Tuesday, August 23, 2011

HARUSI YA KIM KARDASHIAN NA CHRIS HUMPHRIES, PICHA WAKATI WA UCHUMBA WAO

Msanii maarufu Kim Kardashian amefunga pingu za maisha na mcheza kikapu mashuhuri Chris Humphries siku ya jumamosi jioni katika eneo la siri jijini Montecito,Calif huku ikihudhuriwa na wageni wapatao 440.
Watu mashuhuri katika harusi hiyo ni kama ifuatavyo, Demi Lovato, Babyface, Vera Wang, Mario Lopez, Mark Ballas, Ciara, Carmelo Anthony, Eva Longoria and Eduardo Cruz, Ryan Seacrest and Julianne Hough, Alan Thicke, Cheryl Burke, Melanie Brown, Maria Menounos, Sugar Ray Leonard, Serena Williams, Kathie Lee Gifford, Brittny Gastineau, Greta Van Susteren, Jillian Barberie, Brody Jenner and Avril Lavigne, Scottie and Larsa Pippen, and Dina, Ali and Lindsay Lohan.

Kim katika harusi hiyo alivaa gauni la mbunifu wa mavazi Vera Wang na viatu vya Guissepe Zanotti. Zifuatazo ni picha za Kim na Chris wakati wa uchumba wao.

FAMILY TIME   photo | Avril Lavigne, Brody Jenner, Kim Kardashian, Kris Humphries
Kim na Chris (kushoto),wakiwa na kaka yake Kim wa kufikia Broddy Jenner na mchumba wake.

SWEET STROLL   photo | Kim Kardashian, Kris Humphries
Kim na Chris wakiwa kitaani New York,inaelezwa utanashati wa Chris ni miongoni mwa vitu vinavyomvutia Kardashian.

BEACH BABES   photo | Kim Kardashian, Kris Humphries
Chris hapa alipoungana na familia ya Kardashian huko Punta Minta,Mexico katika sherehe ya kuzaliwa ya dada yake Kardashian, Kourtney alipotimiza miaka 32 Aprili 2011.

PARTY TIME!   photo | Kim Kardashian, Kris Humphries
Kim na Kardashian siku ya kuzaliwa Kourtney.

HOLDING STRONG   photo | Kim Kardashian, Kris Humphries
Kim na Kardashian wakiwa "out" enzi za kufukuziana.

PUBLIC ENGAGEMENT   photo | Kim Kardashian, Kris Humphries
Kim na Kardashian siku walipoweka wazi mahusiano yao baada ya kuvalishana pete. Hapa ilikuwa katika maonesho ya Amber huko Monte Carlo jijini Monaco.

MUST LOVE DOGS   photo | Kim Kardashian, Kris Humphries
Siku Kim alipomtambulisha Kardashian kwa mbwa wake, Brody na Gizmo siku chache kabla ya kuvishana pete.

FANCY FEET   photo | Kim Kardashian, Kris Humphries, Mark Ballas
Wakiwa Magharibi mwa Hollywood na aliekuwa mcheza show wa Dancing with the stars Mark Ballas.

BUSTIN' OUT
 photo | Kim Kardashian
Kim Kardashian.

MAN UNITED YAIADHIBU TOTTENHAM HOTSPURS 3-0

Man United jana iliilipua Tottenham magoli 3 kwa ubuyu katika ligi kuu ya Uingereza inayoendelea nchini humo. Magoli yalifungwa na Welbeck,Rooney na Anderson akagongea msumari wa mwisho.
Tazama magoli jinsi yalivyoingia.

Picha ya magoli na matukio katika mechi hiyo

FABREGAS ATIA KAMBANI KWA MARA YA KWANZA DHIDI YA NAPOLI

Fabregas akitia kambani goli lake la kwanza akiwa na Barcelona katika mechi ya Barcelona dhidi ya Napoli ambayo ilikuwa ya kirafiki kuwania kombe la Joan Gamper , ambapo Barcelona iliibugiza Napoli magoli 5-0.
Magoli yalifungwa na Messi 2,Pedro,Seydou Keita na Fabregas.


Matukio na magoli yote katika mechi hiyo

Upinzani washinda urais Cape Verde

Mgombea wa upinzani Jorge Carlos Fonseca ameshinda katika uchaguzi wa urais wa Cape Verde, akimshinda mpinzani wake Manuel Inocencio Sousa kutoka chama tawala.


Wananchi wakishangilia ushindi wa Fonseca

Bw Fonseca alipata takriban aslimia 55 ya kura zote katika duru ya pili ya uchaguzi siku ya Jumapili, ukilinganisha na mwenzake Bw Sousa aliyepata asilimia 45.

Viongozi hao wawili wamewania nafasi hiyo baada ya Rais Pedro Pires kung'atuka kufuatia kumaliza vipindi vyake viwili.

Wachambuzi wanasema, Cape Verde ni moja ya nchi zenye demokrasia thabit barani Afrika.

Bw Fonseca, mwenye umri wa miaka 60, alisema atalenga zaidi kuujenga uchumi wa Cape Verde.

Amenukuliwa na shirika la habari la AFP akisema, "ushindi wangu ni wa kidemokrasia, kwa heshima ya watu wa Cape Verde walioamini mipango yangu."

MTOTO WA GADAFFI AAPA KULA SAMBAMBA NA WAASI

Mtoto wa kiume wa Kanali Muammar Gaddafi, Saif al-Islam, ambaye awali waasi walidai kuwa wamemkamata, amejitokeza katika hoteli moja inayoshikiliwa na wafuasi wa Kanali Gaddafi.

Saif al-Islam
Mtoto wa Gadaffi Saif Al-islam

Mwandishi wa BBC Matthew Price amezungumza na Saif al-islam na kusema kuwa anaonekana kuwa mchangamfu na shauku kuu.

Saif al-Islam amesema waasi wameingia kwenye ''mtego'' mjini Tripoli na kwamba wanajeshi wanaomuunga mkoni Kanali Gaddafi walikuwa ''wamevunja uti wa mgogo wa waasi hao''.

Waasi wanaopigana kuudhibiti mji mkuu wa LibyaTripoli , wamerudishwa nyuma na wanajeshi wanaomuunga mkono Kanali Muammar Gaddafi.

Lakini wakati mapigano yanapoendelea katika maeneo mbalimbali ya mji, msafara wa waasi kutoka mashariki mwa nchi ulirudishwa nyuma.

Bado hajulikani alipo Kanali Gaddafi.

Jumapili iliyopita waasi walidai kuwa walikuwa wamemkamata Saif al-Islam, pamoja na familia yake.

Hata hivyo, bado Kanali Gaddafi hajulikani alipo. Nyumba yake inalindwa na wapiganaji wanaomtii.

Waasi hao walioingia mjini Tripoli jumamosi iliyopita walikaribishwa watu waliokuwa wakisheherekea katika bustani ya Green Square wakati walipowasili siku ya jumapili.

Waasi hao wamesema kuwa wameweka vizuizi katika sehemu mbalimbali za mji lakini wanakabiliwa na upinzani mkali katika baadhi ya maeneo.

Kamanda wa waasi amesema wanadhibiti asilimia 90 ya mji wa Tripoli.

Kiongozi wa Baraza la Mpito la kitaifa (NTC), Mustafa Abdel Jalil, amesema wakati wa ushindi halisi utakuwa pale watakapo mkamata Kanali Gaddafi.

Rais Obama apongeza watu wa Libya.

Rais Barrack Obama amewapongeza watu wa Libya kwa kile alichokitaja kama ''kujitolea mhanga kusipokuwa kwa kawaida''. Obama amesema watu wa Libya wanakaribia kupata kile wanachohitaji.


Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa, Ban Ki-Moon naye amewakumbusha wanachama wa Umoja huo kuwa, wanajukumu la kuheshimu mahakama ya kimataifa ya jinai, ambayo imetoa hati za kuwakamata Kanali Gaddafi, mtoto wake wa kiume Saif al Islam na mkuu wake wa idara ya ujasusi.

Baadhi ya viongozi wa waasi wanasema afadhali wafunguliwe mashtaka nchini Libya na sio katika mahakama ya kimataifa ya ICC, mjini The Hague.