Simba Sports Club
KIKOSI
kizima cha wachezaji wa Simba SC, leo kinatarajiwa kutembelea kituo cha watoto
yatima cha Maungu Orphanage Center, kilichopo Kinondoni Mkwajuni, Dar es Salaam
katika mfululizo wa Wiki ya Simba na Jamii, kuelekea tamasha la kuazimisha
kuzaliwa kwa klabu hiyo, Simba Day, Agosti 8, mwaka
huu.
Wachezaji wa
Simba, wanatarajiwa kujumuika na watoto hao, wanaoishi katika mazingira magumu
na kuwafariji sambamba na kuwapa zawadi
mbalimbali.
Ratiba
inaonyesha kesho Simba watatembelea wagonjwa katika hospitali ya Mwananyamala
mjini Dar es Salaam na keshokutwa ndipo litafanyika Tamasha la Simba Day, Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika
tamasha hilo, litakalotanguliwa na burudani mbalimbali, litafuatiwa na
utambulisho wa wachezaji wote wa kikosi cha msimu ujao cha Simba SC wakiwemo
Mrisho Khalfan Ngassa aliyesajiliwa kutoka Azam FC, Mbuyu Twite kutoka APR ya
Rwanda na wengineo.
Baada ya
utambulisho, Simba itacheza mechi ya kirafiki na timu ambayo hadi sasa
haijatajwa ingawa wachunguzi wa mambo wamefunguka kuwa klabu ya Simba ipo kwenye
mawasiliano na Nairobi City Stars ya Kenya.
Siku
inayofuata, yaani Agosti 9, Simba watatembelea shule ya msingi Mgulani,ili kuhamasisha michezo mashuleni na Agosti 10, mabingwa hao wa
Tanzania, watahitimisha wiki ya Simba na Jamii, kwa kutembelea kiwanda cha
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kilichopo Ilala, Dar es
Salaam.
TBL ndio
wadhamini wakuu wa Simba SC, kupitia bia yao ya Kilimanjaro Premium Lager,
ambayo pia ndio imedhamini Wiki nzima ya Simba na Jamii, kuanzia kwenye Mkutano
Mkuu wa mwaka wa klabu hiyo, jana Bwalo la Maofisa wa jeshi la Polisi,
Oysterbay, Dar es Salaam,
RATIBA YA
WIKI YA SIMBA KWA JAMII:
Agosti 5, 2012: Mkutano
Mkuu wa mwaka Simba SC (Polisi Oystrebay)
Agosti 6, 2012: Kutembelea
watoto yatima Maungu Orphanage Center, K’ndoni
Mkwajuni
Agosti 7, 2012: Kutembelea
wagonjwa Mwananyamala hospitali
Agosti 8, 2012: Simba Day (Uwanja wa Taifa, burudani na
mechi)
Agosti 9, 2012: Kutembelea
shule ya msingi Mgulani kuhamasisha michezo
mashuleni
Agosti 10, 2012: Kutembelea
kiwanda cha TBL Ilala
No comments:
Post a Comment