Vidic akiifungia Manchester bao dhidi ya Bayern
Tulia weweeeeee
Kulikuwa na mechi mbili za mkondo wa kwanza wa robo
fainali ya ligi kuu ya mabingwa barani Ulaya iliyochezwa Jumanne usiku,
Manchester United ya Uingereza ikikabana koo na mabingwa watetezi waligi
hiyo Bayern Munich ya Ujerumani.
Nayo Barcelona ya Uhispania ikikabiliana na Athletico Madrid vilevile ya Uhispania.Wachezaji wa Man U wakishangilia bao
Licha ya kuwa Bayern Munich ilikuwa imepigiwa upatu kutamba dhidi ya Manchester United vijana wa pep Gardiola walikabiliwa na ukuta mrefu wa Manchester uwanjani Old Traford.
Na walipopata fursa nahodha wa Manchester Nemanja Vidic alifunga bao maridadi la kichwa baada ya kuunganisha vizuri kona kutoka kwa Wayne Rooney kunako dakika ya 58 ya kipindi cha pili.
Gonga gonga ya Wajerumani ilikosa kuzaa matunda lakini bao la Bastian Schweinsteiger kunako dakika ya 66 iliwatunuku mabingwa hao wao watetezi bao muhimu la ugenini kabla ya mkondo wa pili utakaochezwa huko Ujerumani .
Bila shaka mashabiki na watani wa kocha David Moyes watakubaliana naye kuwa United itajutia fursa aliopoteza Danny Welbeck alipokuwa ni yeye pekee dhidi ya kipa wa Bayern Manuel Neuer .
United vilevile itamshukuru kipa David de Gea aliyefanya kazi ya ziada kuzuia mashambulizi haswa kutoka kwa Arjen Robben.
Kutokana na sare hiyo sasa mkufunzi Pep Guardiola ana kibarua kigumu pale Man United itakapozuru uwanja wa Allianz Arena wiki ijayo.
Mechi nyingine 2 zimeratibiwa kuchezwa baadaye Jumatano, Real Madrid ya Uhispania ikivaana na Borussia Dortmund kutoka Ujerumani nayo Paris st Germain ikiikaribisha wawakilishi wengine wa Uingereza Chelsea ya Uingereza Katika uwanja wa Parc des Princes.
ATLETICO YAIVIMBIA BARCA
Messi akijaribu kumhadaa Gabi
Messi akikokota kijiji
Vita vya mahasimu wa nyumbani Atletico Madrid na Barcelona viliishia sare ya nne msimu huu timu hizo mbili za Uhispania zilipotoka sare ya moa kwa moja katika mkondo wa kwanza wa
ligi kuu ya mabingwa barani Ulaya iliyochezwa katika uwanja wa Camp nou.
Atletico inayoongoza katika dimba la nyumbani ya la Liga sasa imejipatia bao muhimu la ugenini licha ya kuwa ilifuzu kuingia katika robo fainali hizo kwa mara ya kwanza tangu mwaka wa 1997.
Licha ya barcelona kupigiwa upatu kushinda taji hilo ni Atletico iliyofunga ya kwanza kupitia kwa kiungo Diego aliyekuwa ameingia kuchukua nafasi yake Diego Costa aliyelazimika kuondolewa uwanjani
Neymar akishangilia goli
baada ya kupata jeraha katika dakika ya 30.
Barca ilijifurukuta na kufunga baada ya Andre Iniesta kupenyeza pasi safi katikati ya ulinzi mkali wa Atletico iliyopokelewa na Neymar aliyesawazisha zikiwa zimesalia dakika 20 mechi hiyo kukamilika.
Juhudi za Barcelona za kutafuta bao la Ushindi ziliambulia patupu ngome ya ulinzi ya Atletico ilipoimarishwa na mambo yakasalia kuwa sare .
Athletico inaongoza ligi ya nyumbani kwa alama moja zaidi ya Barca.