Friday, August 24, 2012

BARCELONA YAIBANGUA REAL MADRID 3-2 SUPERCOPA


Christian Ronaldo akishangilia goli la kwanza

Makosa ya mlinda mlango wa Barca Victor Valdes yaliipatia goli la pili Real Madrid katika muda wa lala salama kabla ya Barca kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 katika mchezo wa kwanza wa Supercopa nchini Uhispania mchezo huo ukipigwa katika dimba la Nou Camp, Mchezo wa Pili utachezwa jumatano ijayo katika dimba la Santiago Bernabeu.

Pedro, Messi kwa mkwaju wa penati na Xavi mabao yao yaliibeba Barcelona baada ya kuwa nyuma kwa goli maridadi la kichwa lililotupiwa kambani na Christian Ronaldo katika dakika ya 55 ya mchezo katika dimba la Nou Camp.

Zikiwa zimesalia dakika 5 mtanange huo uishe Angel Di Maria alimharasi Mlinda mlango Victor Valdes katika lango la Barcelona baada ya beki kumrudishia kipa wake na Di Maria kufanikiwa kumnyang'anya mpira V.Valdes na kutupia kambani goli la pili la Real Madrid.

Vilanova akishuhudia maboko ya Valdes akiwa kocha mkuu kwa mara ya kwanza katika mechi ya "Clasico" . "Ni mchezo wa timu hivyo yeyote anaweza kufanya makosa, sichukulii uzito wowote kosa lile" alisema Vilanova.
Wote tunafahamu jinsi Valdes amekuwa mtu muhimu wa kuanzisha mipira nyuma ili kuendana na mfumo wa uchezaji wa Barca.
"Kama atakuwa anapiga mipira mirefu muda wote hatutoweza kuendana na mfumo wa uchezaji wetu, hivyo tutamfariji na kumshauri aendelee na mchezo huo" Aliongeza Vilanova.

PEDRO AOTEA(Offside)
Mascherano alimpenyezea mpira wa juu Pedro na kwa umaridadi aliutuliza mbele ya Coentrao na kutupia kambani kuandika bao la kusawazisha. Luninga zilionesha shambulizi hilo na kupendekeza kuwa Pedro alianzia kwa kuotea kitu ambacho Mourinho hakusita kukizungumzia
"Sijafurahishwa na goli la kwanza la Barca,ni makosa ya kiuamuzi" Alisema Mourinho.

Utamu wa mchezo ulianza pale Sergio Ramos alipomuangusha Andre Iniesta katika eneo la hatari katika dakika ya 70, bila kung'ata filimbi wala kupepesa macho mwamuzi wa mchezo huo aliamuru lipigwe tuta, Messi alitupia kambani mkwaju maridadi wa penati na kufikisha goli la 14 katika mechi zilizozikutanisha Barcelona na Real Madrid.

Iniesta alikokota gozi na kukusanya kijiji kabla hajatoa pasi murua kwa Xavi nae bila ajizi akatupia kambani goli la tatu katika dakika ya 78, kabla ya Cassilas kuondoa mchomo wa Messi aliekaribia kutupia kambani goli la nne.

"Matokeo ya mchezo yamekuwa magumu tofauti na matarajio yetu na nafasi tulizotengeneza, Na sasa itatubidi tucheze mchezo mzuri mechi ya marudiano kama tunataka kubeba kombe" Pedro alisema katika kituo cha luninga cha Uhispania.
 
Messi kama kawaida yake amekusanya kijiji

Hapatoshi ni Ronaldo na Dani Alves

Alexis Sanchez akikabiliwa vilivyo na Coentrao
 
Messi akishangilia baada ya kutupia kambani kwa mkwaju wa penati


Wachezaji wa Barcelona wakiwaaga mashabiki baada ya kuichabanga Madrid 3-2

Jose Mourinho wa Real Madrid akipeana mkono na Tito Vilanova wa Barcelona baada ya mechi ya Supercopa kumalizika.