Wachezaji wa Azam wakishangilia bao lililotupiwa na John Bocco "Adebayor/Boko Haramu" aliekaa chini.
Vilabu vya Azam na Vita vimefanikiwa kuingia nusu fainali ya
michuano ya soka ya Cecafa.
John Bocco alikuwa shujaa pale timu yake ya Azam ya Tanzania, ilipofanikiwa
kuingia nusu fainali ya mashindano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati
baada ya kuwafunga mabingwa wa Tanzania, Simba, mabao 3-1.
Katika mechi hiyo ya robo fainali iliyochezwa Jumanne mjini Dar es Salaam,
Bocco alitupiamo kambanio mabao yote dakika ya 17, 46 na 73, wakati bao la kufutia machozi
la Simba likitupiwa na Shomari Kapombe dakika ya 53.
Timu hiyo sasa itapambana na Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo
kwenye nusu fainali itakayochezwa Alhamisi.
Vita Club walifuzu baada ya kushinda kwa mambao 2-1 dhidi ya Atletico ya
Burundi kwenye mechi nyingine iliyochezwa Jumanne. Mabao ya Vita yalifungwa na
Taddy Etekiama na Basilua Makola wakati bao la Atletico lilifungwa na Pierre
Kwizera.
Matokeo hayo yamekuwa ya kushangaza hasa ikizingatiwa kuwa Simba ni timu
kongwe ambayo imeshinda kombe hili la ukanda mara sita.
Nayo Azam, iliyoanzishwa mwaka 2007, haya ni mashindano yao ya kwanza
kimataifa tangu timu ianzishwe na ilipata tiketi ya kushiriki baada ya kumaliza
ligi msimu uliopita ikiwa nafasi ya pili.
Mafanikio ya Azam yanakuja baada ya kusajili wachezaji kutoka Ivory Coast na
Kenya na kumwajiri kocha kutoka Uingereza.
Mechi zote za nusu fainali zitachezwa Alhamisi kufuatia kuondoshwa Simba
kwenye mashindano.
Timu nyingine zitakazokutana kwenye hatua hiyo ni bingwa mtetezi Yanga ya
Tanzania na APR ya Rwanda.
Fainali itachezwa Jumamosi na bingwa atapewa zawadi ya dola 30,000 na mshindi
wa pili 20,000, na atakayemaliza katika nafasi ya tatu ataondoka na kitita cha
dola 10,000.
Katika mchezo wa huo, kikosi
cha Azam kilikuwa; Deo Munishi, Ibrahim Shikanda, Erasto Nyoni,
Said Mourad, Aggrey Morris, Kipre Michael Balou/Ramadhan Chombo, Kipre Herman
Tcheche/George Odhiambo ‘Blackberry’, Salum Abubakar, John Bocco, Ibrahim
Mwaipopo na Khamis Mcha ‘Vialli’/Jabir Aziz.
Simba SC; Juma Kaseja,
Haruna Shamte, Shomary Kapombe, Lino Masombo, Juma Nyosso, Mussa Mudde, Uhuru
Suleiman/Kiggi Makassy, Mwinyi Kazimoto, Felix Sunzu, Haruna Moshi na Jonas
Mkude/Amri Kiemba.
Mrisho Ngassa akiwa ubaoni
Kocha wa Simba Milovan Cirkovic akiwa amelowana kwa kichapo.
Kocha wa Yanga Tom Saintfiet ,Felix Minziro naMfaume athumani wakifuatilia mtanange kati ya Simba na Azam
Benchi la Simba haliamini kilichotokea katika mechi yao dhidi ya Azam
Mashabiki wa Azam F.C
Mashabiki wa Simba S.C
John Bocco "Boko Haramu" akijaribu kuiponyoka ngome ya Simba
Felix Sunzu akiwa amerudi nyuma kusaidia kuokoa jahazi wakati mpira wa kona ukielekezwa lango la Simba
Kipre Cheche wa Azam akitiririka kuelekea kumsalimu Juma Kaseja
John Bocco "Boko Haram" akishangilia bao la pili
John Bocco 'Boko Haram" na Abubakar Saalum 'Sure Boy' wakishangilia kwa mtindo wa aina yake.
Nazi hii ilivunjwa na kamati ya ufundi ya Simba S.C lakini haikufua dafu!
Kikosi cha Simba
Kikosi Cha Azam F.C