POLAND
Ukraine
Eden Hazard
Klabu ya soka ya England ya Chelsea imetangaza katika tovuti
yake kwamba hatimaye imekubaliana na klabu ya Lille ya Ufaransa kwamba mchezaji
wa kimataifa ya Ubelgiji, Eden Hazard, atajiunga na klabu hiyo ya Stamford
Bridge msimu ujao. Mchezaji huyo, mwenye umri wa miaka 21, tayari afya yake
imekaguliwa na klabu ya Chelsea, na imeonekana hana tatizo lolote.
Walipochukua ubingwa wa ligi ya klabu bingwa, nilijiuliza, "Kwa nini sio
Chelsea?", alisema Hazard.
"Kulikuwa na mvutano kati ya Chelsea na Manchester united, lakini binafsi
naona Chelsea ndio mradi bora zaidi. Ni klabu cha ajabu."
Eden Hazard
Inaarifiwa kwamba Chelsea wameamua kutoa pauni milioni 32 kumpata kijana
huyo, na ambaye akizungumza na kituo cha redio cha nchini Ufaransa, RMC,
aliongezea: "Chelsea ni timu changa, na nitakuwa na nafasi bora zaidi ya
kucheza."
"Ikiwa nitajitahidi kucheza vyema nikiwa Chelsea, huenda nikapata nafasi
katika timu."
Hazard awapo uwanjani shughuli yake ni pevu kama inavyoonekana pichani amekusanya Vijiji
Hazard alikuwepo katika kikosi kilichoshinda ligi wakati Lille ilipopata
ubingwa mwaka 2010-11 na katika msimu wake wa mwisho, alifanikiwa kufunga magoli
21 katika mechi 48.
Katika mechi yake ya mwisho dhidi ya Nancy mwezi uliopita, alifanikiwa kupata
hat-trick (magoli matatu) wakati timu yake ilipocheza dhidi ya Nancy.
Lakini alishindwa kuvuma wakati Ubelgiji iliposhindwa na England katika mechi
ya kirafiki Jumamosi iliyopita.
Hiyo ilikuwa ni mara yake ya 28 kuichezea timu yake ya taifa ya Ubelgiji.
Hazard sasa ni mchezaji wa pili kusajiliwa Chelsea tangu dirisha la usajili
la mwezi Januari, wa kwanza akiwa ni mchezaji wa kimataifa wa Ujerumani, Marko
Marinas.