Mnamo 13 mwezi May jenerali mmoja wa jeshi alitangaza katika
redio ya taifa kwamba rais wa Burundi amepinduliwa na kwamba serikali ya
mpito itabuniwa.Lakini msemaji wa rais alikana habari hizo akidai kuwa
kulikuwa na usaidizi mdogo katika jeshi kwa mapinduzi kutendeka.Rais
Nkurunziza alidaiwa kurudi nchini Burundi kutoka Tanzania ,lakini
imethibitishwa kuwa leo, alishindwa kufanya hivyo na kwamba yungali
nchini Tanzania.
Kiongozi wa kundi la kiraia linalopinga hatua ya rais Nkurunziza
kuwania muhula wa tatu amewataka raia nchini humo kuendelea na
maandamano kulingana na shirika la habari la AFP.
Vital
Nshimiriman amesema kuwa licha ya kundi hilo kupinga jaribio hilo la
mapinduzi,vile raia walivyowashangilia wanajeshi wa jaribio hilo
kulionyesha kwamba kuna hamu kubwa ya mabadiliko.
Nukuu muhimu kutoka kwa Gervais Abayeho,msemaji wa rais Pierre
Nkurunziza akizungumza na kipindi cha BBC cha Newsday.''Mapinduzi
hushirikisha watu wengi Kuna wanajeshi wa nyadhfa za chini ambao
wamesalimu amri na ambao wanawasaidia maafisa wa poisi na uchunguzi
wao,lakini ninaamini watu waliopanga mapinduzi hayo ,wale viongozi hilo
ni swala jingine ni lazima washtakiwe.hakuna mgawanyiko katika
jeshi.Iwapo unaweza kuwaangalia wale waliokuwa wakipanga kutekeleza
mapinduzi ni wachache ...kundi dogo la jeshi'',alisema..
Majenerali wawili waliotekeleza jaribio la mapinduzi nchini Burundi dhidi ya rais Pierre Nkurunziza wamekamatwa.
Hatahivyo kiongozi wa mapinduzi hayo jenerali Godefroid Niyombare ametoroka na anasakwa kulingana na msemaji wa rais.
Awali
Jenerali Niyombare alikiambia chombo cha habari cha AFP kwamba yeye na
wafuasi wake watajisalimisha akiongezea kuwa ''natumai hawatatuua''.
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amesema kuwa amerudi nchini Burund na kwamba anatarajiwa kulihutubia taifa.