wanaocheza soka la hali ya juu huko barani Ulaya na kwa idadi kubwa ya wachezaji wanakipiga La Liga Uhispania katika timu za Real Madrid na Barcelona hakika leo hatumwi mtoto dukani.

Ureno itamtegemea zaidi Christiano Ronaldo na Beki matata Pepe, Varela,Moutinho,Meireles,Luis Nani na wengineo wengi. huku wapinzani wao Uhispania ikimtegemea zaidi A.Iniesta kama mchezeshaji na wakali wengine kama Xavi,Torres,Sergio Bosquets,Sergio Ramos,Gerald Pique,David Silva,Pedro,Fbregas na mlinda mlango mashuhuri Iker Casillas. 

Ureno wamefika hatua ya nusu fainali baada ya Kujikusanyia pointi 6 na kukamata nafasi ya pili katika kundi B. na hivyo kuingia katika hatua ya robo fainali ambapo walikutana na Ugiriki na kufanikiwa kuwasambaratisha wagiriki kwa bao moja kwa nunge likitiwa kambani na Christiano Ronaldo katika dakika ya 78.

Uhispania ilifanikiwa kutinga katika hatua ya robo fainali za michuano ya EURO 2012 pale ilipojikusanyia pointi 7 na kuibuka kidedea katika kundi C, katika hatua ya robo fainali hizo ilikutana na vigogo wengine wa Ulaya Ufaransa na bila aibu kuwafurumusha nje ya michuano hiyo kwa mabao 2 kwa buyu huku mabao yote yatupiwa kambani na Xavi Alonso katika dakika ya 18 na 90.

Katika mtanange wa Nusu fainali ya leo kati ya Ureno na Uhispania ni vigumu mno kutabiri nani ataibuka meno nje kwa jinsi vikosi vyote vilivyosheheni nyota wanaojuana mno kwa ukweli kuwa wanatoka katika vilabu ambavyo hukutana mara kwa mara katika ligi za Ulaya sana sana La Liga ya Uhispania na Premier league ya Uingereza.

Andre Iniesta wa Uhispania (Barcelona)

Gerard Pique Gerard Pique of Spain in action during the International Friendly between Spain and England at the Ramon Sanchez Pizjuan Stadium on February 11, 2009 in Seville, Spain.  (Photo by Alex Livesey/Getty Images) *** Local Caption *** Gerard Pique
Gerald Pique wa Uhispania (Barcelona)


Torres wa Uhispania (Chelsea)

Cesc Fabregas - Spain v Italy - Group C: UEFA EURO 2012
Fabregas wa Uhispania (Barcelona)


Xavi Hernandez (Barcelona)

Moutinho wa Ureno (Sporting Lisbon)


Pepe wa Ureno (Real Madrid)


Silvester Valera wa Ureno (FC Porto)


Luis Nani wa Ureno (Manchester United)