Wednesday, March 12, 2014
ARSENAL YATOLEWA UEFA NA BAYERN MUNICH KWA TAAABU
Ozil akijaribu kuwahadaa walinzi wa Bayern
Arsenal imebanduliwa nje ya michuano ya kuwania kombe
la klabu bingwa barani Ulaya, licha ya kutoka sare ya kufungana bao
moja kwa moja na mabingwa wa Bundes Liga, Bayern Munich.
Kufuatia sare hiyo Bayern sasa imejihakikishia nafasi katika robo fainali ya kombe hilo.Bayern imefuzu kwa robo fainali hizo kwa jumla ya magoli matatu kwa moja, baada ya kushinda mechi ya awamu ya kwanza kwa magoli mawili kwa yai.
Hata hivyo mabingwa hao wa Ujermani wangeliwaadhibu zaidi vijana wa Arsene Wenger, lakini bao la Javi Martinez lilikataliwa na refa wa mechi hiyo, kwa misingi kuwa mchezaji huyo alikuwa amejenga kibanda katika eneo la wenyewe.
Bayern ndiyo ilioona lango la Arsenal, kabla ya Lukas Podolski kusawazisha.
Kipa wa Arsenal aliiepushia klabu yake aibu zaidi pale alipookoa mkwaju wa penalti uliopigwa na Thomas Muller.
Kuondolewa kwa Arsenal katika kinyang'anyiro hicho sasa kumewaacha na nafasi mbili pekee ya kumaliza ukame wao wa miaka tisa wa kutoshinda kombe lolote.
Arsenal ingali inawania kombe la FA na lile la ligi kuu ya Premier ingawa wako alama tisa nyuma ya vinara wa sasa Chelsea.
Mshikemshike katika lango la Bayern
Oxlade Chamberlain akiwekwa chini na Ribery
Mlinda mlango wa Bayern Neur akidaka mpira wa kona.
Pal Mertesacker akiondosha hatari mbele ya Alaba
Podolski akiachia nduki iliyoelekea moja kwa moja wavni na kuipatia Arsenal bao la kusawazisha.
Kazi moja Sagna na Alaba
Robben akiwa chini alipojiangusha na kupatiwa penalt.
Daah tumekufa kiume...................
Bayern 1-1 Arsenal
5 Foods That Could Kill Your Dog
1. Chocolate
2. Xylitol
3. Grapes
4. Onions/Garlic
5. Alcohol
If you believe you pet has ingested a toxic substance, call the ASPCA animal poison control center at 888-426-4435 or the Pet Poison Hotline at 855-213-6680. Both phone lines are open 24 hours a day, seven days a week.
Subscribe to:
Posts (Atom)