Tuesday, July 10, 2012
MPAMBANO WA SOKA WABUNGE WA SIMBA NA YANGA KATIKA PICHA
Timu za wabunge wa Simba na Yanga wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya mpambano
Waamuzi wa mpambano huo wakipiga picha ya pamoja na manahodha wa timu zote mbili
Wabunge wa Simba katika Dua kabla ya mtanange kuanza
Wabunge wa Yanga nao wakipiga dua kabla ya mtanange kurindima
Mashabiki wakiwahi mpambano
Mtanange umeanza
Mwamuzi wa mtanange huo Athuman Kazi akifuatilia kwa karibu kuhakikisha haki inatendeka
Mh Zitto Kabwe wa Simba akitoa pasi murua kama Iniesta vile!
Mbunge wa Simba akitiririka na kabumbu
Katibu uenezi wa CCM Nape Nnauye akifuatilia mpambano wa Wabunge wa Simba na wale wa Yanga katika dimba kuu la Taifa jijini Dar es salaam
Benchi la ufundi la Wabunge wa Simba wakifuatilia mpambano
Benchi la ufundi la Wabunge wa Yanga wakiongozwa na kocha mkuu mpya wa Yanga
Mbunge wa Yanga akiwa hoi bin taaban
Mbunge wa Yanga akijaribu kuihadaa ngome ya wabunge wa Simba
Hali tete mlinda mlango wa wabunge wa Yanga baada ya kichapo kwa njia ya matuta 3-2
Wera weraaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!! wabunge wa Simba hatimae waliwachapa wa Yanga katika matuta baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya 0-0
Nani kama Simbaaaa woyooooo woyooooooooo
Hakunagaa zaidi ya Simba hakunagaa, hakunaaa hakunaaaa hakunaaaaaaaaaa!!!
Weraaaaa tupishe tupiteeee, tupisheeeee tupishe tupiteeeeeeee..Wabunge wa Simba wakiongozwa na Mh Zitto Kabwe na William Ngeleja kuserebuka baada ya kuwaangushia kisago wenzao wa Yanga kwa mikwaju ya penati 3-2
Mpambano Wabunge SIMBA Vs YANGA
Katika mtanange huo baada ya dakika 90 na kipyenga cha mwamuzi Athumani kazi kupulizwa matokeo yalikuwa ni 0-0. Mpambano huo wa kufurahisha na kusisimua uliopigwa katika dimba kuu la Taifa jijini Dar es salaam ikiwa ni katika mchezo wa hisani kukusanya pesa kuchangia ujenzi wa mabweni kwa shule za sekondari nchini!
shukrani za pekee kwa waandaaji wa tamasha hilo ambalo pia liliwakutanisha wasanii wa Bongo flava na Bongo Movie hali kadhalika mpambano wa Masumbwi kati ya wasanii maarufu nchini na wenye kutengeneza vichwa vya habari katika redio na magazeti mbalimbali hapa nchini, ni Wema Sepetu na Jaquiline Wolper ambapo katika mpambano mpambano huo uliodumu kwa raundi mbili matokeo yalikuwa ni droo hakukuwa na mshindi.
KEITA AONDOKA BARCELONA NA "NDOO"14 HUKU TITO AKIMRITHI PEP GUARDIOLA
Seydou Keita
kiungo wa Mali Seydou Keita amekihama klabu ya Barcelona baada ya kukipiga kwa miaka minne.
Katika muda huo wa miaka minne, Keita aliisaidia Barcelona kuzoa jumla ya vikombe 14.
Keita na Sanchez wakiwa wamebeba kombe wakikipiga Barcelona
Kwa wakati huu kuna fununu kwamba mchezaji huyo wa Mali huenda anahamia klabu moja ya Uchina, Dalian Aerbin
Tito Vilanova kocha alierithi mikoba ya Pep Guardiola
Tito Vilanova akiwa na Pep Guardiola
Subscribe to:
Posts (Atom)