Friday, June 29, 2012
RIDHIWANI KIKWETE AFANYIWA KITU MBAYA
Ridhiwani Kikwete akiwa na mwendeshaji The Mboni Show, Mboni Masimba
Katika dunia ya leo maendeleo ya sayansi na teknolojia yamekuwa yakileta tija kila kukicha na kukuza ustawi wa jamii mbalimbali. Kwa kuizungumzia teknolojia ya mawasiliano ambayo imekuwa kwa kasi na kuifanya jamii yetu kuishi maisha ya kisasa ambayo kila kazi imerahisishwa, Maendeleo hayo yamewezesha jamii mbali mbali kubadilishana ujuzi na kuvumbua vitu vipya kila kukicha na kutokana na ukweli juu ya utendaji wa teknolojia hizo sasa dunia imekuwa ni ndogo mno yaani kama kijiji kimoja ambapo watu wanaweza kufanya shughuli mbalimbali bila kujali umbali waliopo baina yao na haya yote ni matunda ya Maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano.
Maendeleo hayo na faida zote pia kuna madhara ya matumizi ya teknolojia hizo hususani za mawasiliano ambapo katika dunia ya sasa kuna mitandao ya kijamii ambayo huwaweka watu karibu zaidi, Na miongoni mwa wahanga wa madhara ya teknolojia hizi ni Ridhiwani Kikwete ambaye ni mtoto wa Rais wa Tanzania Mh Dk Jakaya Mrisho Kikwete.
Akizungumzia yaliyomsibu kutokana na teknolojia ya mawasiliano wakati akihojiwa katika kipindi Cha The Mboni Show kinachoendeshwa na Mboni Masimba na kurushwa na kituo bora kabisa kwa vijana wa kisasa cha East Africa (EATV), Ridhiwani alisema maendeleo ya teknolojia yamemuathiri pale account yake ya mtandao wa Kijamii wa FACEBOOK (ambao umejizolea umaarufu mkubwa ulimwenguni kwa hivi sasa) ilipovamiwa ama kupokwa na wahalifu wanaojulikana kama kitaalamu kama "HACKERS". Walitumia utaalamu wao na kujimilikisha account hiyo na kupost status ambayo ilizua utata mkubwa kwa Ridhiwani na familia yake.
Akielezea kuhusu mkasa huo anasema baada ya ile status kuonekana akiwa hajui hili wala lile alipokea simu usiku wa saa saba, na mara alipopokea hakupata hata salamu na neno la kwanza akaulizwa,"Hivi wewe zinakutosha?" alipatwa na mshangao asijue la kufanya. ndipo alipoingia kwenye internet akagundua kuwa kuna kitu kimefanyika kwenye account yake ya FACEBOOK.
Baada ya kufuatilia sana wale wote waliodhani kuwa maneno yale aliyaandika Ridhiwani waligundua kuwa kweli sio yeye bali kuna wahalifu wa mitandaoni ndio waliomfanyia kitendo kile.
Ridhiwani anasema "haiingii akilini,Rais ni baba yangu halafu niseme maneno kama yale, na itakuwa ni usaliti kwa Chama changu kwani mimi ni mwanachama wa CCM,Hata kama nawapenda wapinzani siwezi kusema kwenye internet nitakaa nalo moyoni"
Wageni wa The Mboni Show kushoto Ridhiwani Kikwete,Mboni,Barnaba na Lisa Jensen
Mboni Masimba katikati akiwa na wageni wake Ridhiwani na Lisa Jensen
Linsa Jensen na Barnaba wakisalimiana na mashabiki waliohudhuria kipindi cha The Mboni Show
BALOTELLI AWALIZA WAJERUMANI AIPELEKA ITALIA FAINALI EURO 2012
Mpira uliopigwa na Balotelli ukitinga kambani kuandika bao la kwanza
Barwuah Balotelli alitupia kambani magoli mawili ya kupendeza mno na kuiwezesha timu yake ya Italia kuishangaza na kuiacha kinywa wazi Ujerumani kwa kuitandika magoli 2-1 katika nusu fainali ya Euro 2012, na kujihakikishia nafasi ya kucheza mechi ya fainali mjini Kiev dhidi ya Uhispania.
Mabao ya mtukutu huyo wa klabu ya Manchester City ya England, alitupia goli la kwanza wavuni kwa kichwa, na la pili kwa mkwaju wa kasi mno katika uwanja wa mjini Warsaw, na Italia kuwathibitishia Wajerumani katika kipindi cha kwanza kwamba ilikuwa na nia kamili ya kufika fainali.
Wajerumani, kufuatia mshituko, walianza kucheza kwa makini zaidi, lakini bao lao la penalti, ambalo lilipatikana katika dakika ya 92, kupitia Mesut Ozil, lilichelewa mno, na halikuweza kuwaokoa.
Italia kamwe hawajawahi kushindwa na Ujerumani katika mashindano makubwa, na wamefanikiwa sasa kucheza mechi nane dhidi ya Ujerumani pasipo kushindwa.
Hii sasa itakuwa mara ya tatu kwa Italia kuingia fainali za michuano hii ya mataifa ya Ulaya, na wataingia fainali kama timu inayodhaniwa kuwa dhaifu ikilinganishwa na mabingwa watetezi Uhispania.
Timu hii ya meneja Cesare Prandelli ilistahili ushindi, kwani sio tu waliweza kupambana na Ujerumani ambayo iliwashinda wapinzani wao kwa urahisi, bali pia walifunga mabao yao mapema katika kipindi cha kwanza.
Timu hiyo ya Azzurri ilikuwa na nafasi ya kujiongezea magoli, lakini ilicheza kwa tahadhari kwa kuhofia kwamba iwapo ingeliongoza mashambulizi zaidi dhidi ya Italia, kulikuwa na uwezekano wa ngome yao kuachwa ikiwa dhaifu, na Wajerumani kuwashambulia.
Italia 2-1 Ujerumani
Mtaalamu Pirlo akiyoyoma na mpira
Balotelli akishangilia bao la pili
Gomez akipiga kichwa kilichopaa golini
I am superman...Balotelli akitunisha misuli baada ya kutupia kambani bao maridhawa
Ukiujua ni raha sana..kama nnaliaaaaaaaa!!!
Viti vya moto..wajerumani wamesepa!!!
Mesut Ozil
Wera weraaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!
Mlinga mlango wa Italia Gianluigi Buffon akishangilia ushindi dhidi ya Ujerumani
Muuaji wa Ujeruman Barwuah Balotelli akishangilia ushindi mwanana
Subscribe to:
Posts (Atom)