Wednesday, April 18, 2012

REAL MADRID YALA KICHAPO MBELEKO YA WEBB HAIKUFAA


Frank Ribbery akiipatia Bayern bao la kuongoza kwa shuti kali

Bao lililofungwa katika dakika za mwisho na Mario Gomez iliiweka Bayern Munich kifua mbele kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Real Madrid katika dimba la Allianz Arena mjini Munich Ujerumani ambapo ndipo kipute cha fainali cha ligi ya mabingwa kitarindimishwa.
Ushindi huo ni katika duru ya kwanza ya mechi ya nusu fainali ya kombe la mabingwa bara ulaya.
Mshambuliaji matata Franck Ribery alikuwa wa kwanza kutupia langoni mwa Real Madrid pale alipofumua mkwaju mkali wa chinichini na kumuacha kipa Iker Casillas akiwa hoi bin taaban.
Katika kipindi cha pili iliwachukua dakika 10 tu Real kurudisha matumaini ya kurudi tena Allianz Arena katika fainali pale Mesut Ozil akiwa hauta chache toka langoni aliipatia bao lake mnamo dakika ya 55.

Ozil na Ronaldo wakishangilia goli la kusawazisha


Wakati watazamaji wakidhania mpambano huo mkali ungeishia kwa sare, hamad! Gomez akachafua hali ya hewa kwa Real Madrid pale alipotupia kambani msumari wa mwisho na wa uchungu kwa Real katika dakika za mwisho.

Gomez akipigilia msumari wa pili

Kabla ya kufunga bao hilo Gomez alipoteza nafasi nyingi za kufunga,huku Webb refa wa mchezo huo akimnyima penati ya dhahiri baada ya Gomez kuangushwa na wachezaji watatu ndani ya eneo la hatari la Real Madrid.

Christian Ronaldo akiwa hoi bin taaban kwa kichapo

Hata hivyo mwamba wa Real Madrid Cristiano Ronaldo hakua na siku njema kwani hakuna kubwa alilofanya akiwa uwanjani bali alikuwa anambwelambwela tu na mpaka kipyenga cha mwisho Bayern 2-1 Real Madrid.

Jinsi Gomez alivyoangushwa eneo la hatari lakini Webb akaipotezea.
BAYERN 2-1 REAL MADRID

AMIN-NI WEWE

AMIN-NI WEWE

WASHINDI WA TUZO ZA KILI MUSIC AWARD 2012













Amin, Charles Baba na Barnaba wakitumbuiza pamoja katika sherehe za utoaji tuzo za muziki katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam

Mtumbuizaji bora wa kike ni Isha Mashauzi

Isha Mashauzi akiwa na tuzo yake ya Mtumbuizaji bora wa kike

Mtumbuizaji bora wa kiume ni Diamond

Diamond akiwa amepakatia tuzo yake

Mwimbaji bora wa kiume ni Barnaba,

Barnaba akipokea tuzo kutoka kwa Adam mchovu

Mwimbaji bora wa kike ni Lady Jaydee

Gadner akichukua tuzo ya mwimbaji bora wa kike kwa niaba ya mke wake Lady Jay Dee

Wimbo bora wa Taarabu ni Full Stop wa Khadija Kopa













Khadija Kopa akitoa burudani akipewa support na wanawe

Wimbo bora wa mwaka ni Hakunaga wa Sumalee











Mwakilishi wa Suma Lee Bab Tale akipokea tuzo ya wimbo bora wa mwaka HAKUNAGA
Suma Lee-Hakunaga

Wimbo bora wa kiswahili wa bendi ni Dunia daraja wa African Stars

Luiza Mbutu akiwa na tuzo ya wimbo bora wa kiswahili wa bendi iliyoenda kwa Afrikan Stars na wimbo Dunia Daraja
Afrikan Stars-Dunia Daraja


wimbo bora wa R&B Number one fan wa Ben Pol












Mwakilishi wa Ben Paul akiwa na tuzo ya wimbo bora wa R&B number one fan


wimbo bora wa Hiphop ni Mathematics.

Wimbo bora wa Reggae ni Arusha Gold – Warrior from the East













Khadija Mwanamboka na Ally Remtullah wakikabidhi tuzo ya wimbo bora wa Reggae kwa msanii wa Warrior from East

wimbo bora wa Ragga/Dancehall ni Maneno maneno wa Queen Darleen ft Dully Sykes
















Queen Darlin akitumbuiza wimbo bora wa Dancehall maneno maneno

Repa bora wa mwaka wa bendi ni Kalidjo Kitokololo














Rapa bora wa bendi Kalidjo Kitokololo akipokea tuzo kutoka kwa Sinta

Msanii bora wa hiphop ni Roma














Prof Jay na Said Fella wakimkabidhi Roma tuzo ya msanii bora wa Hip Hop

Wimbo bora wa Afrika mashariki ni Kigeugeu wa Jaguar


Mwakilishi wa msanii kutoka Kenya Jaguar akipokea tuzo ya wimbo bora wa afrika mashariki kigeugeu
Jaguar-Kigeugeu



Mtunzi bora wa mwaka ni Diamond














Diamond akiwashukuru wapenzi wake baada ya kupokea tuzo

Producer bora ni Maneck

Maneck akijiandaa kupokea tuzo ya mtayarishaji bora wa muziki wa mwaka

Video bora ya muziki ya mwaka ni Moyo wangu ya Diamond.














Diamond akipokea tuzo ya video bora ya mwaka
Diamond-Moyo wangu


Wimbo bora wa Afro pop ni hakunaga wa Sumalee

wimbo bora wa Zouk/Rhumba ni Dushelele ya Ally Kiba

Alikiba akiwashukuru wapenzi wake kwa kupata tuzo ya wimbo bora wa Zouk/Rhumba Dushelele pembeni ni dada yake.
Alikiba-Dushelele


Wimbo bora wenye vionjo vya kiasili ni Vifuu Tundu wa AT ft Mwanne

AT akiwashukuru wapenzi kwa tuzo ya wimbo bora wenye vionjo vya asili Vifuu tundu
AT-Vifuu tundu


Msanii bora anaechipukia ni Ommy Dimpoz













Sharomilionea na mzee Majuto wakimkabidhi Ommy Dimpoz tuzo ya msanii bora anaechipukia

Wimbo bora wa kushirikiana ni Nai Nai wa Ommy Dimpoz ft Ali Kiba


Ommy Dimpoz na Ali Kiba wakiwa na tuzo yao ya wimbo bora wa kushirikiana ambao ni Nainai
Ommy Dimpoz ft Alikiba-Nainai


Hall of fame kwa taasisi imekwenda kwa JKT
watu binafsi ni wanamuziki King Kiki na Remmy Ongala.