KEITA AONDOKA BARCELONA NA "NDOO"14 HUKU TITO AKIMRITHI PEP GUARDIOLA
Seydou Keita
kiungo wa Mali Seydou Keita amekihama klabu ya
Barcelona baada ya kukipiga kwa miaka minne.
Katika muda huo wa miaka minne, Keita aliisaidia Barcelona kuzoa jumla ya
vikombe 14.
Wakati wakithibitisha kuondoka kwa mwamba huyo, Barca walimshukuru Seydou
Keita kwa juhudi zake za kuiletea klabu hiyo ya Uhispania mafanikio na vile
vile wakamtakia kila lakheri anakokwenda.
Keita na Sanchez wakiwa wamebeba kombe wakikipiga Barcelona
Kwa wakati huu kuna fununu kwamba mchezaji huyo wa Mali huenda anahamia klabu
moja ya Uchina, Dalian Aerbin
Ikiwa hatiamae ataishia China basi Keita hatakuwa mchezaji wa kwanza kutoka
bara la Afrika kufanya hivyo.
Majuzi nahodha wa timu ya Ivory Coast Didier Drogba aliwafuata Frederic
Kanoute na Yakubu Aiyegbeni wa Nigeria kujiunga na timu za ligi kuu ya
China.
Keita, mwenye umri wa 32, alijiunga na Barcelona mwaka 2008 kutoka Sevilla
akiwa ni mchezaji wa kwanza kabisa ambaye Pep Guardiola alimsajili mara tu
alipokwaa uongozi wa Barca.
Kabla ya hapo mchezaji huyo alikuwa Olympic Marseille, Lorient na Lens zote
za Ufaransa na ndio baadaye akahima Seville ya Uhispania.
Keita amehama baada ya Guardiola kuondoka kama Meneja wa Barcelona na mahali
pake kuchukuliwa na aliyekuwa naibu wake Tito Vilanova
Tito Vilanova kocha alierithi mikoba ya Pep Guardiola
Tito Vilanova akiwa na Pep Guardiola
No comments:
Post a Comment