Tuesday, May 22, 2012
HII NDIO MARCEDES MAYBACH YENYE THAMANI YA DOLA MILIONI 1.3
Marcedes Maybach Inavyoonekana kwa mbele
Sehemu ya ndani mbele
Sehemu ya ndani nyuma ambapo unaweza kujiachia kama jamaa anavyopata udambwidambwi
Pale kati ina sehemu ya kuhifadhia glasi na vinywaji vya kila aina ili mradi umatemate uwe unaruhusu tu
Unaweza kujiachia namna hii na kusahau kama kuna siku utaiaga dunia na starehe hizo ukawaaachia wenzio
ACHA NDOTO SASA RUDI KATIKA MAISHA YA UWEZO WAKO ALAAAAAH
Huu ndio saizi yetu..au mnasemaje?
BOBAN AANGUUKA NA KUZIMIA UWANJA WA NDEGE
Mgosi na Boban wakiwa katika msiba mjini Kinshasa
MICHAEL MOMBURI, KINSHASA
KIUNGO wa Simba, Haruna Moshi Boban, ameanguka katika Uwanja wa Ndege wa N`Djili mjini Kinshasa kutokana na mapigo ya moyo kushuka ghafla.
Tukio hilo lilitokea jana Jumatatu wakati Boban akiwa anajiandaa kurudi Dar es Salaam baada ya kuhudhuria mazishi ya Patrick Mafisango aliyefariki Alhamisi iliyopita kwa ajali ya gari iliyotokea jijini Dar es Salaam.
Hali ya Boban ilibadilika ghafla akiwa uwanjani hapo na akashindwa kuona mbele kabla ya kulegea na kuanguka.
Madaktari wa uwanja huo walitumia zaidi ya saa 1:30 kumtibu Boban kabla hajarejea katika hali ya kawaida huku bado akiwa na simanzi kubwa kutokana na kifo cha Mafisango.
"Nilimkumbuka sana Mafisango, wakati nikitafakari, nikaona ninalegea, nikashindwa kuona kitu chochote mbele na nikaanguka," Boban aliliambia Mwanaspoti katika uwanja huo wa ndege wa Kinshasa.
Daktari aliyemuhudumia Boban aliliambia Mwanaspoti kuwa: "Alikuwa na hali mbaya sana, mapigo ya moyo yalikuwa chini, yangeweza kuondoa maisha yake."
Licha ya kupata matibabu hayo, Boban pia alipewa kahawa kwa lengo la kuinua mapigo yake ya moyo.
Boban ambaye alikuwa rafiki mkubwa wa Mafisango ikiwa ni pamoja na kulala chumba kimoja wanapokuwa kambini Simba, aliwakilisha wachezaji wengine wa klabu hiyo katika msiba huo mjini Kinshasa.
Mwili wa Mafisango aliyekuwa akicheza nafasi ya kiungo enzi za uhai wake, ulizikwa katika makaburi ya Kinkole nje kidogo ya Kinshasa juzi Jumapili kuhitimisha safari yake ya miaka 32 ya uhai wake duniani.
MILOVAN ALAMBA DUME SIMBA SPORTS CLUB
Kocha Milovan(Kushoto) na mwenyekiti wa Simba(Kulia)Rage
Timu ya Simba Sport Club ambao ni mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara wamemuongezea mkataba kocha wao Milovan Cirkovic kwa miaka miwili zaidi na kumfanya kocha huyo kuwa na uhakika na "umatemate" zaidibaada ya ule waliokuwa wamempa mwanzo wa miezi sita kumalizika.
Mkataba uliomalizika wa Milovan ni baada ya kurithi mikoba ya Mganda Moses Basena, akitangaza kumuongezea mkataba huo kocha Milovan, Makamu mwenyekiti wa Simba Godfrey Nyange Kaburu amesema" Kipimo cha mafanikio ya kocha ni mataji na soka safi,kitu ambacho sisi kama viongozi wa Simba tumekishuhudia chini ya Profesa Milovan,sasa hatuoni kwanini tusimuongezee mkataba."
Kaburu aliongeza kuwa sababu nyingine ni mipango mizuri aliyonayo Milovan kwa soka la Vijana wa Simba, ni kitu ambacho hakipingiki katika ligi iliyokwisha tumeshuhudia Vijana wa Simba wakipata nafasi ya kucheza na dhahiri wameonesha uwezo wao,mfano mzuri Jonas Mkude,Singano na wengine yote hayo ni mafanikio ya kocha Milovan kuwapa nafasi Vijana kuonesha "udambwidambwi" wao.
NADAL BINGWA ITALIAN OPEN AMCHAPA DJOKOVIC
Rafael Nadal (Kushoto) akiwa amebeba kombe la Ubingwa wa Italian Open baada ya kumshinda Djokovic(Kulia)
Rafael Nadal, mchezaji wa Uhispania, alifanikiwa kumshinda mchezaji bora zaidi duniani wa kiume, Novak Djokovic katika mashindano ya Italia Open, na kupata ubingwa wake wa sita katika mashindano hayo ya Italia.
Nadal alipata ushindi wa 7-5 6-3 katika fainali hiyo ambayo ilichezwa Jumatatu baada ya kuahirishwa siku ya Jumapili kutokana na mvua kunyesha mno mjini Roma.
Ushindi huo umemweka Nadal katika nafasi ya pili katika orodha ya wachezaji
bora zaidi katika mashindano ya wanaume duniani.
Pamoja na hali ya hewa kuwa si shwari lakini wapenzi wa mchezo wa Tennis waliendelea kufuatilia mtifuano huo kati ya Nadal an Djokovic
Kabla ya mashindano ya Jumatatu, Djokovic, raia wa Serbia, amekuwa akimshinda Nadal mfululizo katika mashindano saba yaliyopita, kabla ya kuanza kuibuka tena kama mshindi katika fainali ya Monte Carlo Masters mwezi uliopita.
Sasa Nadal amemshinda katika fainali mbili za mwisho walizokutana.
Nadal alisema: "Mawazo ya ushindi yalinijia wakati muwafaka, kwani kumshinda Novak, unahitaji kuwa katika hali yako bora zaidi ya uchezaji, kwani yeye hukusukuma hadi mjwisho katika pambano lote.
"Nadhani kiakili nilikuwa katika hali thabiti kila wakati muhimu nilipohitajika kuwa hivyo."
Nadal Vs Djokovic
Subscribe to:
Posts (Atom)