Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, anatarajiwa kuwa
nyota wake aliyesajiliwa kwa kitita cha pauni milioni 42, atarejea katika
hali yake ya kawaida na kuonyesha mchezo mzuri, baada ya matokeo mabaya
wikendi iliyopita.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, kutoka
Ujerumani,Metsut Ozil hajatupia kambani katika mechi nane zilizopita huku akiwa
amechangia kupatikana kwa magoli mawili pekee katika mechi hizo.Metsut Ozil
Lucas Podolski
Ozil, ambaye alijiunga na Arsenal, kutoka kwa klabu ya Real Madrid Septemba mwaka uliopita, alianza vyema kwa kufunga magoli manne na kuchangia magoli sita katika mechi zake kwanza kumi na mbili za ligi kuu.
Lakini mcheza kiungo huyo, alishutumiwa vikali kufuatia mchezo aliouonesha wakati Arsenal ilipovurugwa magoli 5-1 na Liverpool, hali iliyomlazimu Wenger kumuondoa kunako dakika ya sitini na moja.
Akiongea kabla ya mechi yao katika Uwanja wa Emirates siku ya Jumatano usiku, Wenger alisema kuwa anadhani David Moyes anaweza kufanikiwa kama kocha wa United ikiwa atapewa muda.
Van Persie
Wayne Rooney
Julai mwaka uliopita, Moyes aliteuliwa kuchukua mahala na Sir Alex Ferguson ambaye alistaafu kama kocha wa Manchester United baada ya kushinda ligi kuu ya Premier mara 13 katika kipindi cha miaka 27, lakini amekuwa na kibarua kigumu kufuata nyayo za Ferguson.
Manchester United inashikilia nafasi ya saba kwenye msururu wa ligi kuu na alama 41 na hata ikishinda mechi yake dhidi ya Arsenal, Vijana hao wa Moyes watasalia katika nafasi hiyo hiyo.