Thursday, August 25, 2011

MASTAA WANAPOKUWA UFUKWENI MAMBO HUWA MSWANO

HALLE BERRY photo | Halle Berry
Halle Berry akiwa Malibu,Calif Beach.

BROOKE BURKE & DAVID CHARVET photo | Brooke Burke, David Charvet
Hapa nikawabamba Brook Burke na David Chavret wakifanya mambo ya faragha hadharani kweupeeeee.


RIHANNA photo | Rihanna
Nikamuotea Rihhana akiwa ndani ya boat akitokea Barbados akielekea Saint Lopez.


RIHANNA  photo | Rihanna
Hapa Rihhana yupo kwao kabisa alipozaliwa nida ya nite nite hukooo Barbados.


DAVID BECKHAM  photo | David Beckham
Hapa nikamkuta staa wa soka David Beckham na wanawe Brooklyn (12), Romeo(8), Cruz(6) wakijiachia pande za Malibu,Calif Beach.


KELLAN LUTZ  photo | Kellan Lutz
Mbunifu wa mavazi mwenye mbavu nene Kellan Lutz akipasha katika pwani ya Los Angeles.


JENNIFER LOPEZ photo | Jennifer Lopez
Mwanadada J Lo nae alikuwa pande za Miami akila bata kimtindo, mwanadada huyo kwa sasa yupo single kama unamhitaji nipigie nikupe namba yake ya simu.


WHITNEY PORT photo | Whitney Port
Whitney Port nae alikuwepo pande za Miami.


ASHLEY TISDALE photo | Ashley Tisdale
Ashley Tisdale nae aliponiona nakatiza maeneo ya bwawa la kuogelea la klabu ya Venus iliyopo Las Vegas alitoka mbio na kuweka pozi ili nimpige picha.


BAR REFAELI photo | Bar Rafaeli
Usione kanuna nilianza kwa kumtongoza akakasirika akaona nataka kumletea shida katika familia yake, basi mwisho nikamwambia pozi basi japo picha ingawa umenikataa. Nilimkuta maeneo ya Porto Cevo nchini Italy.


KRIS HUMPHRIES photo | Kris Humphries
Hapa mume wa Kim, Chris Humphries akiwanyanyasa wenzake kwa kudaka mipira yote ya juu kwa kuw yeye ni mcheza basketball, hapa ni maeneo ya Ufukwe wa Tao pande za Las Vegas.


DEREK HOUGH photo | Derek Hough
Derek Hough nae akanitonya nimfotoe japo yupo single pande za ufukwe wa Miami.


CIARA photo | Ciara
Mwanadada Ciara, nilijikaza sana wakati nampiga picha hii nilipomkuta pande za Miami


DAVID BECKHAM photo | David Beckham
Beckham hapa kawaacha madogo na kuwaambia kuwa sasa ameamua kwenda maji ya shingo na wasimfuate, nikamuwahi nikamfotoa hapa ilikuwa pande zilezile za Malibu,ufukwe wa Calif.


CHANNING TATUM & JENNA DEWAN photo | Channing Tatum, Jenna Dewan
Channing Tatum na Jenna Dewan wakijiachia ufukweni walipokuwa mapumzikoni katika Hotel ya Viceroy Anguilla huko Caribbean.

MASTAA WALIVYOJIACHIA MSIMU WA KIANGAZI "SUMMER TIME"

EVA & EDUARDO
 photo | Eduardo Cruz, Eva Longoria
Eva Longoria akiwa na baasha-ake Beau Cruz katika fukwe za Miami.


BRITNEY & JASON   photo | Britney Spears, Jason Trawick
Britney na Jason wakiwa ndani ya Boat wakila bata pamoja na watoto wao wa kiume Jayden miaka 4 na nusu, na Sean Preston miaka 5 na nusu katika kisiwa cha Long jijini New York.


SELENA & JUSTIN   photo | Justin Bieber, Selena Gomez
Selena na Justin Beiber wakijivinjari pande za Hawaii.


JENNIFER & JUSTIN   photo | Jennifer Aniston
Jennifer Aniston akiwa na mpenzi wake mpya Theroux pande za Hawaii.


JULIANNE & RYAN   photo | Julianne Hough, Ryan Seacrest
Mwendeshaji wa mashindano ya American Idol, Seacrest akimbusu mpenzi wake Hough pande za Miami.


MEGAN & BRIAN   photo | Brian Austin Green, Megan Fox
Megan na Brian wakiwa pande za Kona,Hawaii.


LEANN & EDDIE   photo | Eddie Cibrian, LeAnn Rimes
Leann na Eddie wakijiachia vilivyo walipokuwa Honeymoon pande za Cabo san Lucas nchini Mexico.


JENNA & CHANNING   photo | Channing Tatum, Jenna Dewan
Jenna na Channing pande za Caribbean beach.


CAMERON & ALEX   photo | Alex Rodriguez, Cameron Diaz
Cameron Diaz akiwa na mpenzi wake Rodriguez, ambaye ni mcheza baseball wa timu ya New York Yankee wakiwa katika pozi pande za miami.


KIM & KRIS   photo | Kim Kardashian, Kris Humphries
Kim Kardashian na mumewe Chris Humphries wakibebana kwa mahaba pande za Punta Mita ndani ya Mexico.

Ratiba Ligi Kuu Uingereza Mwisho wa wiki hii 27-28 Agosti 2011

WIMBO WA LEO "THEY DON CARE ABOUT US"

BUNGE LIMEDHARAULIWA WAZIRI MKUU AMEDHALILIKA

Sakata la Jairo kukusanya fedha katika taasisi mbalimbali ili kutoa rushwa kwa wabunge ili "bajeti mbovu" ya wizara ya nishati na madini ipitishwe kiulaini liliibuliwa na wabunge wakitaka lichunguzwe kwanini rushwa itumike kupitisha bajeti? Hii ina maana wabunge walikuwa na uhakika na wanachokinena kamwe sitarajii mbunge ambaye ametumwa kazi na wananchi na kula kiapo cha kuwa bungeni halafu leo hii amsingizie mtu kitu hii sio kweli lazima kuna ukweli ndani yake.

Hivyo sakata hili lilipaswa kuchunguzwa huku Bunge likipewa kipaumbele katika kulichunguza na kutoa maamuzi kwani Bunge ni muhimili mkubwa katika taifa, linaweza lisiwe na maamuzi fulanifulani lakini kushirikishwa ni lazima haswa kwa ishu ambayo imetokea bungeni.
Tofauti na mawazo ya wengi baada ya kusikia Jairo kasimamishwa kwa uchunguzi, walio wengi tulijua sasa serikali imefikia hatua nzuri ya utawala bora kumbe duuuuh..kesi ya nyani bwana akaipata Ngedere.. anaechunguza ni mtumishi wa serikali na anaechunguzwa ni mtumishi wa serikali....mh uamuzi ukatoka arudi kazini kwa kuwa hakuna uthibitisho wa shutuma hizo na kwamba ni kawaida kwa taasisi kuchangisha fedha katika kufanikisha mabo fulanifulani. Sasa najiuliza hii ni Taarifa kutoka Ikulu kwa mkuu wa nchi,je imetolewa bila Rais kushirikishwa? kama ameshirikishwa basi na yeye ni fisadi. kwanini nasema hivyo? Ikumbukwe Waziri mkuu mtoto wa mkulima Mh Mizengo Kayanza Pinda alisema alipokuwa bungeni kuwa angekuwa na mamlaka ya kumtimua Jairo angemtimua lakini mwenye mamlaka hayo ni Rais.

Kutokana na Waziri mkuu kutoa kauli ile ina maana tayari alijua kuwa kuna tatizo hivyo alikuwa akimsubiri Rais atoe maamuzi ya kumfukuza Jairo, sasa kwa kauli ya Ikulu kumkingia kifua Jairo ina maana Waziri mkuu yupo kinyume na Ikulu na amekosea kutoa kauli ile bungeni? Kama ni hivyo Waziri mkuu pia yupo kinyume na Rais kwani ndie aliemchagua. Hapa tumejifunza kuwa Ikulu pia inamdharau waziri mkuu kwani imepingana na kauli yake aliyoitoa Bungeni.

Wakati Jairo ameamriwa kuripoti kazini "kinyume na taratibu" Ngeleja ameripotiwa na vyombo vya habari akitoa kauli ambayo kwa namna moja au nyingine ni ya kumkingia kifua Jairo, Kwani alipohojiwa juu ya Maamuzi ya kumrudisha Jairo kazini alisema"Unajua nchi yetu inaongozwa kwa sheria na kanuni hivyo haki imetendeka" khaaaa Ngeleja?????? Hizo sheria na kanuni nani anazitunga? bila shaka ni Bunge sasa kama sheria zinazotungwa na bunge ndio zimetumika kumsafisha Jairo iweje haohao wabunge wagomee maamuzi hayo? Ndio lazima wagome hawakushirikishwa, kwa hili Ngeleja wewe pia ukiwa ni mbunge umekurupuka kuongealea swala hilo bora ungekaa kimya badala yake umeleta mkanganyiko zaidi..ooh nchi inaongozwa na sheria na kanuni..labda kuna zingine tusizozijua sio hizi ambazo wabunge wetu watukufu wanazijua na kuzitumia kutetea haki za wanyonge, Namsifu Jairo ameonesha ukomavu wa kisiasa/uongozi kwani alipohojiwa kama anatarajia kumchukulia hatua mtu yeyote, hakutoa kauli za kuleta mikanganyiko na badala yake akasema amemsamehe aliemshutumu, sio kweli kwamba amemsamehe bali zile ni busara akitaka mambo yapoe maana angetoa kauli ya tofauti angeendeleza malumbano.

Kwa hayo yote inanishurutisha kusema kuwa Ikulu, Katibu mkuu kiongozi, Ngeleja wote wachukuliwe hatua kwa kulidhalilisha Bunge letu tukufu na kwa kumdhalilisha Waziri mkuu(Pinda). kwa kuingilia kazi za bunge,kwa kupingana na kauli ya waziri mkuu kwani nina imani ni kiongozi mkubwa serikalini hivyo hawezi kukurupuka na kutoa tamko lazima amefikiria na kujua ukweli uko wapi, na kama angekuwa na mamlaka ya kumtimua Jairo siku nyingi angekuwa amerudi kijijini kwao kufuga kuku.

Sasa ni wakati wa mtukufu Rais kuzungumzia swala hili kwani watendaji wako wanajikanganya sasa ukiacha waendelee kulumbana na Bunge ambalo ndio wananchi watakufikisha pabaya maana inaonekana wengi wao bado sio wakomavu na wamekosa busara za kuwa viongozi.
Shukurani za pekee zimwendee Mh Zitto Kabwe kwa kuongoza vyema mjadala huo na wabunge wote wa Bunge letu tukufu isipokuwa Ngeleja. Pia napenda nimpongeze Mh Waziri mkuu Mizengo Pinda, ninachoweza kusema kwa hili wanajaribu kukukatisha tamaa lakini usife moyo tupiganie wakulima walalahoi wenzio wewe ndio kiongozi wa pekee mwenye kuwajali wanyonge. Wanafanya haya kwa kujua kuwa wewe unaweza kuwa kikwazo kikubwa katika UFISADI wao, kwa maana mara nyingi umeonekana ukichukizwa na vitendo vya viongozi kufuja mali za umma.

ARSENAL YAIADHIBU UDINESE YATINGA HATUA YA MAKUNDI KLABU BINGWA ULAYA

Timu ya Arsenal ya Uingereza hatimae imefanikiwa kutinga katika hatua ya makundi ya michuano ya klabu bingwa ya ulaya baada ya kuilaza Udinese ya Italy 2-1, kwa matokeo hayo yaliiondosha Udinese kwa jumla ya mabao 3-1 kwani ikumbukwe mchezo wa kwanza uliochezwa Emirates Arsenal ilishinda
1-0.
Katika mesci hiyo Udinese ndio walikuwa wa kwanza kutia kambani kupitia mchezaji wake De Natali kabla ya Arsenal kusawazisha kupitia Mshambuliaji mahiri Van Persie baada ya kazi nzuri na ya kuridhisha iliyofanywa na Gervinho kwa kuwachambua mabeki wa Udinese na kumwagia majaro safi Van Persie nae bila ajizi akatia kambani, Goli la pili lilifungwa na Theo Walcott ambaye alionekana mwiba katika mechi hiyo akishirikiana vizuri na Gervinho.

Tazama magoli yalivyopatikana



UHOLANZI NAMBA 1 KWA UBORA DUNIANI KATIKA SOKA

Uholanzi imeipiku Hispania katika nafasi ya kwanza ya ubora Fifa wa kusakata soka duniani, huku Englan ikipanda nafasi mbili juu hadi ya nne.
Wachezaji wa Uholanzi
Wachezaji wa Uholanzi

Hispania mabingwa wa soka duniani na Ulaya, wameporomoka hadi nafasi ya pili baada ya kupoteza pointi katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Italia.
England, licha ya mchezo wake wa kirafiki dhidi ya Uholanzi kuahirishwa, imepanda kwa sababu Brazil ilifungwa na Ujerumani.
Jamhuri ya Ireland imepaa nafasi mbili hadi ya 31, Scotland imeruka nafasi sita na sasa inashikilia nafasi ya 55, Ireland Kaskazini nayo imefanikiwa kwenda nafasi tatu zaidi hadi ya 59, lakini Wales imeporomoka hadi nafasi ya 117.
Kwa kushika nafasi hiyo ya kwanza kwa mara ya kwanza, Uholanzi inakuwa ni taifa la saba kushikilia nafasi hiyo ya juu kisoka duniani zikiwemo - Argentina, Brazil, Ufaransa, Ujerumani na Italia ambazo ziliwahi kukalia kiti hicho.
Hispania ilikuwa inashikilia nafasi ya juu tangu mwezi wa Julai mwaka 2010 kufuatia ushindi walioupata wa Kombe la Dunia dhidi ya Uholanzi nchini Afrika Kusini.
Ujerumani inashikilia nafasi ya tatu, wakati Uruguay ndiyo nchi ya Amerika Kusini iliyo nafasi ya juu kwa dunia ikishika nafasi ya tano kutokana na kushinda Kombe la Copa America hivi karibuni nchini Argentina, wakati Brazil ipo nafasi ya sita.
Italia, Ureno, Argentina na Croatia wamefanikiwa kushikilia nafasi 10 za juu.
Viwango vya ubora wa soka vya Fifa vinatokana na kukusanya matokeo, umuhimu wa mechi zilizochezwa na ubora wa timu pinzani.