Friday, November 11, 2011
Reggie Love"Obama's little Brother" kuacha kazi na kuondoka Ikulu ya Marekani "WHITE HOUSE"
Obama na Reggie wakicheza mpira wa kikapu.
Huenda hakuna msaidizi wa ikulu ya Marekani aliye karibu zaidi na Rais Obama zaidi ya Reggie Love, Love mwenye umri wa miaka 30 ni mchezaji wa zamani wa mpira wa miguu na kikapu ambaye amekuwa msaidizi wa Rais Obama tangu kipindi alipokuwa seneta.
Akiwa msaidizi binafsi wa Obama Love amekuwa nae karibu zaidi bila hata kuacha umbali wa futi kadhaa pindi anaposaini Aotographs na anapoweka "swaga" kwa ajili ya kupiga picha.
Amekuwa karibu zaidi na Obama na mara nyingi wamekuwa wakicheza Mpira pamoja na Obama amekaririwa akisema Reggie Love ni mdogo wake na mtu wake wa karibu ambavyo hajawahi kutokea,na sasa anaondoka.
Muda wa mazoezi..Obama akiwa katika jogging,Reggie hayuko mbali
Reggie akiwaonesha jambo maafisa wa Ikulu pamoja na Rais Obama
Nipe Gwala...Obama akimpa tano Reggie
Obama ndani ya Gari na "mdogo wake" Reggie
Obama akiteta jambo na Reggie
Obama akifunga kwa staili ya Lay up
Obama na Reggie wakikatiza mitaa kuelekea mazoezini
Reggie kipindi anacheza mpira wa Kikapu na timu ya Duke
Love akipiga chabo kwanza kabla ya Obama kutoka
Obama na Reggie ndani ya ndege ya rais
Ikulu ya Marekani haijatoa taarifa zaidi ya kuondoka kwa Reggie Love lakini watu wa karibu wamesema Reggie anataka ajikite zaidi katika kumalizia Masters yake katika chuo kikuu cha Pennsylvania (University of Pennsylvania's Wharton Business School).
Mkali wa Kwenye udongo vs mkali wa kwenye nyasi
Uwanja huu sio wakugushi, mastaa Roger Federer na Rafael Nadal walipepetana katika maonesho ya mwaka 2007 katika jiji la Mallorca huko Spain. Ukiwa umetengenezwa kwa udongo nusu uwanja na nusu uwanja nyasi nia na madhumuni kumpata bingwa wa viwanja vya aina zote, ambapo Nadal aliibuka na ushindi wa seti tatu dhidi ya Federer.
Uwanja wa Tennis wa ajabu zaidi Duniani.
Huu ni uwanja ambao utawekwa kwenye kumbukumbu zaidi kwa kuwakutanisha Andre Agassi na Roger Federer zaidi ya walipokutana Wimbledon,U.S open au katika viwanja vingine. Uwanja huu upo futi 700 juu ya pwani ya Jumeirah katika hotel ya nyota saba ya Burj Al Arab nchini Dubai. Mpambano huo ulifanyika february 2005.
Taifa Stars uso kwa uso na Chad leo 11-11-11.
Timu ya taifa ya Tanzania,TAIFA Stars leo itacheza staili ya kushambulia mwanzo-mwisho dhidi ya wenyeji wao timu ya taifa ya Chad katika pambano muhimu la awali kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia. Mechi inapigwa kwenye Uwanja wa Idriss Mahamat Ouya jijini N’Djamena.
Mbwana Samatta anatarajiwa kuongoza mashambulizi ya Stars dhidi ya Chad leo
Kocha wa Stars, Jan Poulsen amekumbushia falsafa yake ya kucheza kwa kushambulia, ambapo atawatumia viungo wawili na kujaza washambuliaji mbele Abdi Kassim, Nizar Khalfan, Mrisho Ngassa na Mbwana Samata.
Stars waliwasili jijini N’dJamena saa saba usiku juzi kwa ndege ya shirika la ndege la Kenya itaingia uwanjani ugenini kusaka matokeo bora katika pambano hilo la awali kabla ya kurudiana na wenyeji wao katika uwanja wa taifa Jumanne jioni.
Katika kujiandaa na pambano la leo, jana Stars walifanya mazoezi yao jioni katika uwanja wa Idriss Mahamat Ouya huku wakimkosa mlinzi wa kulia wa timu hiyo, Erasto Nyoni ambaye alianza kusumbuliwa na malaria tangu alipotua jijini N’Djamena.
Kwa mujibu wa Poulsen, kiungo chipukizi, Shomari Kapombe anatazamiwa kuziba nafasi ya Nyoni huku winga mahiri Mrisho Ngassa akitazamiwa kuanza pambano hilo baada ya kukosekana katika vikosi vya kwanza vya kocha Poulsen katika mechi za karibuni.
Kurudi kikosini kwa Ngassa kunatokana na kujitoa kwa mshambuliaji Danny Mrwanda ambaye amekuwa akianza katika mechi za karibuni kama mshambuliaji anayesaidia mashambulizi kuanzia upande wa kushoto.
Poulsen ameimbia Mwananchi, haifahamu timu ya Chad lakini akaahidi kubadili fomesheni ya Stars dakika kadhaa baada ya kuanza kwa pambano hilo kutokana na jinsi atakavyowasoma wapinzani wake.
“Siijui vizuri Chad. Nitawaangalia katika dakika 20 za mwanzo na kama kuna uwezekano wa kubadili fomesheni basi nitafanya hivyo. Lakini kama ilivyo kawaida yangu, asilimia 95 ya mchezo wa timu yangu unategemea zaidi na jinsi tunavyocheza wenyewe kuliko ambavyo mpinzani wetu anacheza.” alisema Poulsen.
Hata hivyo, Poulsen alisema atafurahi zaidi kucheza soka la kushambulia kwa ajili ya kupata matokeo mazuri badala ya kucheza soka la kujihami ambalo haliisaidii timu.
Naye kocha wa Chad ambaye kikosi chake kilifanya mazoezi ya mwisho katika uwanja wa Idriss Mahamat Ouya, Mohamed Omary alisema dakika tisini ndio zitaaamua mshindi wa leo na si vinginevyo.
“Sichezi mpira nje ya uwanja. Nacheza ndani ya uwanja. Dakika tisini ndio zitaamua matokeo ya mechi ya kesho (leo).” Alisema Omary
Endapo Stars itapata matokeo mazuri katika mechi zake mbili dhidi ya Chad ambazo zinachezwa ndani ya siku nne, itapata nafasi ya kucheza kundi la kufuzu kwenda kombe la dunia ikipangwa pamoja na Gambia, Ivory Coast na Morocco
Mwamuzi wa pambano la leo ni Ogunkolade Bunmi wa Nigeria akisaidiwa na Abidoye Tunde na Baba Abel ambao wote pia ni Wanigeria.
Kwa mujibu wa Poulsen kikosi kamili cha Stars leo ni Juma Kaseja, Shomari Kapombe, Aggrey Morris, Juma Nyoso, Idrisa Rajab, Shaabani Nditi, Henry Joseph,
Abdi Kassim, Nizar Khalfan, Mrisho Ngassa na Mbwana Samata
ADEBAYOR ARUDI TOGO
Emmanuel Adebayor
Emmanuel Adebayory amerejea kuichezea timu yake ya taifa baada ya kuhakikishiwa usalama wake na chama cha soka cha Togo (FTF).
Adebayory, 27, alikutana na maafisa wa FTF siku ya alhamisi kuzungumzia wasiwasi wake huo.
Mshambuliaji huyo anayechezea Tottenham amesema yupo tayari kuichezea timu yake ya taifa wiki ijayo dhidi ya Guinea Bissau katika mchezo wa kufuzu kucheza Kombe la Dunia mwaka 2014.
"Ninafurahi kusema kuwa narejea kuichezea Togo, na niko tayari kuanzia wiki ijayo dhidi ya Guinea Bissau." Adebayor ameiambia BBC.
Mchezaji huyo alistaafu kuichezea timu yake ya taifa baada ya shambulio dhidi ya timu hiyo ambapo watu wawili waliuawa wakati wakielekea katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2010.
Adebayor amesema maehakikishiwa na uongozi wa mchezo huo kuwa nchi itarekebisha hali ya usalama kwa wachezaji wote katika michezo ijayo.
Mwanamama Johnson-Sirlief anaongoza kwa kura je, kuendelea kuiongoza Liberia?
Rais anaetetea kiti chake Liberia Johnson Sirleaf
Wakati kura zinaendelea kuhesabiwa nchini Liberia, rais wa sasa wa nchi hiyo , Ellen Johnson-Sirleaf, anaelekea kupata ushindi wa rahisi katika uchaguzi wa duru ya pili ya rais.
Matokeo ya awali yaliyotolewa na tume ya kitaifa ya uchaguzi imempa Bibi Johnson-Sirleaf ushindi wa zaidi ya asilimia 90 ya kura zote.
Mpinzani wake Winston Tubman amepata asilimia tisa pekee, licha ya wito kwa wafuasi wake kusususia uchaguzi huo.
Bwana Tubman alidai uchaguzi huo ulikumbwa na visa vya udanganyifu katika duru ya kwanza ya upigaji kura, japo waangalizi wa kimataifa wamepinga hilo.
Mpinzani wake Winston Tubman
Bibi Johnson-Sirleaf amesema licha ya idadi ndogo ya watu kujitokeza kupiga kura, matokeo ya uchaguzi huo ni halali.
''Shughuli nzima ya upigaji kura ni halali na hii ni kwa sababu inatosheleza mahitaji ya kikatiba. Tarehe 11 Oktoba watu wa Liberia walipiga kura na japo tulikuwa wagombea 16, asilimia 44 walinipigia kura''. Rais Ellen Johnson-Sirleaf amesema.
Hata hivyo mgombea wa upinzani aliyesusia uchaguzi wa rais wa duru ya pili, Winston Tubman, amepinga uhalali wa uchaguzi huo wa rais, Bwana Tubman amesema ''matokeo yaliyotolewa na tume ya uchaguzi ni ya juu na sidhani walifikisha kiwango hicho''.
Mwandishi wa BBC nchini Liberia anasema kuwa watu wachache walijitokeza kupiga kura.
Takriban thuluthi moja pekee ya wapigaji kura ndio walijitokeza, na hii huenda ikadhoofisha uhalali wa ushindi wa Bibi Johnson-Sirleaf pia, huenda ikazidisha wasiwasi nchini humo.
11-11-2011
Ni vyema ukahakikisha siku ya leo unaandika tarehe ya leo kwa mkono wako, Leo ni tarehe 11-11-2011.
Hizi namba zinavyonana hasa wale tunaopenda kuandika kwa kifupi,mfano leo tutaiandika hivi 11-11-11. Kutokana na ufupisho huo ukiutazama kwa makini ni kama unaona milango mitatu,sasa basi kwa mtazamo huo na kwa jinsi namba za tarehe hii zinavyofanana ni ukweli kuwa hazitatokea tena katika siku za maisha yetu yote.
Milango mitatu kwa mtazamo maana yake ni hii,
Mlango wa kwanza, Huu ni kwa wale ambao hawana imani ya dini yeyote,huku hawapo na kule hawapo na hata hapo walipo hawapo,mlango huu wa kwanza kutoka kushoto unaashiria tarehe na kama tunavyofahamu tarehe inadumu kwa masaa 24 tu halafu inabadilika..tafakari
Mlango wa Pili,yaani katikati ambao unawakilisha mwezi, Huu ni kwa wale ambao imani zao ni mguu nje mguu ndani yaani vuguvugu. Kama tunavyojua mwezi ni siku 30 ama 31 halafu unabadilika.....Tafakari
Mlango wa Tatu,yaani mlango wa kulia huu ni maalum kwa wale ambao imani zao zipo sawia na matakwa ya Mungu wao,Na upande huu unawakilisha mwaka na kama tunavyojua mwaka una siku 365 na 1/4 halafu unabadilika unakuja mwaka mwingine..tafakari.
Fanya uamuzi sasa aidha uwe baridi,vuguvugu au baridi.
Kwahiyo basi ni vizuri ukatenga muda wako japo kwenye kipande cha karatasi ukaiandika tarehe ya leo na kwa imani yako takatifu utakuwa umejitendea haki kwani tarehe hii ni muhimu katika kujipima imani yako imelala upande gani..Naamini kwa kusoma habari hii tayari kwa muda huu umekuwa karibu na mungu wako. 11-11-11.
Subscribe to:
Posts (Atom)