Robin Van Persie "R.V.P" akitupia kambani goli la kusawazisha dhidi ya Newcastle
Thomas Vermaelen na Sagna wakishangilia goli la pili na la ushindi
Thomas Vermaelen alifunga bao la ushindi katika dakika ya 95 dhidi ya Newcastle, na kupunguza tofauti ya pointi kati yake na Tottenham kuwa ni pointi moja tu.
Tottenham imo katika nafasi ya tatu, na Arsenal inashikilia nafasi ya nne.
Hatem Ben Arfa aliwawezesha Newcastle kupata bao la kwanza katika mechi hiyo ya Jumatatu jioni kwa bao la chini kwa chini, lakini furaha yao ilizimwa hata kabla ya dakika moja kumalizika.
Theo Walcott alimsukumia mpira Robin van Persie, na ambaye alifunga bao lake la 33 msimu huu.Mvutano ulizuka uwanjani baada ya kipenga cha mwisho, kufuatia bao la Vermaelen ambalo liliingia wavuni huku mechi ikielekea kumalizika, na mechi hiyo ikiwa ni ya nne ambayo Arsenal, baada ya kuachwa nyuma, iliweza kujitahidi na kupata ushindi.
Ulikuwa ni ushindi wa kusisimua kwa mashabiki wa Arsenal, timu ambayo imecheza vizuri sana hivi karibuni, hasa ikifikiriwa kwamba majirani Spurs walikuwa na tofauti ya pointi 12 kati yao na Arsenal, kabla ya mechi sita zilizopita.
Arsenal 2-1 Newcastle United