Thursday, March 1, 2012
SCOTT PARKER AKABIDHIWA MIKOBA ENGLAND AWAPIKU GERRALD,MILNER NA JOE HART
Scott Parker nahodha mpya wa England
kiungo wa klabu ya Tottenham Scott Parker ataongoza Timu yake ya taifa kama nahodha kwa pambano la kirafiki dhidi ya Uholanzi kwenye uwanja wa Wembley.
Kocha msimamizi Stuart Pearce amemteua Parker badala ya orodha yenye majina kama Steven Gerrard wa Liverpool na James Milner wa Manchester City na Joe Hart.
Parker, mwenye umri wa miaka 31, ameiwakilisha Timu ya Taifa mara 10 tangu mwaka 2003 na mwaka 2011 alijitokeza mara saba katika mechi 9.
Mapema wiki hii alichaguliwa na mashabiki kama mchezaji bora wa mwaka jana nchini England.Scott Parker ni mcheza kiungo anayetumia maguvu na ngwara, na ni mwaka jana nyota ya mchezaji huyu iliposhamiri mno.
Kati ya mwaka 2003 na 2010, aliweza kuichezea Timu ya Taifa mara tatu ingawa alihama mara tatu kutoka vilabu - Charlton, Chelsea na Newcastle.
Mwaka jana baada ya kuibuka mchezaji bora wa wandishiw a habari za soka kwa mchango wake kwa klabu ya West Ham iliyoshuka daraja alijiunga na klabu ya Tottenham kwa kitita cha pauni £5.5m.
Katika pambano la hivi karibuni mchezaji huyu alionyeshwa kadi mbili za njano kwa utumiaji wake nguvu wakati wa pambano lenye sifa ya uhasama mkubwa wa vilabu viwili vya eneo la kaskazini mwa London, Arsenal na hivyo hatoshiriki pambano muhimu la klabu yake dhidi ya Manchester United siku ya jumapili ijayo.
KUELEKEA KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA, KENYA KIDEDEA, UGANDA, TANZANIA HOHEHAHE
Dennis Odhiambo wa Kenya akichuana vikali na Segbefia Rince(14) wa Togo katika mechi ambayo Kenya iliibamiza Togo 2-1
Katika michezo, matokeo ya mechi zilizochezwa leo katika kinyanganyiro cha kuchuja Timu zitakazoshiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika huko Afrika kusini"BONDENI" mwaka 2013, Madagascar imechapwa na Cape Verde 4-0.
Tanzania ikalazimishwa sare ya 1-1 na Msumbiji mjini Daresalam.Rwanda ikaibania Nigeria kwa kutoa suluhu 0-0, Ethiopia ikatoa sare ya 0-0 na Benin mjini Adis Ababa.Burundi ikaichapa Zimbabwe 2-1 mjini Bujumbura. Mjini Nairobi, Kenya ikafanikiwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Togo. Mjini Ndjamena Chad ikaitoa Malawi 3-2. Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ikaanza vizuri kampeini kwa kuinyunyizia Ushelisheli 4-0. Juhudi za Uganda katika kipindi cha kwanza kuishinikiza Congo Brazzaville mjini Brazaville ziliichosha na kuchapwa 3-1.
Katika michuano kama hio kwa bara Asia, Saudi Arabia imeondolewa katika michuano ya Kombe la Dunia la mwaka 2014 kwa kipigo cha mabao 4-2 na Australia huku Oman ikisonga mbele kuingia hatua za mwisho za Timu kutoka bara Asia.
Timu nyingine ngumu kutoka eneo hilo Korea ya kusini imepona aibu kama Saudi Arabia kwa kuichapa Kuwait 2-1 na Qatar ikapata bao la dakika za majeruhi kusawazisha mawili ya Iran licha ya Bahrain kuinyunyizia Indonesia mabao 10-0.
Bahrain ilihitaji mabao 8 na Qatar ipoteze mechi yake ili iweze kusonga mbele lakini Qatar ilijizatiti na kupata mabao mawili dhidi ya IRAN ambayo tayari ilikua imeisha fuzu
Subscribe to:
Posts (Atom)