Wednesday, May 9, 2012

BURUDANI LEO. WIMBO WA BLAD KEY-VINAPANDA BEI

LIVERPOOL YALIPA KISASI KWA CHELSEA YAIBAMIZA 4-1


Caroll akibinjuka tik-tak mbele ya beki wa Liverpool

Ikiwa ni siku tatu tu baada ya Chelsea kuichapa Liverpool katika fainali ya kombe la FA kwa
Ivanovic aliesimama na Essien alielala wakishuhudia mpira uliopigwa na Suarez na kumgonga Essien ukitumbukia kimiani

magoli 2-1. Hatimaye Liverpool wakiwa katika dimba lao la Nyumbani pale Anfield wamewararua Chelsea kwa kamba 4-1 bila huruma mbele ya mashabiki 40,721 waliohudhuria mtifuano huo.


Luis Suarez akishangilia goli la kwanza la Liverpool

Kiama cha Chelsea kilianza katika dakika ya 18 pale Suarez alipoilamba vyenga ngome ya Chelsea na kuingia na mpira mpaka kwenye eneo la hatari pembeni ya uwanja alipoingiza kati mpira kwa ufundi na ukamgonga Essien na kutumbukia kambani na kuandika bao la kuongoza kwa Liverpool.

Caroll na Henderson wakishangilia kamba ya pili iliyotupiwa na J Henderson

Iliwachukua dakika 24 Liverpool kuendeleza kipigo pale J Henderson alipotupia kambani goli la pili kwa Liverpool na kuwaacha Chelsea wakiwa hawaamini kimbunga kinachowanyemelea.

Mara nyingine tena D Agger katika dakika ya 27 alitupia kambani bao la tatu ambalo kwa kiasi kikubwa liliwanyong'onyesha Chelsea kama sio kuwazorotesha na mbwembwe zote za Ubingwa wa FA zikawatokea puani.

J Hernandes waoooooooooooooooooooo

Mungu sio Athumani mnamo dakika ya 49 mchezaji mwenye juhudi na bidii na ubishi wa kiafrika ingawa ni mbrazili Ramires aliipatia Chelsea bao la kupangusia machozi ya kipigo katika mechi hiyo.


Mtifuano kati ya Terry na Suarez

Wakati kila mtu akiamini kichapo kimefikia mwisho, Golikipa wa akiba wa Chelsea alifanya boko la maana pale alipiga mpira katikati ya uwanja ili hali hayupo golini na ndipo kingekewa cha kupata goli kilipomuangukia J Shevley nae bila ajizi akatupia kambani kwa shuti kali katika dakika ya 60 na kuhitimisha dhoruba kali la mabao 4-1 kwa Chelsea toka kwa Liverpool.
Poleni sana fans wa Chelsea msife moyo mnaweza jipoza kwa Bayern Munich haa haaa haaaaaaa!!!

OKWI, BOBAN NA SUNZU KWENYE REKODI ZA C.A.F ,SIMBA YAIFUATA AL AHLY SHANDY



Emmanuel Okwi

Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho, Simba wanaondoka leo kwenda Khartoum, Sudan tayari kwa mchezo wa marudiono dhidi ya Al Ahly Shendi, washambuliaji nyota wa Wekundu hao wa Msimbazi, Emmanuel Okwi na Felix Sunzu wameingia kwenye rekodi ya wafungaji bora Afrika katika michuano ya Kombe la Shirikisho la soka Afrika.

Haruna Moshi "BOBAN"

Okwi, raia wa Uganda na Felix Sunzu ambaye ni Mzambia, wote wametajwa kuwa na mabao matatu kila mmoja kwa mujibu wa mtandao wa tensport.com.
Mshambuliaji huyo anayechezea pia Uganda Cranes, alifunga bao moja dhidi ya Entente Sportive de Setif katika mchezo wa kwanza kati ya mawili walioshinda mabao 2-0 Dar es Salaam na moja likifungwa na Haruna Moshi.

Felix Sunzu
Mchezo wa marudiano, Okwi alifunga moja wakati Simba ikilala mabao 3-1. Mshambuliaji huyo alifunga dhidi ya Al Ahly Shendi kati ya mabao matatu huku mengine yakifungwa na Boban na Patrick Mafisango.
Kwa hali hiyo, Boban na Sunzu kila mmoja wana mabao matatu. Sunzu aliyafunga katika mchezo walioshinda mabao 2-1 dhidi ya Kiyovu ya Rwanda na lingine likifungwa na Parick Mafisango.
Mbali na wachezaji hao, wengine wenye mabao matatu ni Komara, Niamba wote wa Leopards ya Congo, Chinyengetere (Hwange ya Zimbabwe, Moco (InterClube (Angola) na Raouf (ENPPI, Misri) na Seri wa Asec Mimosa ya Ivory Coast.
Mpaka sasa Fiston (Lydia Academic, Burundi) na Girma wa St George ya Ethiopia wana mabao manne kila mmoja.
Wakati huo huo, msafara wa Simba unaondoka leo mchana kwenda Sudan kupitia Nairobi, Kenya tayari kwa mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Al Ahly Shandy baada ya kukwama kuondoka kutokana na majambazi kuvunja na kuiba katika ubalozi wa Sudan.
Juzi usiku majambazi walivunja sefu ya kuhifadhia fedha na kuiba zaidi ya dola 40,000 ubalozini hapo pamoja fedha nyingine pamoja na kuiba kompyuta zote zinazotumika kuhifadhia kumbukumbu mbalimbali.
Kutokana na hali hiyo, Simba walikwama kupata viza zao juzi na jana na zinataraji kutolewa leo asubuhi kabla ya kuondoka saa 10:00 kwenda Sudan kupitia Nairobi ikiwa na wachezaji wote wa timu hiyo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile alithibitisha juzi kutokea tukio hilo.