Liverpool wakishangilia ubingwa wa Carling
Ilikuwa fainali ya kukata na shoka iliyochezwa kwa muda wa dakika 120 baada ya kukosa mbabe ndani ya dakika 90 na hatimaye mshindi alipatikana kutokana na mikwaju ya penati.
Joe Mason akitia "kambani" goli la kuongoza dhidi ya Liverpool
Martin Skrtel akiisawazishia Liverpool dakika ya 60
Ni miaka sita tangu kuwe na ukame wa vikombe kwa Liverpool na sasa wamekinyaka cha Carling. Mpambano ulianza kwa kasi na Cardiff ndio walikuwa wa kwanza kutikisa nyavu za Liverpool goli likifungwa na Joe Mason, lakini Liverpool walijibu mapigo na kujipatia goli la kusawazisha kwa bao lililofungwa na Skrtel dakika ya 60.
Liverpool vs Cardiff
Dirk Kuyt muuaji wa goli la pili
Katika kipindi cha pili cha dakika za nyongeza Mshambuliaji wa Liverpool Dirk Kuyt, alieingia kuchukua nafasi Andy Carrol alitia kambani na kuipatia Liverpool goli la pili katika dakika ya 108.
Vijana wa Cardiff hawakukata tamaa na zilipotimia dakika 118 mchezaji Ben Turner wa Cardiff alizima ndoto za Liverpool kuibuka mabingwa ndani ya dakika 120 baada ya kutupia kambani baada ya kizaazaa kutokana na kona iliyoelekezwa langoni mwa Liverpool.
Ben Turner akitia kambani baada ya kizaazaa kutokea langoni mwa Liverpool kutokana na Kona
Mashabiki wa Liverpool
Baada ya dakika 120 kukamilika ndipo changamoto ya mikwaju ya penati ilipofikia ambapo Liverpool walifanikiwa kufunga penati 3 zilizotiwa nyavuni na Dirk Kuyt, Glen Johnson na Downing. Waliokosa ni Steven Gerrard na Charli Adam.
Timu ya Cardiff walifanikiwa kutia nyavuni penati mbili zilizopigwa na Don Cowie na Wittingham, na wachezaji waliokosa penati ni Kenny Miller, Rudy Gestede na Anthony Gerrard.
Wachezaji wa Liverpool wakishangilia ubingwa baada ya binamu yake Steven Gerrald,Anthony Gerrald kukosa penati ya mwisho ya Cardiff.