Arsenal waliizabua Swansea kwa bao 1-0 katika dimba lao la Emirates mpambano ukishuhudiwa na watazamaji wapatao 58,359. Umati huo ulishuhudia mpambano mkali ambao ulitawaliwa zaidi na timu ya Arsenal huku wakikosa magoli mengi katika mpambano huo. Baada ya kosakosa nyingi katika dakika ya 85 wakati jua likielekea magharibi ya roho sio mwingine bali ni kipenzi cha waingereza Jack Wilshere aliewainua vitini mashabiki wa Arsenal kwa kutupia kambani goli pekee na la ushindi kwa mkwaju mkali uliomshinda Vorm mlinda mlango wa Swansea.
Mpaka mwamuzi wa mchezo huo Clattenburg anapuliza kipyenga cha mwisho matokeo yalikuwa Arsenal 1-0 Swansea. Kwa matokeo hayo Arsenal wameitupa nje ya kombe la FA timu ngumu ya Swansea na kupenya raundi ya nne.
Wilshere akifumua nduki iliyotinga moja kwa moja kambani kuandika bao la Arsenal
Wilshere akilipuka kwa furaha baada ya kufunga goli dhidi ya Swansea
Patashika langoni mwa Swansea
Vikosi vilikuwa;
Arsenal
- 01 Szczesny
- 03 Sagna
- 04 Mertesacker
- 05 Vermaelen
- 28 Gibbs
- 02 Diaby (Ramsey - 82' )
- 10 Wilshere
- 14 Walcott
- 19 Cazorla
- 22 Coquelin
- 12 Giroud
Substitutes
- 24 Mannone
- 11 Santos
- 25 Jenkinson
- 15 Oxlade-Chamberlain
- 16 Ramsey
- 23 Arshavin
- 09 Podolski
Swansea City
- 01 Vorm
- 02 Bartley
- 04 Chico
- 21 Tiendalli
- 07 Britton
- 12 Dyer
- 15 Routledge
- 20 De Guzman (Ki Sung-Yeung - 60' )
- 26 Agustien (Pablo - 59' )
- 29 Richards
- 10 Graham (Michu - 71' )
Substitutes
- 25 Tremmel
- 16 Monk
- 33 Davies
- 09 Michu
- 11 Pablo
- 24 Ki Sung-Yeung
- 17 Shechter
Man United nao walifanikiwa kuivurumisha nje ya kombe la FA timu ya Westham baada ya kuibanjua kwa goli 1-0 katika dimba la Old Trafford huku mtanange huo ukihudhuriwa na mashabiki wapatao 71,081. Alikuwa ni Wayne Rooney akiripoti rasmi baada ya kuwa nje ya dimba kwa wiki nne alipotupia kamabni bao la pekee na la ushindi katika dakika ya 8 tu ya mchezo baada ya kupata pande murua kutoka kwa Chicharito.
Rooney akifunga goli dhidi ya Westham
Rooney akipiga penati ambayo iliota mbawa
Carrick akijaribu kuwatoka mabeki wa Westham
Manchester United
- 13 Lindegaard
- 02 Rafael
- 04 Jones
- 12 Smalling
- 28 Buttner
- 07 Valencia
- 08 Anderson (Carrick - 67' )
- 11 Giggs
- 17 Nani (Scholes - 77' Booked )
- 10 Rooney
- 14 Hernandez
Substitutes
- 40 Amos
- 05 Ferdinand
- 16 Carrick
- 22 Scholes
- 26 Kagawa
- 19 Welbeck
- 20 Van Persie
West Ham United
- 22 Jaaskelainen
- 02 Reid
- 05 Tomkins
- 27 Spence Booked
- 33 Potts
- 14 Taylor
- 21 Diame (Collison - 65' )
- 23 Diarra
- 32 O'Neil
- 09 Cole (Nolan - 65' Booked )
- 12 Vaz Te (Lee - 78' )
Substitutes
- 30 Spiegel
- 20 Demel
- 04 Nolan
- 07 Jarvis
- 10 Collison
- 43 Lletget
- 47 Lee
ARSENAL 1-0 SWANSEA
MAN U 1-0 WESTHAM U