Monday, July 25, 2011
AMY WINEHOUSE AFARIKI DUNIA
Mwimbaji maarufu mwanamke wa Uingereza, Amy Winehouse, amekutwa amekufa katika fleti yake mjini London.
Amy amefariki akiwa na umri wa mika 27 tu.
Amy Winehouse alishinda tuzo kadha kwa albamu yake ya pili, Back to Black, ambayo ilitolewa mwaka 2006.
Sababu ya kifo chake haijajulikana.
Lakini mwimbaji huyo amekuwa akipambana na uraibu wa ulevi na mihadarati kwa muda.
Mara nyingi alitokeza kwenye tamasha akiwa amelewa.

BALLOTELI ATOLEWA UWANJANI BAADA YA KUFANYA MZAHA KWA TIMU PINZANI
Mchezaji wa Manchester City Mario Balotelli alitolewa nje katika kipindi cha kwanza katika mechi yao dhidi ya LA Galaxy kwa kutoonyesha heshima kwa wapinzani wake.
Kocha wa Manchester City Roberto Mancini alimpumzisha Balotelli kutokana na tukio hilo lakini wakati akitoka nje ya uwanja alionekana kujibizana na kocha wake.
Awali Balotelli alifunga bao kupitia mkwaju wa penalti katika mechi hio ya kirafiki iliomalizika kwa sare ya 1-1.
Man City Imepata ushindi wake wa tatu katika mechi zake za kujiandaa kwa msimu wa ligi kuu ya England.Katika uwanja huo mashabiki wa LA Galaxy walimzomea Balotteli kwa kitendo chake hicho.
Hii si mara ya kwanza kwa mchezaji huyo wa zamani wa Inter kujikuta katika matatizo na Kocha Mancini, ambaye pia alikuwa kocha wake nchini Italia.
Mancini na Balotelli
Mshambuliaji huyo wa Italia mwenye umri wa miaka 20 alikuwa karibu kufunga goli,lakini hakufunga na badala yake akapiga mpira kwa kisigino na kukosa goli.Kocha wa Manchester City Roberto Mancini alimpumzisha Balotelli kutokana na tukio hilo lakini wakati akitoka nje ya uwanja alionekana kujibizana na kocha wake.
Awali Balotelli alifunga bao kupitia mkwaju wa penalti katika mechi hio ya kirafiki iliomalizika kwa sare ya 1-1.
Man City Imepata ushindi wake wa tatu katika mechi zake za kujiandaa kwa msimu wa ligi kuu ya England.Katika uwanja huo mashabiki wa LA Galaxy walimzomea Balotteli kwa kitendo chake hicho.
Hii si mara ya kwanza kwa mchezaji huyo wa zamani wa Inter kujikuta katika matatizo na Kocha Mancini, ambaye pia alikuwa kocha wake nchini Italia.
Subscribe to:
Posts (Atom)