Monday, June 11, 2012

KAMA UNA MOYO MWEPESI DON WATCH DIS!!!!

HII NI KWELI TUPU (18+)

STARS YAWALIZA GAMBIA,SAMATTA KAMA KAWA


Mshambuliaji wa Star Mbwana Samatta"Samagoal" akipiga kichwa langoni mwa Gambia

Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars jana iliwatoa kimasomaso watanzania baada ya kuibugiza Gambia kwa mabao 2-1 katika mchezo mkali uliopigwa katika dimba kuu la taifa jijini Dar es salaam.Gambia ndio walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa mshambuliaji Mustafa Jarju akitupia kambani kwa kichwa.
Wakati Gambia wakiamini wataiadhiri Stars nyumbani hamad...Shomari Kapombe akazifuta ndoto za wagambia kwa kusawazisha goli maridadi akitupia kambani kwa kichwa na kufanya matokeo kuwa 1-1 dakika ya 65 ya mtanange huo.

Mbwana Samatta"Samagoal" kama wanavyomuita mashabiki wa TP Mazembe ya kule jamhuri ya kidemokrasia ya kongo anakokipiga alikuwa mwiba mkali katika mechi hiyo kwa udambwidambwi wake kama kawa akaipepeta ngome ya Gambia kwa kumuadhiri beki wa kushoto kwa vyenga vya maudhi na kumuacha chini,Samatta alimimina krosi maridadi langoni katika mwachemwache ndipo beki wa Gambia akaunawa mpira katika eneo la hatari na mwamuzi bila ajizi akatenga maguu kumi na mbili ya mtu mzima..kama analia Erasto Nyoni akatupia kamba ya pili kwa Stars na ndipo hekaheka ,nderemo,mwachemwache zilipoibuka katika dimba kuu la Taifa..mpaka mwisho wa Mchezo Stars 2-1 Gambia. na Stars imejiweka pazuri katika kampeni za kuwania kushiriki kombe la dunia nchini Brazil 2014.

Kikosi cha Stars

Kikosi cha Gambia


Mbwana Samatta akiwa amewekwa chini baada ya kutaka kuleta madhara langini mwa Gambia


Nyinyi watoto wadogo tuu!!! 


Mwachemwache kati ya Samatta na mabeki wa Gambia


Kambaaaaaaa!! Erasto Nyoni akishangilia pamoja na Samatta baada ya Nyoni kutupia kamba ya pili na ya ushindi ya Stars


Ndio ukubwa kakaa..Ndivyo anavyosema kocha wa Stars Kim Poulsen akimwambia kocha wa Gambia Luciano Mancini baada ya mtanange kumalizika kwa Star kuibuka washindi



EURO 2012,CROATIA YAIDUNGUA JAMHURI YA IRELAND


Goooooooooo, bao la kwanza la Croatia

Goli la pili la Croatia...kazi imeanza!!

Matumaini ya Jamhuri ya Ireland kuvuka hatua ya makundi katika mashindano ya Euro 2012 yalididimia, baada ya kulazwa magoli 3-1 na Croatia katika mji wa Poznan, Poland.
Mario Mandzukic aliweza kufunga kwa kichwa, huku juhudi za kipa Shay Given kuuzia mpira huo zikikosa kufua dafu.
Lakini juhudi za wachezaji wa Jamhuri ya Ireland hatimaye zilifanikiwa, wakati Sean St Ledger aliposawazisha.

Ireland wakisawazisha bao na kuwa 1-1 kabla ya dhahama kuwaangukia


Shabiki wa Jamhuri ya Ireland akiwa katika swaga za aina yake

Hata hivyo, kabla kipenge cha kukamilisha nusu ya kwanza ya mchezo, Nikica Jelavic alibadilisha matokeo, na kuiwezesha Croatia kuongoza 2-1.

Mandzukic aliweza kuandikisha bao la tatu, ambalo mpira uliingia wavuni ukisindikizwa kimakosa na kipa wa Given.

Jamhuri ya Ireland haiwezi kulalamika sana kuhusiana na matokeo ya mechi hiyo, kwani ilikuwa wazi timu yao bado haijajiandaa vyema.

Kabla ya mechi, mashabiki wengi kutoka Jamhuri ya Ireland walikuwa na matumaini ya kufanya vyema katika mechi hiyo ya kundi C, lakini uwanjani ilikuwa ni wazi kwamba Croatia ndio timu bora, meneja wao mzoefu, Giovanni Trapattoni, bila shaka itambidi kufanya kazi ya ziada ikiwa Jamhuri ya Ireland itaepuka fedheha katika mashindano hayo.
Croatia vs Ireland

ITALIA NA HISPANIA ZAGAWANA UMASKINI KWA SARE YA 1-1


De Natale akitupia kambani mbele ya Iker Casilas

Mabingwa wa Dunia Uhispania wameanza utetezi wa Kombe lao la ubingwa wa mashindano ya Ulaya kwa sare ya 1-1 dhidi ya Italia katika pambano la kundi C mjini Gdansk.


Barwuah Balloteli akioneshana kazi na Pique

Italia ndiyo iliyotangulia baada ya kipindi cha kwanza kumalizika bila bao lolote kufungwa na alikua Antonio Di Natale aliyeingia badala ya Balloteli kufunga bao katika dakika ya 60.


Mwachemwache za mashabiki wa Italia

Dakika nne baadaye Mabingwa wa Dunia na Ulaya walifumania lango la Italia na licha ya juhudi na umahiri wa Mabeki David Silva alimuona Cesc Fabregas na kumuwekea pasi maridhawa na bila kufanya makosa akaupenyeza mpira kumpita goli wa Italia Buffon.


Fabregas akiiandikia Hispania bao la kuongoza

Matokeo hayo yanaliweka kundi la C wazi ambapo Italia na Uhispania zinaondoka zote zikiwa na pointi moja.
Kabla ya mashindano haya wadadisi walionelea kama Uhispania itakabiliwa na kibarua kigumu kutetea taji lake kutokana na wachezaji wake wengi kuwa wachofu mno. Jumla ya wachezaji 23 wa timu hii ya Taifa wamecheza jumla ya dakika 89,884 katika msimu uliopita ikilinganishwa na wenzao walioshiriki kwa upungufu wa dakika 17,000.


Walinda milango Iker Casillas wa Hispania na Buffon wa Italia wakipeana pongezi kwa kupangua michomo mikali katika mtifuano wa timu zao

Timu mbili zilizomo kwenye kundi la C Jamhuri ya Ireland na Croatia lazima zimeridhishwa na matokeo haya zikiona kua na fursa ya kufanya vyema na uwezekano mkubwa wa kufuzu kutoka michuano ya makundi.
Hispania Vs Italia

EURO 2012 UJERUMANI YAINYANYASA URENO,DENMARK YAIOTEA UHOLANZI

Germany's Mario Gomez (2R) scores a goal against Portugal's Rui Patricio during their Group B Euro 2012 soccer match at the new stadium in Lviv, June 9, 2012. REUTERS/Darren Staples (UKRAINE - Tags: SPORT SOCCER)
Gomez akitupia kambani kwa kichwa

Ujerumani ilianza kampeni yake ya kutafuta kombe la UEFA EURO 2012 kwa ushindi muhimu wa goli moja kwa sifuri dhidi ya Ureno. Nayo Denmark iliiduwaza Uholanzi kwa kuifunga hilo hilo goli moja kwa sifuri.      
Ujerumani iliendeleza sifa yake ya kuanza taratibu vinyang'anyiro vikubwa Jumamosi jioni mjini Lviv, Ukraine. Mchezo wa nguvu, wenye mtiririko ambao ulidhihirishwa na Ujerumani katika fainali za kombe la dunia mwaka wa 2010 nchini Afrika Kusini, kwa mfano, ulikosekana hasa katika kipindi cha kwanza.

Tulia wewe yangu hiyoo!!! Mwachemwache na udambwidambwi kati ya Christiano Ronaldo na Bastian

Jerome Boateng mjerumani mwenye asili ya Ghana akimwaga udambwidambwi

Ni kiungo mshambuliaji pekee Mesut Özil ambaye alionekana kuonyesha ubunifu katika safu ya katikati mwa uwanja kwa upande wa kikosi cha Wajerumani.
Lakini wakati Wajerumani wakishjindwa kuonyesha makali, Ureno nayo ilikuwa katika hali hiyo hiyo. Nahodha Cristiano Ronaldo ndiye aliyejaribu tu kuonyesha umahiri wake na kuitatiza Ujerumani, na chanzo kingine cha hatari kilikuwa mchezaji wa ubavuni Nani.
Bao la Ujerumani lilitokea katika dakika ya 72 kwa njia rahisi. Bastian Schweinsteiger alikuwa amenyimwa krosi safi katika upande wa kulia, wakati alipoipokea nje ya kijisanduku. Krosi yake ilimgonga mchezaji wa Ureno Joao Moutinho na Gomez akatia kichwa safi hadi pembeni mwa lango. Ujerumani na Uholanzi sasa zitarejesha uhasimu wao wa jadi mjini Kharkiv siku ya Jumatano.
Kocha wa Uholanzi Bert van Marwijk anasema hawatavunjika moyo. Kwamba ni lazima waizabe Ujerumani.

Uholanzi yachapwa
Katika mchauno wa kwanza, Uholanzi ilipoteza nafasi chungu nzima za wazi katika kichapo hicho ambacho hakikutarajiwa. Nyota kama vile Robin van Persi, ambaye ni mfungaji bora wa ligi ya Uingereza, na Arjen Robben ndio waliofanya makosa makubwa wakati timu hiyo iliposhindwa kutumia nafasi 28 za goli walizopata.


Mhh tumeumbuka!!!!! Ndivyo anavyotafakari Mshambuliaji wa Uholanzi Arjen Robben

Hatoki mtu hapa!!! mwachemwache kati ya Bendtner wa Denmark na Heitinga wa Uholanzi

Denmark, ambaye ndiye mshindi wa UEFA EURO 1992, ilijipatia goli mojja safi lililotupiwa kambani na Michael Krohn-Dehli katika dakika ya 24 na kujihakikishia ushindi kwenye kundi B.
Awali nchini Poland, shirikisho la soka la Urusi lilishitakiwa na shirikisho la UEFA baada ya ukanda wa video kuonyesha mashabiki wa Urusi wakiwashambulia walinzi wa uwanjani baada ya ushindi wa timu hiyo wa mabao manne kwa moja dhidi ya Jamhuri ya Czech mjini Wroclaw Ijumaa.
Wafanyakazi wanne wa usalama walitibiwa hospitalini. Jopo la nidhamu la UEFA litaisikiliza kesi hiyo dhidi ya Urusi Jumatano ijayo. Linatafuta ushahidi zaidi ili kuchunguza madai ya ubaguzi yaliyofanywa dhidi ya wachezaji wa Czech.
Uholanzi Vs Denmark

Ujerumani Vs Ureno