Thursday, August 11, 2011

JE WAJUA?

Msitu wa Amazoni unazalisha 20% ya Oxygen ipatikanayo duniani.

Mto wa Amazon unatiririsha maji mengi kuingia Bahari ya Atlantic, na zaidi ya maili 100 za bahari zinaingia katika mdomo wa mto ambapo hutoa maji safi kuelekea baharini.
Ujazo wa maji ya mto wa Amazon ni mkubwa ukilinganisha na jumla ya ujazo wa mito saba mikuu duniani kwa ujumla na mto Amazon unatambaa mara tatu zaidi ya mito yote ya U.S.

SONG OF THE DAY

Ipo poa sana....utaipenda

SIGARA INA MADHARA ZAIDI KWA WANAWAKE KULIKO WANAUME

Utafiti mpya umeonyesha kwamba wanawake walio na uraibu wa kuvuta sigara wako katika hatari ya kupata maradhi ya moyo zaidi kuliko wanaume walio na uraibu huo.
Utafiti ulioendeshwa miongoni mwa zaidi ya watu milioni mbili umepata wanawake wako kwenye hatari ya maradhi ya moyo kwa asili mia 25 wakati wanapotumia tumbako.

Sababu za matokeo haya hazijatolowa japo watafiti kutoka Marekani wamesema wanawake wako kwenye hatari kubwa ya kuvuta kemikali zenye simu kutoka kwa sigara ikilinganishwa na wanaume.

Hali hiyo wameongeza imejitokeza katika idadi ya wanawake wanaopata saratani ya mapafu ikilinganishwa na wanaume wanaovuta sigara.