Arsenal "The Gunners" Watauanza msimu wa ligi kuu ya Uingereza kwa mwaka 2011-2012 kwa mechi ya ugenini dhidi ya Newcastle United mnamo tarehe 13-8-2011. Mechi ya pili Arsenal watawakaribisha vijogoo wa London Liverpool katika dimba la Emirates mnamo tarehe 20-8-2011 kabla ya kuwafuata mashetani wekundu Manchester United katika dimba la Old Trafford mnamo tarehe 27-8-2011 kucheza mechi ya tatu katika msimu mpya wa ligi kuu chini Uingereza.
USD 100,000 unaweza kuzitumia kununua vitu vingi sana na vya kifahari, unaweza nunua gari ya kifahari,boti la kifahari ama nyumba ya kisasa hivyo ni vichache tu. na kama tayari una gari yakifahari kwa mfano Audi na una boti vilevile una nyumba ya kisasa huu ni wakati wako sasa ukanunua wembe uliotengenezwa kwa madini ya sapphire, wembe unaosemekana unadumu kwa miaka 10 na makali yake yanaweza kutumika kwa miongo mingi. Sifa kubwa ya wembe huu hata kama utautumbukuza kwenye moto hauungui utabaki kama ulivyo wataalamu wanasema hata moto wa volcano hauambui kitu katika wembe huu. Kampuni iliyotengeneza wembe huu inasema ni mabadiliko kama ilivyokuwa kutoka kwenye CB Radio mpaka iPhone na sasa wembe wa kawaida mpaka kwenye hii modeli ya USD 100,000.