Balotelli akitupia kambani bao la pili na la ushindi
Cassano akiwa hewani na kupiga kichwa kilichazaa bao la kwanza la Italia
Italia ilipata ushindi dhidi ya timu ya Jamhuri ya Ireland ambayo tayari wachezaji wake walikuwa tayari wameshafungasha virago kuondoka kutoka mashindano ya Euro 2012, kwa kuwafunga magoli 2-0.
Jamhuri ya Ireland walianza mchezo huo wa Jumatatu usiku, wakithibitisha nia yao ya kujitahidi kupata ushindi, lakini Antonio Cassano, mchezaji wa Italia, ndiye aliyefanikiwa kuliona lango la Ireland akitupia kambani kwa kichwa kufuatia mpira wa kona iliyopigwa na Andrea Pirlo.
Hapa kazi tu!!! Thiago Motta wa Italia akichumpa hewani huku chini ni Kevin Doyle wa jamhuri ya Ireland
Iwapo Ireland ingelisawazisha, kama alivyokaribia kutupia kambani Keith Andrews
lakini kipa wa Italia Gianluigi Buffon alikuwa imara kuokoa mchomo wake, ingelimaanisha Italia,
katika kundi C, wangelijikuta wametupwa nje ya mashindano hayo ya Ulaya, hasa
kama Croatia ingelipata bao la kusawazisha dhidi ya Uhispania, mechi iliyochezwa
sambamba na hii, na iliyokwisha kwa ushindi wa Italia wa bao 1-0.
Andrews aliamrishwa na mwamuzi kuondoka uwanjani, baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya manjano, na Mario Balotelli akafanikiwa kutupia bao la pili na kuwatuliza mashabiki wa Italia.
Kutokana na Uhispania kuishinda Croatia, sasa itakutana na mshindi wa kundi D.
England ni miongoni mwa mataifa katika kundi hilo.
Kamba ya Balotelli
No comments:
Post a Comment