Monday, August 6, 2012
YANAYOJIRI LONDON OLYMPIC 2012
Mkimbiaji wa Uingereza Tiffany Potter katika mbio za mita 100 kuruka viunzi wanawake
Usain Bolt akipiga dua kwa staili yake kabla ya kuanza kutoka nduki katika mbio za mita 100 kwa wanaume
Juliana Silva wa Brazil akishangilia ushindi katika mchezo wa Beach Volleyball huku Sara Goller na Laura wakiwa wamelowa kwa kichapo
Benjamin Kleibrink wa Ujerumani akizichapa na Alexander Massialas wa Marekani
Juliana Silva wa Brazil akirudisha mchomo katika mchezo wa Beach Volleyball dhidi ya Ujerumani
Tonje Nostvold wa Norway mwenye mpira akikabiliana na Andrea Barno San Martin wa Uhispania katika mpira wa mikono(Handball)
Mchuano wa Mpira wa mikono (Handball) ukikutanisha Urusi(Nyeupe) na Montenegro(Nyeusi)
Tulia weweeee!!! Mtanange mkali kati ya Karoline Dyhre wa Norway na Mata Manguez Gonzalez wa Spain katika mchezo wa mpira wa mikono katika dimba la Copper Box
Ezekiel Kiomboi wa Kenya mshindi wa medali ya dhahabu akisherehekea pamoja na Mehiedine Mekhissi-Benabad wa Ufaransa mshindi wa medali ya fedha baada ya kumaliza mbio za mita 3000 wanaume katika dimba la Olympic(Olympic Stadium)
SIMBA KUTEMBELEA YATIMA NA WAGONJWA KUELEKEA SIMBA DAY
Simba Sports Club
KIKOSI
kizima cha wachezaji wa Simba SC, leo kinatarajiwa kutembelea kituo cha watoto
yatima cha Maungu Orphanage Center, kilichopo Kinondoni Mkwajuni, Dar es Salaam
katika mfululizo wa Wiki ya Simba na Jamii, kuelekea tamasha la kuazimisha
kuzaliwa kwa klabu hiyo, Simba Day, Agosti 8, mwaka
huu.
Wachezaji wa
Simba, wanatarajiwa kujumuika na watoto hao, wanaoishi katika mazingira magumu
na kuwafariji sambamba na kuwapa zawadi
mbalimbali.
Ratiba
inaonyesha kesho Simba watatembelea wagonjwa katika hospitali ya Mwananyamala
mjini Dar es Salaam na keshokutwa ndipo litafanyika Tamasha la Simba Day, Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika
tamasha hilo, litakalotanguliwa na burudani mbalimbali, litafuatiwa na
utambulisho wa wachezaji wote wa kikosi cha msimu ujao cha Simba SC wakiwemo
Mrisho Khalfan Ngassa aliyesajiliwa kutoka Azam FC, Mbuyu Twite kutoka APR ya
Rwanda na wengineo.
Baada ya
utambulisho, Simba itacheza mechi ya kirafiki na timu ambayo hadi sasa
haijatajwa ingawa wachunguzi wa mambo wamefunguka kuwa klabu ya Simba ipo kwenye
mawasiliano na Nairobi City Stars ya Kenya.
Siku
inayofuata, yaani Agosti 9, Simba watatembelea shule ya msingi Mgulani,ili kuhamasisha michezo mashuleni na Agosti 10, mabingwa hao wa
Tanzania, watahitimisha wiki ya Simba na Jamii, kwa kutembelea kiwanda cha
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kilichopo Ilala, Dar es
Salaam.
TBL ndio
wadhamini wakuu wa Simba SC, kupitia bia yao ya Kilimanjaro Premium Lager,
ambayo pia ndio imedhamini Wiki nzima ya Simba na Jamii, kuanzia kwenye Mkutano
Mkuu wa mwaka wa klabu hiyo, jana Bwalo la Maofisa wa jeshi la Polisi,
Oysterbay, Dar es Salaam,
RATIBA YA
WIKI YA SIMBA KWA JAMII:
Agosti 5, 2012: Mkutano
Mkuu wa mwaka Simba SC (Polisi Oystrebay)
Agosti 6, 2012: Kutembelea
watoto yatima Maungu Orphanage Center, K’ndoni
Mkwajuni
Agosti 7, 2012: Kutembelea
wagonjwa Mwananyamala hospitali
Agosti 8, 2012: Simba Day (Uwanja wa Taifa, burudani na
mechi)
Agosti 9, 2012: Kutembelea
shule ya msingi Mgulani kuhamasisha michezo
mashuleni
Agosti 10, 2012: Kutembelea
kiwanda cha TBL Ilala
RAGE AWAFUNGUKIA YANGA DAU LA OKWI NI BILIONI 3,AUSTRIA KULIPWA MIL 57 KWA MWEZI
Emmanuel Okwi
KATIKA kile kinachoonekana kuwa ni kutaka kuwakomoa mahasimu wao wa jadi, Yanga, klabu ya Simba imetangaza kuwa tayari kumuuza straika wao Emmanuel Okwi kwa dau kufuru la dola za Marekani milioni 2, ambazo ni sawa na Sh. bilioni 3.
Bei hiyo ya
Okwi kwa Yanga inazidi mara 13 ya kiasi cha pesa walichokihitaji Simba wakati
wakimuuza straika wao Mbwana Samatta kwenda klabu tajiri ya TP Mazembe ya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambayo ilikuwa ni dola za Marekani 150,000 tu,
sawa na Sh. milioni 230!
Mwenyekiti
wa Simba, Ismail Aden Rage, ndiye aliyetangaza dau hilo linaloonekana wazi kuwa
na dhamira ya kufuta ndoto za Yanga kumtwaa Okwi wakati akizungumza kwenye
mkutano wa klabu hiyo ya Msimbazi uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Bwalo la
Mafisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage akizungumza katika mkutano uliofanyika kwenye bwalo la Polisi Oysterbay jijini Dar.
Aidha, dau
hilo la Okwi pia linazidi takriban mara mbili ya bajeti ya Simba kwa mwaka ujao
wa fedha ambayo ilisomwa jana kwenye mkutano huo na kukadiriwa kuwa haitazidi
Sh. bilioni 1.6.
Rage alisema
kuwa Okwi bado ni mchezaji halali wa klabu yao na kama Yanga wanamuhitaji kweli,
basi watoe fedha taslim kiasi cha dola za Marekani milioni 2 (Sh. bilioni
3).
Hata hivyo,
inakumbukwa kwamba ni wiki iliyopita tu, Simba ilisema kuwa inatarajia kumuuza
Okwi kwa euro 600,000 (sawa na Sh. bilioni 1.1) kwa mabingwa wa Austria, klabu
ya Redbull Salzburg ambayo ilishiriki hivi karibuni ilitoka kushiriki hatua ya
awali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Viwango
tofauti vya bei ya mchezaji huyo, vinamaanisha kwamba Simba iko tayari kumuuza
Okwi kwa bei poa Ulaya kuliko kumuona anajiunga na Yanga; na kwamba thamani ya
straika huyo wa kimataifa wa Uganda ni mara 13 ya Mbwana Samatta waliyemuuza kwa
TP Mazembe.
Akieleza
zaidi kwenye mkutano huo uliohudhuriwa na wanachama zaidi ya 700, Rage alisema
kuwa kwa vyovyote vile, Okwi hawezi kukataa ofa ya mshahara wa euro 30,000 (sawa
na Sh. milioni 57) kwa mwezi nchini Austria na kujiunga na watani zao, Yanga
ambao wanasemekana wako tayari kumlipa mshahara wa Sh. milioni 2.5 kwa mwezi
endapo atakubali kujiunga nao.
Subscribe to:
Posts (Atom)