Sunday, May 6, 2012

CHELSEA BINGWA FA


Ramires akitupia bao la kwanza

Chelsea wamechukua ubingwa wa Kombe la FA Cup kwa mara ya saba, kufuatia magoli kutoka kwa Ramires na Didier Drogba dhidi ya Liverpool.

Ramires alifunga kufuatia kosa la Jay Spearing, kabla ya Didier Drogba kufanikiwa kumkwepa Martin Skrtel na kuandikisha bao la pili.


Drogba akishangilia baada ya kutia kambani bao la pili

Liverpool walionyesha mchezo duni hadi Andy Carroll alipofunga bao moja baada ya John Terry kukosa kuimarisha ngome ya Chelsea kikamilifu, na mabao kuwa ni magoli 2-1.


Patashika katika fainali hiyo

Kulikuwa na ubishi kwa muda uwanjani baada ya Carroll kudhani alikuwa amefunga bao la kusawazisha kwa kichwa, na Petr Cech kuutema mpira huo, ambao kwanza uligonga mwamba na kuanguka mbele ya msitari.

Wachezaji na mashabiki wa Liverpool wote walidhani mpira ulikuwa umevuka msitari.
Binafsi kwangu mimi lile lilikuwa goli safi kabisa lakini mbeleko katika soka imoooo!

Wachezaji wa Chelsea wakishangilia na kombe la FA


Drogba na Kalou wakiwa wameposs na kombe la FA


Kocha aliepata mafanikio ya muda mfupi na Chelsea Robert De Matteo