Hii ilikuwa katika mechi dhidi ya Man City..shabiki uzalendo ulipomshinda na kuanza kumporomoshea mitus kocha wa Man United 'The Chosen One'' David Moyes.
Manchester City iliendelea kujiimarisha na kuikosesha amani klabu ya Manchester United katika ligi kuu ya premier.
Sio hilo tu bali Man City wanaongeza shinikizo kali kwa Chelsea walio juu kwenye jedwali la ponti katika ligi hiyo. Man Uinted walipata kichapo cha mbwa cha mabao matatu bila nyumbani Old Trafford. Edin Dzeko alitupia mabao mawili katika kila
kipindi kwa City hapo jana huku Yaya Toure akizidisha machungu kwa bao
la tatu mwishoni mwa mechi bila jibu kutoka kwa Man United. Sasa vijana hao wa City wanashikilia nafasi ya pili nyuma ya Chelsea.