Monday, October 27, 2014

NAHODHA WA BAFANABAFANA AUAWA KWA RISASI


Senzo Meyiwa enzi za uhai wake

Nahodha ambaye pia ni golikipa wa timu ya soka ya taifa la Afrika kusini Senzo Meyiwa amefariki dunia baada ya kupigwa risasi. Jeshi la polisi la nchi hiyo limesema.
Tukio hilo limeripotiwa kutokea katika nyumba ya mpenzi wake iliyopo katika mji wa Vosloorus kusini mwa Johannesburg.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 aliichezea klabu ya Orlando Pirates na alicheza mechi nne zilizopita za timu yake ya taifa katika mechi za kufuzu za fainali ya mataifa ya Afrika.
Jumamosi alikuwepo katika tukio la timu yake pindi waliposonga mbele katika nusu fainali ya ligi ya Afrika kusini.
Katika maelezo yake Jeshi la polisi la afrika kusini limesema kwamba Meyiwa ameripotiwa kufariki wakati akiwasili hospitalini.
 
Senzo enzi za uhai wake akifanya vitu uwanjani







Marehemu Senzo akinyaka mpira Bafanabafana ilipoumana na Nigeria

MAN UTD YAIVIMBIA CHELSEA ZATOKA SARE

Mashabiki wa soka wakijiandaa kuingia kushuhudia mpambano

Haikuchukua muda mwingi punde tu baada ya kuanza kwa kipute hicho, mchezaji mkongwe Didier Drogba akawainua mashabiki wa Chelsea baad ya kufunga goli zuri la kichwa.
Goli hili liliweza kudumu hadi dakika za nyongeza za mchezo huo na kuwapa matumaini mashabiki wa timu hiyo kuamini kuwa wangekusanya point zote tatu kutoka kwa Man U.
Dakika ya 93 ya mchezo Mholanzi Robin van Persie akawainua mashabiki wa timu yake pamoja na kocha wake Louis van Gaal baada ya kuisawazishia timu yake kwa shuti kali la guu la kushoto na kufanya matokeo kuwa ni sare ya 1-1 mpaka kipyenga cha mwisho.
Baada ya kupata goli la dakika za lala salama Kocha Louis Van Gaal hajafurahishwa na timu yake ya Manchester United japokuwa vijana hao wa Old Trafford wameweza kuondoka na point moja muhimu katika mchezo dhidi ya Chelsea uliochezwa katika dimba la Old Trafford. '' hatujatumia faida ya kuwa nyumbani na tungeweza kushinda mchezo huu'' alisema Mholanzi huyo.
Goli la kichwa la Didier Drogba liliisaidia Chelsea kushika usukani katika mchezo huo kabla ya Robin van Persie kusawazisha na kuwasaidia vijana
 
Didier Drogba akitupia kambani kwa kichwa goli la kuongoza


Drogba akishangilia


Niacheni jamaniii hapa kazi tuuu

Di Maria akimhadaa Willian


 
Van Persie akitupia goli la kusawazisha


Wachezaji wa Man Utd wakishangilia goli ka kusawazisha dhidi ya Chelsea

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho akisalimiana na kocha wa Man Utd Van Gaal

 
MAN UTD 1-1 CHELSEA