Wednesday, September 12, 2012

HAKUNA KAMA MNYAMA..SIMBA..SIMBA..SIMBA


Nahodha wa Simba Juma K Juma akinyanyua juuu Ngao ya Hisani

Mabingwa wa soka Tanzania Bara, kombe la Urafiki na Super 8 Simba SC wametawazwa rasmi kuwa mabingwa wa Ngao ya Jamii baada ya kuilaza Azam FC kwa mabao 3-2 kwenye mchezo uliopigwa katika dimba kuu la Taifa jijini Dar es Salaam. Mpaka mapumziko, Azam FC walikuwa wanaongoza kwa mabao 2-1, mabao yaliyowekwa kimiani na John Bocco"Adebayor" na Kipre Tchetche wakati la Simba likitupiwa kambani kwa penati na Mghana Daniel Akuffo. Simba walijipatia ushindi katika kipindi cha pili kupitia kwa mshambuliaji hatari hatari, Emmanuel Okwi akisawazisha na kuwa 2-2 na maafa yakapelekwa kwenye kiwanda cha lambalamba na kiungo mstaarabu Mwinyi Kazimoto akitupia kambani bao la tatu na la ushindi. Mpaka mwisho wa mchezo Simba 3, Azam FC 2 na hivyo Simba sports Club ama wekundu wa msimbazi wakiibuyka mabingwa wa Ngao ya Hisani ambapo sehemu ya mapato ya mtanange huo yatapelekwa katika hospitali ya Temeke jijini Dar es salaam.

Ngao ya Hisani


Emmanuel Okwi akijaribu kumchomoka beki kisiki wa Azam Agrey Morris


Homoud wa Azam akimfanyia madhambi mchezaji wa Simba.


Umati wa mashabiki wa soka wa Simba waliofika kushuhudia mtanange huo


Mlinda mlango wa Azam Deogratius Munishi"Dida" akinyaka mchomo wa Akuffor


Mgeni rasmi naibu waziri wa kazi na ajira Makongoro Mahanga akimkabidhi Ngao ya hisani nahodha wa simba Juma K Juma


Sekeseke katika lango la Azam


Sekeseke langoni mwa Simba


Beki wa Simba "Chollo" akiangushwa katika eneo la hatari na mlinda mlango wa Azam "Dida"


Wachezaji wa Simba wakienda mapumziko hapa walikuwa wameshalala 2-1 duuh


Hapa Azam


Hapa Simba