Robo fainali ya kwanza ya michuano ya Tusker kati ya Tanzania Stars na Rwanda umemalizika jijini Kampala katika dimba la Lupogo,na timu ya Tanzania Stars ikitinga nusu fainali kwa kuichapa Amavubi mabao mawili kwa bila. Shujaa wa leo ni Mwinyi Kazimoto alietengeneza pande la maana kipindi cha kwanza katika dakika ya 33 na Amri Kiemba kumalizia kwa kumchambua kipa wa Rwanda na kutupia kambani bao la kwanza.
Dakika ya 54 ilikuwa ni Mwinyi Kazimoto"Iniesta" aliepiga shuti kali lililomshinda kipa wa Rwanda na bila kupepesa njumu, bila kupepesa bukta John Bocco "Adebayor" akauwahi mpira na kuutupia kambani na kufanya mabao kuwa ni 2-0.
Wakati Tanzania inatinga nusu fainali ndugu zao Zanzibar muda huu wapo uwanjani wakipepetana na Burundi katika robo fainali ya pili katika dimba hilohilo la Lupogo jijini Kampala,Uganda.
Wachezaji wa Tanzania wakishangilia goli lililofungwa na John Bocco(14)
Monday, December 3, 2012
ROBO FAINALI TUSKER TANZANIA,ZANZIBAR KUPENYA?
ROBO
FAINALI YA MICHUANO YA TUSKER CHALLENGE CUP 2012 INAYOENDELEA UGANDA
Desemba 3,
2012
Tanzania Vs
Rwanda Saa 8:00 mchana Lugogo
Zanzibar Vs
Burundi Saa 10:00 jioni Lugogo
Desemba 4,
2012
Kenya Vs
Malawi Saa 10:00 jioni Namboole
Uganda Vs
Ethiopia Saa 1:00 usiku Namboole
Subscribe to:
Posts (Atom)