Thursday, June 21, 2012
MREMBO WA SIKU
On Saturday evening, Mena Suvari put a sexy spin on the little black dress when she showed up at the Motion Picture & Television Fund gala in a barely-there Maria Lucia Hohan cocktail frock
WALIOONGOZA KWA KUTUPIA KAMBANI KATIKA HATUA YA MAKUNDI EURO 2012
1-(3) Alan Dzagoev wa Urusi ameshatupia kambani mara mpaka kumalizika kwa hatua ya makundi, amekwishapoteza matumaini ya kunyakua daruga la dhahabu kwani Urusi haikufanikiwa kufuzu katika hatua ya robo fainali katika kundi A.
2-(3) Mario Gomez wa Ujerumani amekwisha kutupia kambani mara tatu na ana matumaini makubwa ya kuibuka kidedea kwa kutupia kambani katika michuano ya EURO 2012 baada ya Ujerumani kufuzu katika hatua ya robo fainali baada ya kuibuka namba moja katika kundi B ikijikusanyia pointi zote 9 ikifuatiwa na Ureno iliyomaliza kwa pointi 6.
3-(2) Andriy Shevchenko nahodha wa Ukraine ambao ndio wenyeji wenza wa michuano ya EURO 2012 ametupia kambani mara 2 na kwa bahati mbaya wenyeji hao wametupwa nje ya michuano hiyo baada ya kumaliza katika nafasi ya 3 katika kundi D, Uingereza na Ufaransa zikipenya kwa hatua ya robo fainali.
4-(2) Christian Ronaldo wa Ureno amekwisha tupia mara 2 na ana matumaini makubwa ya kuwa kinara wa mabao katika mashindano hayo baada ya Ureno kufuzu robo fainali baada ya kushika nafasi ya pili katika kundi B nyuma ya Ujerumani.
5-(2) Fernando Torres wa Uhispania ametupia mara 2 na anaweza kuendelea kutupia baada ya timu yake ya Uhispania kufuzu kwa hatua ya robo fainali baada ya kuongoza kundi C.
6-(2) Francesc Fabregas wa Uhispania amekwishatupia kambani mara 2 matumaini ya kuendelea kutupia yanabaki baada ya timu yake kutinga katika hatua ya robo fainali ikiongoza kundi C na sasa atachuana na mhispania mwenzake Fernando Torres katika mbio za kuvaa daluga la dhahabu.
7-(2) Mario Mandzukic wa Croatia ametupia mara 2 na ndio mwisho baada ya Croatia kushindwa kuvuka hatua ya makundi kuelekea robo fainali za michuano ya EURO 2012 ikimaliza katika nafasi ya 3 kundi C
8-(2) Michael Krohn-Dehli wa Denmark ametupia kambani mara 2 na matumaini ya kuvaa daluga la dhahabu yaliyeyuka pale Denmark waliposhindwa kufuzu kwa hatua ya robo fainali baada ya kushika nafasi ya 3 kundi B
9-(2) Nicklas Bendtner wa Denmark ametupia mara 2 na ndio amemaliza hapo baada ya Denmark kuburuzwa nje ya michuano hiyo katika kundi B
10-(2) Olof Mellberg wa Sweden nae amefanikiwa kutupia kambani mara 2 na kutokana na ukweli kwamba Sweden haijafuzu kwa hatua za robo fainali matumaini yake ya kunyakua kiatu cha dhahabu yamezikwa rasmi.
11-(2) Petr Jiracek wa Jamhuri ya Czech ametupia mara mbili na itambidi asubiri miaka minne ijayo ili aendelee kuwania ufungaji bora kwasababu Timu yake imeshindwa kufuzu kwa hatua ya robo fainali za EURO 2012.
12-(2) Vaclav Pilar wa Jamhuri ya Czech nae ametupia kambani mara 2 lakini kutokana na timu yake kushindwa kufuzu kwa hatua ya robo fainali sasa matumaini yake ya kutwaa daluga la dhahabu yameishia hapo.
13-(2) Zlatan Ibrahimovic mshambuliaji wa Sweden ametupia kambani mara 2 na ki ukweli kabisa kama Sweden ingesonga katika hatua ya robo fainali basi huenda angetupia mara nyingi zaidi kutokana na uwezo alionao, lakini sasa ndio basi tena Sweden wameshatupwa nje baada ya kushika mkia katika kundi D.
RATIBA YA MECHI ROBO FAINALI EURO 2012
Uefa Euro 2012 | FIXTURES
Thursday 21 June 2012 |
25 | Czech Republic | v | Portugal |
Friday 22 June 2012 |
26 | Germany | v | Greece | Arena Gdansk |
Saturday 23 June 2012 |
27 | Spain | v | France | Donbass Arena |
Sunday 24 June 2012 |
28 | England | v | Italy | NSC Olimpiyskiy |
Wednesday 27 June 2012 |
29 | Winner Q/F 1 | v | Winner Q/F 3 | Donbass Arena |
Thursday 28 June 2012 |
30 | Winner Q/F 2 | v | Winner Q/F 4 | Warsaw National Stadium |
Sunday 01 July 2012 FINAL |
31 | Winner SF1 | v | Winner SF2 | Olympic Stadium |
FAHAMU ZILIZOINGIA ROBO FAINALI EURO 2012 BAADA YA HATUA YA MAKUNDI
Uefa Euro 2012 | LOGS
Group A
Pos | Team | P | W | D | L | GF | GA | GD | Pts |
1 | Czech Republic | 3 | 2 | 0 | 1 | 4 | 5 | -1 | 6 |
2 | Greece | 3 | 1 | 1 | 1 | 3 | 3 | 0 | 4 |
3 | Russia | 3 | 1 | 1 | 1 | 5 | 3 | 2 | 4 |
4 | Poland | 3 | 0 | 2 | 1 | 2 | 3 | -1 | 2 |
Group B
Pos | Team | P | W | D | L | GF | GA | GD | Pts |
1 | Germany | 3 | 3 | 0 | 0 | 5 | 2 | 3 | 9 |
2 | Portugal | 3 | 2 | 0 | 1 | 5 | 4 | 1 | 6 |
3 | Denmark | 3 | 1 | 0 | 2 | 4 | 5 | -1 | 3 |
4 | Netherlands | 3 | 0 | 0 | 3 | 2 | 5 | -3 | 0 |
Group C
Pos | Team | P | W | D | L | GF | GA | GD | Pts |
1 | Spain | 3 | 2 | 1 | 0 | 6 | 1 | 5 | 7 |
2 | Italy | 3 | 1 | 2 | 0 | 4 | 2 | 2 | 5 |
3 | Croatia | 3 | 1 | 1 | 1 | 4 | 3 | 1 | 4 |
4 | Ireland | 3 | 0 | 0 | 3 | 1 | 9 | -8 | 0 |
Group D
Pos | Team | P | W | D | L | GF | GA | GD | Pts |
1 | England | 3 | 2 | 1 | 0 | 5 | 3 | 2 | 7 |
2 | France | 3 | 1 | 1 | 1 | 3 | 3 | 0 | 4 |
3 | Ukraine | 3 | 1 | 0 | 2 | 2 | 4 | -2 | 3 |
4 | Sweden | 3 | 1 | 0 | 2 | 5 | 5 | 0 | 3 |
RUNGU LA UEFA LAIANGUKIA ENGLAND KUFUATIA VURUGU ZA MASHABIKI EURO 2012
Mashabiki wa soka wa Uingereza wakilipuka kwa mayowe ya ushindi
Chama cha soka cha England, FA, kimelimwa faini ya Euro 5,000 (sawa na pauni 4000), kutokana na utovu wa nidhamu wa mashabiki wake ambao Ijumaa iliyopita walijaribu kuuvamia uwanja baada ya England kuichabanga Sweden.
Faini hiyo ni kufuatia mashabiki kujaribu kuingia uwanjani baada ya England kuiangushia kipigo Sweden cha 3-2 katika mechi ya kundi D mjini Kiev.
Chama cha FA kimeamua hakitakata rufaa kuhusiana na faini hiyo, na kwa kuwa UEFA haijaitoza FA pesa nyingi, inaashiria kwamba shirikisho hilo la soka ya Ulaya linalichukua tukio hilo kama jambo dogo.
"Tunakubali hatua iliyochukuliwa, na tunalifikiria tukio hili kama jambo ambalo limetatuliwa," taarifa ya FA ilielezea.
Baada ya magoli ya England yaliyotiwa wavuni na Theo Walcott na Danny Welbeck, mashabiki kati ya 20 hadi 30 walivikaribia vizuizi uwanjani, na kutaka kuingia ndani ya uwanja wa Olympic, lakini walifanikiwa kuifikia sehemu ya riadha tu.
Chama cha FA, kikijitetea, kiliweza kutoa ushahidi thabiti wa video mbele ya UEFA na kuonyesha kwamba “uvamizi” huo ulikuwa ni jambo ambalo lilitokea ghafula, na wala mashabiki hao hawakuwa wamepanga kutekeleza kitendo hicho.
Tukio hilo lilichukuliwa kama jambo dogo, na hata afisa wa UEFA katika mechi hiyo hakulitaja katika ripoti yake kuhusiana na mechi.
Chama cha FA pia kimethibitisha kwamba hakuna mashabiki wa England waliokamatwa aidha nchini Poland au Ukraine katika mashindano ya mwaka huu.
Subscribe to:
Posts (Atom)