Tuesday, June 19, 2012

NI AJABU NA KWELI


Katika Picha hii kuna maajabu wajameni, Fuata hatua mbili zifuatavyo ujionee maajabu;

1- Tazama kidoti cha njano puani kwa jamaa kwa sekunde 10
Halafu.....
2- Tazama sehemu ya kulia ambayo haina picha

Ni Vijimambo tu vya utaalamu wa wataalamu wa mambo.

BURUDANI LEO-NIGHT CLUB MAREKANI

WAKATI TANZANIA INALIA NA MFUMUKO WA BEI, KABEJI MOJA CANADA INAUZWA DOLA 27


Je, unaweza kununua kabeji moja kwa dola 27 au kuku mmoja kwa dola 65, au maji ya lita kumi na mbili kwa dola 100? Hiyo bila shaka sio gharama ya mlo mmoja katika hoteli ya kifahari, lakini ndio bei ya vyakula muhimu katika maduka makubwa jimbo la Nunavut, kaskazini mwa Canada.

Wenyeji wa Iqaluit, mji mkuu wa jimbo hilo na wale wa Arctic Bay, Pond Inlet na Igloolik, pamoja na watu waliokerwa na bei hizo katika maeneo mengine nchini Canada, wamekuwa wakiandamana katika juhudi zao kuonyesha kero lao la bei ghali ya chakula katika maeneo ya vijijini.
Sasa kwa nini bei ya chakula ni ghali hivyo?

Nunavut ni mji ulio na ukubwa sawa na eneo zima la Magharibi mwa Uropa na eneo hilo limekalia sehemu kubwa Arctic iliyoko Canada lililo na watu 30,000.

Hali ya hewa ni mbaya na ukiwa unaishi maeneo ya kaskazini ina maana kuwa hakuna viwanda vya kilimo.

Vyakula vyote lazima vifikishwe katika eneo hilo kwa ndege kila siku kutoka sehemu zingine za nchi .

Kabla ya kuwasili kwa watu wa bara Uropa wenyeji wa sehemu hizo walitegemea uwindaji na uvuvi.

Lakini mabadiliko katika mfumo wa maisha una maana kuwa sasa watu wanategemea sana chakula kutoka nje na kwa muda mrefu watu wa maeneo hayo wanaweza tu kufikiwa kwa ndege.

"hatuna barabara zozote au njia za reli kutoka maeneo ya kusini kwa hivyo inabidi chakula kuletwa hapa kwa ndege kila siku," anasema Madeleine Redfern, meya wa mji mkuu wa, Iqaluit. "chakula muhimu kama maziwa na mkate huletwa hapa kila siku na wala sio sana katika sahemu zingine zilizo mbali kutoka hapa."

Michael McMullen, makamu wa rais wa kampuni ya North West ambayo ina maduka 32 katika maeneo ya vijijini nchini Canada, anasema kuwa kusafirisha chakula hadi kwenye maduka hayo, inagharimu mara kumi na moja zaidi kuliko maeneo ya Kusini. Anasema inagharimu doka 104.99 kufungisha maboksi ya chupa za maji ikizingatiwa gharama hiyo ni kabla ya kuzisafirisha.

"Usafirishaji pekee unatugharimu asilimia 13 ya gharama zote tunazotumia" alisema McMullane.

"Pia inatugharimu sana wakati tuzingatia mambo mengine kama umeme"

mboga ya kabeji

"Sio rahisi kusafirisha chakula, tunapata hasara kubwa zaidi wakati wa usafirishaji kulekea kaskazini kuliko maneo ya Kusini." aliongeza McMullen
Kulisha familia yangu.

Wakati bei ni nafuu kutuma chakula kinachoweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu kwa meli msimu huu nayo ina matatizo yake. "Kuna tatizo na uhifadhi wa vyakula hivyo" alisema bi Redfern. "tafakari tu kuleta hapa karatasi za kutumia vyooni yatakayotumika kwa mwaka mmoja kwa kwa watu wa hapa, ni pesa nyingi "

Leesee Papatsie, aliyeandaa maandamano hayo anayeishi eneo la Iqaluit, ana kazi nzuri lakini bado anatumia zaidi ya thuluthi moja ya mshahara wake kwa chakula, takriban dola 500- 600 kwa wiki.

"Chakula kina bei ghali sana" alisema mama huyo. " Mimi sijagutushwa na bei hiyo, angalau nimeishi katika mji mkubwa , katika miji midogo maisha huwa ghali"

Mshahara mdogo zaidi unaolipwa hapa Nunavut ni dola kumi na moja kwa saa, lakini kwa sababu ya bei ghali na mfumuko wa bei, ina maana kuwa pesa hizo ni kidogo sana kuweza kununua chochote kikubwa. Pia kuna ukosefu mkubwa wa ajira hapa inafika asilimia 16.

Afisaa mkuu wa umoja wa mataifa kuhusu haki ya chakula, Olivier De Schutter,hivi karibuni wakati wa ziara yake nchini Canada, alisema kuwa kati ya watu milioni mbili hadi milioni tatu nchini humo, hawawezi kumudu lishe wanayohitaji kuishi maisha mazuri yenye afya nzuri.

Alisema kuwa watu milioni moja na wengine 55,000 wa mji, wako katika hali mbaya.

Wenyeji wengi wa kusini mwa Canada wamekuwa wakiuliza ikiwa wenyeji huwinda na kutafuta chakula msituni ili kuweza kuepuka bei ghali ya chakula.

"Kuwinda na kutafuta chakula ni muhimu" alisema bi Redfern, lakini wakati mwingine inakuwa vigumu hata kupata chakula wakati wa shughuli ya uwindaji.

ITALIA YATINGA ROBO FAINALI EURO 2012 BALOTELLI ATUPIA



Balotelli akitupia kambani bao la pili na la ushindi

Cassano akiwa hewani na kupiga kichwa kilichazaa bao la kwanza la Italia

Italia ilipata ushindi dhidi ya timu ya Jamhuri ya Ireland ambayo tayari wachezaji wake walikuwa tayari wameshafungasha virago kuondoka kutoka mashindano ya Euro 2012, kwa kuwafunga magoli 2-0.

Jamhuri ya Ireland walianza mchezo huo wa Jumatatu usiku, wakithibitisha nia yao ya kujitahidi kupata ushindi, lakini Antonio Cassano, mchezaji wa Italia, ndiye aliyefanikiwa kuliona lango la Ireland akitupia kambani kwa kichwa kufuatia mpira wa kona iliyopigwa na Andrea Pirlo.

Irish Forward Kevin Doyle (L) Vies AFP/Getty Images
Hapa kazi tu!!! Thiago Motta wa Italia akichumpa hewani huku chini ni Kevin Doyle wa jamhuri ya Ireland
 
Iwapo Ireland ingelisawazisha, kama alivyokaribia kutupia kambani Keith Andrews lakini kipa wa Italia Gianluigi Buffon alikuwa imara kuokoa mchomo wake, ingelimaanisha Italia, katika kundi C, wangelijikuta wametupwa nje ya mashindano hayo ya Ulaya, hasa kama Croatia ingelipata bao la kusawazisha dhidi ya Uhispania, mechi iliyochezwa sambamba na hii, na iliyokwisha kwa ushindi wa Italia wa bao 1-0.

Andrews aliamrishwa na mwamuzi kuondoka uwanjani, baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya manjano, na Mario Balotelli akafanikiwa kutupia bao la pili na kuwatuliza mashabiki wa Italia.
Kutokana na Uhispania kuishinda Croatia, sasa itakutana na mshindi wa kundi D.
England ni miongoni mwa mataifa katika kundi hilo.
Kamba ya Balotelli

EURO 2012 JESUS AIPELEKA SPAIN ROBO FAINALI


Jesus Navas akitupia kambani goli la pekee na la ushindi

Jesus Navas alikuwa ni mkombozi wa timu ya Uhispania, pale alipotupia kambani dakika za lala salama dhidi ya Croatia, na kuiwezesha nchi yake kufuzu katika hatua ya robo fainali za mashindano ya Euro 2012.


Nakuja kwako Modric.........Andre Iniesta"fundi" akiwa amekusanya kijiji cha wa-croatia

Ilielekea kana kwamba mabingwa watetezi Uhispania walikuwa wakicheza mechi hiyo ya Jumatatu usiku kwa wasiwasi.
Hata hivyo Jesus, ambaye ni mchezaji wa Seville ya Uhispania, aliweza kupenyezewa pande maridadi na Andres Iniesta, na zikiwa zimesalia dakika mbili kabla ya mechi kumalizika, alifanikiwa kuipatia Uhispania bao, na kuwahuzunisha mashabiki wa Croatia.

Bao hilo moja lilihakikisha Uhispania inaongoza kundi la C.
Uhispania walicheza karata yao vyema, kwani kwa kumtoa Fernando Torres na mahala pake kuingia Jesus Navas, ni mchezaji huyo wa zamu aliyeweza kutupia kambani.

Sasa mabingwa watetezi wanasubiri kujua kama watakutana na England au Ufaransa katika timu nane ambazo zitasalia kucheza robo fainali.
A Croatian Football Fan Reacts AFP/Getty Images
Mhh ishakuwa sooo!!! shabiki wa Croatia akiwa amelowa baada ya chama lake kuchapwa na Spain

Croatian Midfielder Ivan Perisic (L) Vies AFP/Getty Images
Iniesta akifanya udambwidambwi

Croatian Midfielder Luka Modric Controls AFP/Getty Images
Luka Modric akituliza ngozi mbele ya Xavi

Fans Of Croatia's National Football Team  React At The End Of The Euro 2012 Football Championships AFP/Getty Images
Kichapo ni noma asikuambie mtu, mashabiki wa Croatia wakisononeka kwa machungu kufuatia kamba ya Jesus dakika za lala salama

Fans Of Croatia's National Football Team  React At The End Of The Euro 2012 Football Championships AFP/Getty Images
Shabiki wa Croatia akimnyamazisha mwenzake alieangua kilio uwanjani baada ya kichapo cha bao 1 kwa 0 kutoka kwa Spain katika dimba la Gdansk Arena

Fans Of Croatia's National Football Team React At The End Of The Euro 2012 Football Championships AFP/Getty Images
Jikaze babaaa ndio mpira huoo

A Fan Of Croatia's National Football Team Reacts AFP/Getty Images
A Fan Of Croatia's National Football Team Reacts AFP/Getty Images
A Fan Of Croatia's National Football Team Reacts AFP/Getty Images
Croatian Defender Ivan Strinic Reacts AFP/Getty Images
Croatian Defender Vedran Corluka  Reacts AFP/Getty Images
Wachezaji na mashabiki wa Croatia wakiwa katika majonzi mazito baada ya kushindwa kutinga robo fainali ya mashindano ya EURO 2012