Mtanange huo ulitawaliwa na Barcelona lakini walishindwa kabisa kuipenya ngome ya AC Milan waliokuwa wanalinda lango lao na kufanya mashambulizi ya kushtukiza na ya kasi. AC Milan walianza kuwazidi akili Barcelona katika dk 56 pale mzaliwa wa Ghana Kevin Prince-Boateng alipotupia kambani goli la kuongoza na kulipua nderemo na vifijo toka kwa mashabiki9 waliofurika katika dimba la San Siro.
Barcelona walihaha kusawazisha goli bila mafanikio kabla ya kutepeteshwa kwa bao la pili katika dk 80 likitupiwa kambani na Raia wa Ghana Suley Muntari.
Mchezaji mtukutu aliesajiliwa hivi karibuni na AC Milan akitokea Manchester City ambae nae pia ni mchezaji mwenye asili ya Ghana Mario Barwuah Balotelli alionekana uwanjani akiwa na mchumba wake na kundi la masela wakishangilia ushindi wa AC Milan kwa hisia kali.
Boateng na Muntari wakishangilia goli la kwanza
Nimeuaaaaaaaaaaaaaaaaa
Kazi kweli kweli Iniesta na Boateng
Mungu wangu tumetepeteshwa namna hii...
Messi akijaribu kuchanja mbuga
Kamata mwizi meeeeeeeeeeeeen!! Boateng akijaribu kumchimoka Puyol
Kulala kwenuu..Messi na Alves wakiwa chini kufuatia patashika nguo kuchanika ya mpambano huo
Muntari akiachia kombora kuandika bao la pili dk 80
Muntari na Boateng wakishangilia goli la pili
Balotelli na mchumba wake wakifuatilia mpambano