Monday, September 12, 2011
TORRES KWENDA AC MILAN
Italian giants AC Milan are keeping a close eye on Fernando Torres’ situation at Chelsea.
Sources in Italy confirm that the Rossoneri would dearly love to take the Spaniard to the San Siro, but are well aware that this would not be possible on a permanent basis, with Torres priced out of reach.
However, with the former Liverpool striker struggling to rediscover his best form at Stamford Bridge, Milan believe there may be an opportunity to take the 27-year-old on loan.
Milan have enjoyed similar such arrangements with Chelsea in the past, first taking Hernan Crespo on loan from Stamford Bridge when the Argentine failed to hit the heights expected of him in a blue shirt, and more recently snapping up Andriy Shevchenko on loan for the 2008/09 season.
The hope is that if Torres continues to struggle to show his best, Chelsea boss Andre Villas-Boas may be open to the idea of sending the Spain international to Milan for a morale-boosting stint.
The Rossoneri could even offer to send Alexandre Pato or Robinho the other way to smooth the deal.
Torres has yet to complete 90 minutes this season for Chelsea, finding himself substituted in the club’s first three games, while he was consigned to the bench for the Blues’ 2-1 win at Sunderland this weekend.
Should the Spaniard continue to misfire, Milan’s astonishing dream of taking the player to Serie A may move closer towards becoming a reality in time for the January transfer window.
TOTTENHAM KUMPA MODRIC MKATABA MNONO
Baada ya kukataa kumuuza Modric Tottenham sasa inapanga kujadili juu ya mkataba wake na kumpa offer nono katika mkataba huo aliosaini 2010 ambao ni wa miaka sita.
Bosi wa Tottenham,Harry Redknap amesema,
“Luka will just get on with it – the chairman will sit down and discuss his contract and make a deal,” explained Spurs boss Harry Redknapp.
“We are looking to make him a good offer.
“The transfer window being shut now makes my job easier because he has to just get on with playing.”
Miss Tanzania 2011-2012
Miss Tanzania 2011-2012 Salha Israel katikati akiwa na shangazi yake (kushoto) na mshindi wa pili (kulia) Tracy Sospeter muda mfupi baada ya kuvishwa taji hilo na aliyekuwa Miss Tanzania 2010-2011 Genevieve.
MAN CITY KUMSAJILI SERGIO KUTOKA BARCELONA
Sergio Busquets
Habari kutoka Italia (Tutto Mercato) zinasema Man City ya Uingereza inatarajia kutangaza dau la paundi za Uingereza milioni 35 ili kumnasa kiungo wa Barcelona ya Uhispania Sergio Busquets,Taarifa zaidi zinaelezea pamoja na Man City kumhitaji Sergio inaonekana zoezi linaweza kuwa gumu.
JUVENTUS ILIPOIADHIBU PARMA 4-1
Picha ya Video ikionesha matukio na magoli yote wakati Juventus ilipotoa kichapo kwa Parma katika ligi kuu ya Italia maarufu kama Serie A.
STEVEN GERRAD KURUDI DIMBANI DHIDI YA EVERTON
SIMBA YASHIKWA SHATI NA AZAM WAKATI IKIKWEA KILELENI
SIMBA wameshindwa kulipiza kisasi kwa Azam baada ya kulazimisha suluhu iliyowapeleka kileleni mwa Ligi Kuu, huku Shirikisho la Soka TFF ikizipeleka Yanga na Simba kucheza mechi zao kwenye Uwanja wa Azam Chamazi.
Matokeo hayo yanaifanya Simba kufikisha pointi kumi kileleni moja zaidi kwa JKT Ruvu huku Azam ikifikisha pointi tano katika michezo minne na Yanga wakiwa mkiani na pointi zao tatu.
Simba waliokuwa na deni la kulipiza kisasi cha mabao 3-0 na kuchezewa samba msimu uliopita na Azam kwenye Uwanja Taifa walizidiwa ujanja na matajiri hao wa Chamazi waliotawala sehemu kubwa ya mchezo huo, lakini walikosa umakini kwenye umaliziaji.
Azam walitengeneza nafasi nyingi za kufunga langoni kwa Simba na kuwafanya mashabiki wengi wa wekundu hao wa Msimbazi waliofurika uwanjani hapo kimya muda mrefu.
Viungo wa Simba, Gervais Kago na Haruna Moshi waliingia kwenye eneo la hatari la Azam dakika ya tisa kwa kugongea pasi, lakini kipa Mwadini Ally alikuwa makini kuokoa hatari hiyo.
Simba iliendeleza mashambulizi yake dakika 20, beki Juma Nyoso aliunganisha vizuri kona ya Ulimboka Mwakingwe, lakini uhodari wa kipa Mwadini ndiyo ulioinusuru Azam.
Krosi ya Mwakingwe ilitua mguuni mwa Kago aliyepiga shuti kali lililopaa juu ya goli na kuwaacha mashabiki waliofurika uwanjani hapo wakishika vichwa.
Tofauti na mechi ya Yanga na Ruvu Shooting iliyoingiza mashabiki 6,566, mchezo wa jana watazamaji walikuwa wengi kutokana na ushindani uliopo baina ya Simba na Azam.
Kiungo Jabir Aziz wa Azam alijaribu kumtungua kipa Juma Kaseja aliyekuwa ameacha goli kwa shuti la umbali wa mita 25 hata hivyo lilipaa juu kidogo ya lango la Simba.
Mshambuliaji John Boko alipoteza nafasi tatu ikiwemo ile ya dakika 45, alipopokea pasi ya Kipre Tchetche akiwa yeye na Kaseja, lakini akapiga nje.
Azam walitawala sehemu kubwa ya kipindi cha kwanza katika kiungo wakiongozwa na Ibrahim Mwaipopo, huku Mrisho Ngassa na Tchetche walikuwa wakianzisha mashambulizi yao kutoka winga na kuifanya Simba kubaki nyuma muda mwingi.
Dakika 72, Mwaipopo nusura afunge goli baada ya mpira wake wa adhabu kugonga mwamba upande wa kulia na kurudi uwanjani.
Mwamuzi Isihaka Shirikisho alitoa kadi za njano kwa Haruna, Shija Mkina kwa Simba kwa upande wa Azam ni Ngasa, Mwaipopo na Morris.
Kocha wa Simba Moses Basena aliwashanga wengi pale alipoamua kumtoa Mkina aliyekuwa ameingia uwanjani baada ya Amri Kiemba kwa dakika kumi na nafasi yake kuchuliwa na Uhuru Selemani.
Naye Steward Hall alimpumzisha Kipre na kumwingiza Wahaba Yahya, pia Simba ilimtoa Kago na kuingia Shomari Kapombe.
SIMBA YANGA KUTUMIA UWANJA WA CHAMAZIHatimaye klabu za Yanga na Simba zimepata nafasi ya kuutumia uwanja wa Azam, Chamazi wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 2000 kwa ajili ya mechi zao za Ligi Kuu kuanzia wiki hii.
Taarifa ya Simba na Yanga kutumia uwanja wa Chamazi ilitolewa jana na Shirikisho la Soka nchini TFF ikiwa ni kutii maagizo ya Serikali ya kutaka Uwanja wa Taifa utumike kwa michezo miwili tu kwa wiki.
Uongozi wa Azam ambao awali ulikataa kuziruhusu klabu hizo kongwe nchini kutumia uwanja wake kutokana na kuhofia uhalibifu wa mali zake wamefanya mazungumzo na Simba na Yanga na kukubaliana.
Mechi zitakazochezwa Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Dar es Salaam; mechi namba 35- Simba vs Polisi Dodoma (Septemba 14), mechi namba 29- African Lyon v Yanga (Septemba 15), mechi namba 45- Yanga vs Villa Squad (Septemba 21), mechi namba 66- Simba vs Ruvu Shooting (Oktoba 19) na mechi namba 71- Yanga vs Oljoro JKT (Oktoba 23).
Huku Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ukitumika kwa mechi namba 39- Azam vs Yanga (Septemba 18), mechi namba 50- Simba vs Mtibwa Sugar (Septemba 25), mechi namba 52- Yanga vs Coastal Union (Septemba 28) na mechi namba 58- Yanga vs Kagera Sugar (Oktoba 13).
Nyingine ni mechi namba 62- Simba vs African Lyon (Oktoba 16), mechi namba 65- Yanga vs Toto Africans (Oktoba 20), mechi namba 72- Simba vs JKT Ruvu (Oktoba 22), mechi namba 78- Yanga vs Simba (Oktoba 29) na mechi namba 86- Moro United vs Simba (Novemba 2).
Vikosi
Azam: Mwadini Ally, Erasto Nyoni, Waziri Omari, Said Morad, aggrey Morris, Ibrahimu Mwaipopo, Mrisho Ngasa, Jabir Aziz, John Boko, Kipre Tchetche na Ramadhan Chombo.Simba: Juma Kaseja, Nassoro Said, Amir Maftah, Juma Nyoso,Victor Costa, Partick Mafisango, Amri Kiemba(Shija Mkina/ Uhuru Seleman), Jerry Santo, Gervais Kago, Haruna Moshi, Ulimboka Mwakingwe.

KIUMBE MPYA KUBAINI ASILI YETU AGUNDULIWA A.KUSINI
Mabaki ya kale ya viumbe wawili waliopatikana huko Afrika ya kusini wanaofanana na binadamu yanaweza kubadili mtazamo wetu kuhusu asili yetu.
Mabaki hayo yanayokadiriwa kuwa yamepatikana baada ya miaka milioni 1.9 yalielezewa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2010, na kupewa jina la kitaalamu Australopithecus sediba.
Tangu hapo kundi la wataalamu lililofanya ugunduzi wakati ule limerudi na uchambuzi wa kina zaidi.
Kundi hilo limelifahamisha jarida linalochapisha habari za Sayansi kua maumbile yaliyoshuhudiwa ya ubongo, miguu, mikono na mifupa ya nyongo yote yameonyesha kama viumbe hawa ni wa kwanza katika asili yetu -binadamu - ama kwa jina la kitaalamu - Homo sapiens.
Profesa Lee Berger wa Chuo kikuu cha Witwatersrand mjini Johannesburg anasema kuwa "wamechunguza sehemu muhimu za binadamu zinazoelezea umbo linalombainisha binadamu na viumbe wengine, na kuna uwezekano wa sehemu za binadamu kukuwa kwa nyakati tofauti na A.sediba anaonyesha kutimiza vigezo vya maumbile ya mwanadamu, kiongozi wa kundi la wataalamu aliifahamisha BBC.
Ni madai makubwa, na ikiwa yana ukweli, basi kuna uwezekano wa rekodi zilizokuepo kuhusu asili yetu kuwekwa kando.
Nadharia inashikilia msimamo kuwa binadamu wa sasa anaweza kudai urithi wake kutoka kwa kiumbe anayejulikana kama Homo erectus aliyeishi zaidi ya miaka milioni moja iliyopita.
Mnyama huyu, kwa mujibu wa wataalamu wa anthropolojia, huenda naye alikua na asili ya aina ya kiumbe ambaye hakustaarabika ajulikanaye kama hominin, mfano ni Homo habilis au Homo rudolfensis.
Jambo la kuridhisha kuhusu madai juu ya A. sediba ni kwamba ingawa ni wa kale kuliko wenzake , baadhi ya maumbile yake na uwezo wake yanaonyesha kuwa alikuwa na uwezo zaidi kuliko wenzake wa baadaye.
Kwa kifupi inaaminika A.sediba yuko karibu zaidi na babu wa mwanadamu Homo erectus.
Mabaki ya sediba yalifukuliwa huko Malapa katika eneo maarufu la asili ya mwanadamu , nje kidogo na kaskazini magharibi mwa Johanesburg.
Viumbe hawa waliotambuliwa kama mwanamke my mzima na mvulana kijana, wametambuliwa kuwa mama na mwana. Kilichobainika ni kuwa walifariki kwa pamoja kufuatia ajali iliyowasababisha kudondoka ndani ya mfumo huo wa shimo kuu au walikwama humo ndani.
Baada ya kufariki, miili yao ilisukumwa ndani ya shimo lenye tope na kuganda humo kwa mda mrefu kama mabaki ya wanyama wengine yaliyokwama humo.
AJALI YA MELI ZANZIBAR YAUA MAMIA YA WATU
Watu wasiopungua 197 wamekufa baada ya meli iliyokuwa imezidisha mizigo kuzama katika pwani ya kisiwa cha Zanzibar ikiwa na watu takriban 800.
Msemaji wa serikali amesema watu 620 walionusurika wameokolewa. Serikali imetangaza siku tatu za maombolezo.Inadhaniwa kuwa meli hiyo ilizama baada ya injini yake kukosa nguvu.
Shughuli za uokoaji zilikwazwa kwa kuwa meli hiyo ilizama usiku.
Zaidi ya watu 100 bado hawajulikani walipo, lakini watu 325 walionusurika wameokolewa, kwa mujibu wa waziri wa masuala ya dharura wa Zanzibar.
Meli hiyo, MV Spice Islander ilikuwa ikisafiri kati ya Kisiwa kikuu cha Unguja kuelekea Pemba.
Meli hiyo ilikuwa ikirejesha watu baada ya kumalizika kwa mfungo wa Ramadhani.
Msaada
Serikali ya Zanzibar imeunda kituo cha uokoaji na kutoa wito kwa taasisi zote kusaidia katika shughuli za uokozi. Serikali hiyo pia imeomba msaada kutoka nchi nyingine za nje, kama vile Kenya na Afrika Kusini.Walionusurika walichukuliwa na boti za kibinafsi na kupelekwa katika bandari ya Zanzibar, amekaririwa kamishna wa polisi wa Zanzibar Mussa Hamis.
Miili ya watu imekuwa ikisukumwa katika pwani ya Zanzibar na mawimbi. Mpaka sasa miili ya watu 100 wamepatikana, amesema mwandishi wa BBC Ali Saleh akiwa Zanzibar.
Maelfu ya ndugu na jamaa wanasubiri kusikia taarifa za ndugu zao ambao walikuwa ndani ya meli hiyo, anasema mwandishi wetu.
Mohhamed Aboud, waziri wa masuala ya dharura wa Zanzibar anasema watu 259 walionusurika wameokolewa lakini 40 kati yao wamejeruhiwa sana.
"Boti yetu imechelewa kwa sababu wanatumia vyombo vyote vya baharini kuokoa watu"Anasema Catherine Purvis
Catherine Purvis, mtalii kutoka Uingereza aliyepo Zanzibar, akisubiri boti ya kwenda Dar es Salaam amesema ameshuhudia miili ya watu wengi ikitolewa ndani ya maji.
"Nimesimama katika bandari ya Zanzibar nikiwa na watalii wengine kama 10 wa Marekani na Uingereza.
"Boti yetu imechelewa kwa sababu wanatumia vyombo vyote vya baharini kuokoa watu".
Rubani mmoja wa helikopta Kapteni Neels van Eijk alipita juu ya eneo la tukio.
"Tuliona walionusurika wakiwa wameshikilia magodoro na majokofu au chochote kile kinachoweza kuelea. Ni vigumu kusema idadi kamili, lakini naweza kusema walikuwepo zaidi ya watu 200 walionusurika ndani ya maji na miili ya watu pia," ameiambia BBC.
"Wakati huo, kulikuwa na boti chache zilizofika katika eneo hilo. Walikuwa wakitafuta walionusurika, ingawa bahari haikuwa imechafuka sana, mawimbi walikuwa makubwa, kwa hiyo ilikuwa vugumu kuona walionusurika.
"Tulirusha ndege yetu na kuziongoza boti hadi kwa watu walionusurika ili waweze kuwachukua. Kulikuwa na miili kadhaa ndaniya maji."
Meli hiyo iliondoka Unguja takriban saa tatu usiku saa za Afrika Mashariki na inadhaniwa kuwa ilizama majira ya saa saba usiku.
Ilikuwa imebeba abiria wengi kiasi kwamba baadhi ya abiria waligoma kupanda, amekaririwa abiria mmoja aliyenusurika Abdullah daid, akizungumza na shirika la habari la AP.
Subscribe to:
Posts (Atom)