Wednesday, August 17, 2011

Man City to Complete Deal Worth £57.3m to Sign Arsenal Star Samir Nasri Within 48 Hours



Samir Nasri has confirmed he is close to following Cesc Fabregas out of Arsenal and claimed he will do so with a sense of ‘anger and bitterness’.
A day after accusing fans of being disrespectful on Twitter, Nasri left a message for Facebook followers to reinforce his feelings.
‘It’s nearly done,’ said the France midfielder in reference to a proposed £23million transfer to Manchester City.

‘I will leave with bitterness and anger in my heart. I am proud for having played with the Gunners.
‘I have been very disappointed by the supporters last weekend. I am still an Arsenal player but I will leave very soon.’
City hope to complete the transfer before the weekend, with Arsenal at home to Liverpool on Saturday lunchtime.
It was during the goalless draw at St James’ Park when visiting Gunners fans reworked their usual celebratory Nasri song to accuse him of being greedy.
The sentiment stems from his refusal to extend a contract at the Emirates which expires next summer.
Arsenal have offered a new deal worth £90,000 a week but City have dwarfed it with a package worth £165,000 a week

SIMBA NA YANGA KUTIFUANA LEO

                                                          



Wapinzani wa jadi katika soka la Tanzania, timu za Simba na Yanga leo zitaingia katika vita nyingine pale zitakaposhuka dimbani kukabiliana katika mechi ya kuwania Ngao ya Jamii itakayofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mpambano huo unaoashiria ufunguzi wa msimu mpya wa Ligi Kuu itakayoanza Jumamosi hii, unatarajiwa kuwa na upinzani mkali huku ukiwa unafanyika takribani siku 36 tu tangu timu hizo zilipokutana katika mechi ya fainali ya michuano ya Kombe la Kombe la Kagame katika mechi iliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa na Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Ugumu wa mpambano huo unatokana na ukweli kwamba Simba itataka kulipiza kisasi baada ya kufungwa kwa penalti katika mechi ya msimu uliopita ya Ngao ya Jamii wakati Yanga ikitarajia kulinda heshima yake baada ya kufuta uteja wa kufungwa na mpinzani wake kwa takribani miaka nane mfululizo.

Maandalizi.

Timu zote zinaonekana kujiandaa kikamilifu kutokana na kucheza mechi kadhaa za kirafiki za kujipima nguvu na timu za ndani na nje ya nchi.

Wakati Yanga ilisafiri hadi nchini Sudan kucheza na mabingwa wa nchi hiyo timu ya El Hilal, Simba ilijichimbia visiwani Zanzibar kwa takribani wiki mbili, ambapo ilicheza na timu za Polisi Zanzibar na timu ya taifa ya vijana Zanzibar,Karume Boys kabla ya kuhamishia kambi jijini Arusha, ambapo ilialika timu za Victors ya Uganda na AFC Leopards ya Kenya na kucheza nazo mechi za kirafiki.

Makocha:

Kocha wa Yanga, Mganda Sam Timbe amesema ataendeleza rekodi yake kwa kuibuka na ushindi katika mchezo wa leo, ambapo pia aliahidi kuibuka na ushindi kila wakati timu hizo zitakapokutana ili awape raha mashabiki wa klabu yake.

Naye Moses Basena ambaye pia ni raia wa Uganda amewataka mashabiki wa klabu hiyo kutokuwa na wasiwasi akisema amefunga njia zote ambazo wapinzani wanaweza kuchoropoka ili kuepuka kipigo.

Vikosi:

Baadhi ya sura zilizokuwapo wakati wa michuano ya Kagame hazitarajiwi kuonekana dimbani leo kwa upande wa Simba, sura hizo ni pamoja na mshambuliaji Mussa Mgosi aliyeuzwa katika timu ya DC Motema Pembe ya DR Congo, Mohammed Idd Banka aliyesitishiwa mkataba pamoja pia Mwinyi Kazimoto na Ulimboka Mwakingwe ambao ni majeruhi wakati Yanga inatarajiwa kumkosa kiungo mkabaji Nurdin Bakari.

Wachezaji wanaotarajia kuanza kwa upande wa kikosi cha Simba ni pamoja na
kipa Juma Kaseja, Said Nassoro' Chollo', Amir Maftah, Obadia Mangusa, Juma Nyosso, Jerry Santo, Uhuru Suleiman, Patrick Mafisango, Felix Sunzu, Haruna Moshi 'Boban' na Emmanuel Okwi.
Wakati kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuwa; Yaw Berko, Shadrack Nsajigwa, Oscar Joshua,Nadir Haroub 'Cannavaro',Chacha Marwa, Juma Seif kijiko, Godfrey Taita, Haruna Niyonzima, Kenneth Asamoah, Jerry Tegete na Kigi Makasi.
Waamuzi
Idd Mbaga, Israel Mjuni, Hamis Chang'waru.

Ulinzi:
Mkurugenzi wa Kampuni ya mafuta ya Big Bon waliyonunua mechi hiyo, Ahmed Baashwani mbali ya kusema watatumiachombo maalumu kuwabaini watu watakaoghushi tiketi, pia alisema vyombo vya usalama vitakuwa imara kudhibiti vurugu huku akiwataka mashabiki kukaa katika majukwaa kulingana na maelekezo ya tiketi zao.


VUMBI LAHAMIA NOU CAMP LEO

LEO ni fainali ya Hispania Super Cup, ambapo Barcelona itakuwa ikikabiliana na Real Madrid katika mechi ya pili ya kuwania kombe hilo baada ya timi hizi kukutana kwa mara ya kwanza Jumapili iliyopita kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu na kutoka sare ya 2-2.

Katika mechi ya kwanza iliyozikutanisha Real Madrid na Barcelona ya kuwania Hispania Super Cup siku ya Jumapili, timu ya Real Madrid ilipiga mashuti mengi golini, lakini mabingwa wa Ulaya na mabingwa wa Ligi Kuu ya Hispania wao walipata faida ya magoli mawili ya ugenini.

Timu hizi mbili zimekutana kwa mara ya kwanza katika kuwania Hispania Super Cup, ambapo katika mechi ya leo ya marudiano kwenye uwanja wa Camp Nou, Barcelona inapewa nafasi kubwa ya kutwaa kombe hilo.

Katika mechi ya kwanza kipa wa Real Madrid, Iker Casillas alishindwa kuzuia mipira ya hatari golini mwake kwa sababu mipira miwili ya hatari iliyopigwa golini mwake yote ilitinga nyavuni kati ya mashuti manne waliyopiga Barcelona.

Hivyo uwezo walioonyesha Barcelona ni wazi timu ya Real Madrid iliyo chini ya kocha Jose Mourinho itabidi ibadilishe mikakati yake katika mechi ya leo, lakini tangu Mourinho alipojiunga na Real Madrid ameweza kutoa ushindani mkubwa kwa klabu ya Barcelona tangu 2010.

Real Madrid itaingia leo kwenye Nou Camp ikiwa inajiamini kwamba juhudi zao walizozionyesha katika mechi ya kwanza wataziendeleza katika mechi hii ya leo, Real Madrid katika mechi hiyo ya mwanzo walionekana kuwa imara na hawakusumbuliwa na mfumo wa pasi nyingi wa Barcelona.

Ingawa Karim Benzema hakufunga katika mechi ya kwanza, lakini aliweza kusaidia vizuri Mesut Ozil ambaye alikuwa mchezaji muhimu wa Real Madrid katika mechi hiyo.

Cristiano Ronaldo vilevile alikuwa katika kiwango chake cha kutandaza soka, pia kocha Mourinho alipanga safu imara ya ulinzi hata hivyo Barcelona waliweza kuipenya ngome hiyo na kufunga magoli.

Katika mechi ya kwanza, Barcelona haikumtumia beki wake Carles Puyol na pia katika mechi ya leo beki huyo hatacheza. Kukosekana kwa beki huyo wa kati kulionyesha wazi pengo hilo, ingawa mabeki Javier Mascherano na Eric Abidal walijitahidi sana kucheza katika mechi hiyo.

Swali kubwa linalomkabili kocha Pep Guardiola katika mechi ya leo ni kama atampanga kiungo wake mpya Cesc Fabregas na kama atampanga atamtumia kwa muda gani.

Tangu siku ya Jumatatu Cesc Fabregas alianza kufanya kazi na wachezaji wenzake wa Barcelona hata hivyo mchezaji huyo anayetokea Arsenal ya England kwa muda mrefu sasa amekuwa hachezi mechi za ushindani.

Kocha wa Barcelona, Pep Guardiola anakabiliwa na wachezaji wake mahiri kutokuwa fiti, ambapo katika mechi ya kwanza dhidi ya Real Madrid wachezaji wake Xavi Hernandez, Gerard Pique na Pedro walitokea benchi.

Katika mechi ya leo Je, Barcelona itanufaika na kikosi chake na kutwaa ubingwa wa Hispania Super Cup ? au Real Madrid itaondoka na kombe hilo katika uwanja wa Camp Nou unaomilikiwa na Barcelona?

ARSENAL IPO TAYARI KUMUACHIA EMMANUEL EBOUE KWENDA GALATASARAY YA UTURUKI KWA KITITA CHA PAUNDI ZA UINGEREZA MILIONI 4 IMEELEZWA KUTOKA KLABUNI HPOA JIJINI LONDON UINGEEZA.

ARSENAL YAANZA VYEMA LIGI MABINGWA YAISASAMBUA UDINESE


Theo Walcott

Arsenal imeweza kuizabua Udinese ya Italy kwa goli 1 kwa mtungi kwa goli maridadi la Thoe Walcott katika mechi ya kwanza ya hatua za mtoano katika ligi ya mabingwa ulaya ili kuelekea katika makundi.
Ikicheza bila nahodha wake Fabregas ambaye sasa ni mchezaji wa Barcelona ya Spain ilipata bao hilo katika dakika ya nne baada ya kazi nzuri ya Ramsey ambaye alitia majaro nzuri kabisa iliyomkuta Walcott katika nafasi nzuri ya kufunga nae bila ajizi akafanya hivyo kwa kuutia mpira kambani na kuifanya Arsenal kuwa mbele kwa bao hilo. Mchezaji wa Arsena Gibbs aliumia na nafasi yake kuchukuliwa na Djourou ambaye hata hivyo nae aliumia katika mechi hiyo.

VAN PERSIE AVAA VIATU VYA FABREGAS

Mshambuliaji wa Arsenal Robin van Persie amethibitishwa kuwa nahodha mpya wa klabu hiyo.
Robin van Persie
Robin van Persie

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28 anayechezea pia timu ya taifa ya Uholanzi, amekuwa katika klabu ya Arsenal tangu mwezi wa Mei mwaka 2004 na anachukua nafasi hiyo kutoka kwa Cesc Fabregas, aliyehamia klabu ya Barcelona wiki hii.
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema: "Van Persie ni kiongozi kutokana na uchezaji wake, kutokana na ushawishi wake na ari aliyonayo ya kushinda.
"Amekuwa aktika klabu hii kwa muda mrefu na kiufundi ni kiongozi."
Van Persie, ambaye msaidizi wake anakuwa mlinzi Thomas Vermaelen, amesema amefurahia kupata nafasi hiyo.
"Kuwa nahodha, unakuwa ni balozi kwa klabu na nipo tayari kwa hilo," amesema Van Persie. "Nimekuwa katika soka kwa zaidi ya miaka 10, kwa hiyo naelewa namna ya kutekeleza majukumu yangu.
"Kila mara unalazimika kuonesha heshima mbele za watu.
Van Persie hataiongoza Arsenal katika mechi dhidi ya Udinese usiku wa Jumanne katika kuwania nafasi ya kufuzu mechi za Ubingwa wa Ulaya, kwa sababu anatumikia adhabu ya kufungiwa mechi moja na Uefa.
Lakini atachukua hatamu za kuiongoza Arsenal watakapomenyana na Liverpool katika uwanja wa Emirates siku ya Jumamosi kwenye pambano la Ligi Kuu ya Soka ya England.