Wale wanaopenda kukaa na kuangalia Luninga(TV) muda wote ambao kwa kitaalamu tunawaita "Couch Potatoes" mpo katika hatari ya kupata madhara katika afya zenu kwa kutazama luninga kwa masaa mawili au zaidi ambapo utafiti umeonesha kuna hatari ya kupata Type 2 diabetes,Cardiovascular disease na vifo vya mapema kutokana na hayo madhara na inaripotiwa na jarida ya chama cha madawa cha Marekani (J.A.M.A).
Uangaliaji wa luninga unahusishwa na kutokuwa na mpangilio mzuri katika ulaji wa chakula, kuongezeka kwa uzito, athari za kisukari,magonjwa ya moyo na maisha mafupi. Utafiti umeonesha pia kutolala kwa usahihi pia kunasababishwa na uangaliaji wa luninga ambapo kwa kawaida mtu anatakiwa alale masaa saba mpaka nane. Kwa haya yote hatupaswi kulaumu luninga kwani sisi ndio tunaoiwasha na kushika remote na kukaa masaa yote kwenye kochi.Angalia tabia ya kuangalia luninga inavyoweza kuhatarisha afya yako:
1} TYPE 2 DIABETES; zaidi ya wamarekani milioni 26 wana kisukari kwa hili wana hatari kubwa ya kupata magonjwa ya moyo na kiharusi.Type 2 diabetes husababishwa na uzito kupita kiasi,maisha ya sedentary (sedentary lifestyle),mlo usiokamili, Ili kuepukana na hili punguza uzito na fanya mazoezi kwani kunasaidia insulin kufanya kazi ambayo ndio sababu kubwa ya kisukari.
2} CARDIOVASCULAR DISEASE (CVD). Hii inahusisha ugonjwa wa moyo,mapigo ya moyo kwenda mbio(high blood pressure),maumivu ya kifua,kiharusi na moyo kushindwa kufanya kazi. utafiti unaonesha madhara haya huwapata wanaoangalia TV kwa masaa 2 kwa siku, mwanga wa TV unaowaingia watoto unapunguza njia machoni mwao na siku za usoni wanaweza kupatwa na CVD.
Njia ya kujikinga ni kufanya mazoezi kwa nusu saa kwa siku tano au zaidi kwa wiki, kupima blood pressure na cholestrol mara kwa mara.
3}ALL CAUSE MORTALITY. Utafiti wa (J.A.M.A) umeonesha uangaliaji wa TV kwa masaa zaidi ya matatu kwa siku kunapelekea kuwa na mazoea na TV yaani "couch potato" Njia ya kuepuka hili ni ni kama zile za kujikinga na kisukari na CVD.
4}SLEEP DEPRIVATION. Kiafya tunahitaji masaa 7-8 ya kulala kila siku lakini watu wengi hawayapati ipasavyo, utafiti unaonesha uangaliaji wa TV karibu na kitanda ni wa kulaumu. Utafiti umeonesha kuwa mwanga wakati wa usiku ikiwamo wa TV una hatari ya kusababisha kansa ya maziwa kwa wanawake.
Njia ya kuepuka hili,zima TV kwa saa moja kabla ya kwenda kulala kwasababu mwanga wa TV unaupa ubongo uwezo wa kufanya kazi na hivyo kukufanya iwe ngumu kupata usingizi kwa haraka.
5} NEARSIGHTEDNESS IN KIDS. Hii imeathiri watu zaidi ya bilioni 1.6 duniani kote,idadi ni kubwa zaidi katika nchi ambazo watoto wanaangalia TV na kucheza Computer game badala ya kucheza viwanjani yaani nje.Tokyo na Hongkong 30%-50% ya watoto ni myopic(nearsightedness) na 20% U.S.A. Utafiti wa mwaka 2009 umeonesha watoto wenye athari hii ni wale wanaotumia muda wa saa 4-5 kwa wiki katika TV.
Njia ya kujikinga, utumiaji wa saa 2 kwa siku nje hupunguza tatizo hili kwa watoto na tuwashauri kuangalia vitu vilivyo mbali ili kuimarisha uwezo wa macho kuona. michezo ya nje pia huimarisha uzito wa mtoto kulingana na afya yake.
kwa maswali jiffjeff@yahoo.com +255712184598