Sakata la Jairo kukusanya fedha katika taasisi mbalimbali ili kutoa rushwa kwa wabunge ili "bajeti mbovu" ya wizara ya nishati na madini ipitishwe kiulaini liliibuliwa na wabunge wakitaka lichunguzwe kwanini rushwa itumike kupitisha bajeti? Hii ina maana wabunge walikuwa na uhakika na wanachokinena kamwe sitarajii mbunge ambaye ametumwa kazi na wananchi na kula kiapo cha kuwa bungeni halafu leo hii amsingizie mtu kitu hii sio kweli lazima kuna ukweli ndani yake.
Hivyo sakata hili lilipaswa kuchunguzwa huku Bunge likipewa kipaumbele katika kulichunguza na kutoa maamuzi kwani Bunge ni muhimili mkubwa katika taifa, linaweza lisiwe na maamuzi fulanifulani lakini kushirikishwa ni lazima haswa kwa ishu ambayo imetokea bungeni.
Tofauti na mawazo ya wengi baada ya kusikia Jairo kasimamishwa kwa uchunguzi, walio wengi tulijua sasa serikali imefikia hatua nzuri ya utawala bora kumbe duuuuh..kesi ya nyani bwana akaipata Ngedere.. anaechunguza ni mtumishi wa serikali na anaechunguzwa ni mtumishi wa serikali....mh uamuzi ukatoka arudi kazini kwa kuwa hakuna uthibitisho wa shutuma hizo na kwamba ni kawaida kwa taasisi kuchangisha fedha katika kufanikisha mabo fulanifulani. Sasa najiuliza hii ni Taarifa kutoka Ikulu kwa mkuu wa nchi,je imetolewa bila Rais kushirikishwa? kama ameshirikishwa basi na yeye ni fisadi. kwanini nasema hivyo? Ikumbukwe Waziri mkuu mtoto wa mkulima Mh Mizengo Kayanza Pinda alisema alipokuwa bungeni kuwa angekuwa na mamlaka ya kumtimua Jairo angemtimua lakini mwenye mamlaka hayo ni Rais.
Kutokana na Waziri mkuu kutoa kauli ile ina maana tayari alijua kuwa kuna tatizo hivyo alikuwa akimsubiri Rais atoe maamuzi ya kumfukuza Jairo, sasa kwa kauli ya Ikulu kumkingia kifua Jairo ina maana Waziri mkuu yupo kinyume na Ikulu na amekosea kutoa kauli ile bungeni? Kama ni hivyo Waziri mkuu pia yupo kinyume na Rais kwani ndie aliemchagua. Hapa tumejifunza kuwa Ikulu pia inamdharau waziri mkuu kwani imepingana na kauli yake aliyoitoa Bungeni.
Wakati Jairo ameamriwa kuripoti kazini "kinyume na taratibu" Ngeleja ameripotiwa na vyombo vya habari akitoa kauli ambayo kwa namna moja au nyingine ni ya kumkingia kifua Jairo, Kwani alipohojiwa juu ya Maamuzi ya kumrudisha Jairo kazini alisema"Unajua nchi yetu inaongozwa kwa sheria na kanuni hivyo haki imetendeka" khaaaa Ngeleja?????? Hizo sheria na kanuni nani anazitunga? bila shaka ni Bunge sasa kama sheria zinazotungwa na bunge ndio zimetumika kumsafisha Jairo iweje haohao wabunge wagomee maamuzi hayo? Ndio lazima wagome hawakushirikishwa, kwa hili Ngeleja wewe pia ukiwa ni mbunge umekurupuka kuongealea swala hilo bora ungekaa kimya badala yake umeleta mkanganyiko zaidi..ooh nchi inaongozwa na sheria na kanuni..labda kuna zingine tusizozijua sio hizi ambazo wabunge wetu watukufu wanazijua na kuzitumia kutetea haki za wanyonge, Namsifu Jairo ameonesha ukomavu wa kisiasa/uongozi kwani alipohojiwa kama anatarajia kumchukulia hatua mtu yeyote, hakutoa kauli za kuleta mikanganyiko na badala yake akasema amemsamehe aliemshutumu, sio kweli kwamba amemsamehe bali zile ni busara akitaka mambo yapoe maana angetoa kauli ya tofauti angeendeleza malumbano.
Kwa hayo yote inanishurutisha kusema kuwa Ikulu, Katibu mkuu kiongozi, Ngeleja wote wachukuliwe hatua kwa kulidhalilisha Bunge letu tukufu na kwa kumdhalilisha Waziri mkuu(Pinda). kwa kuingilia kazi za bunge,kwa kupingana na kauli ya waziri mkuu kwani nina imani ni kiongozi mkubwa serikalini hivyo hawezi kukurupuka na kutoa tamko lazima amefikiria na kujua ukweli uko wapi, na kama angekuwa na mamlaka ya kumtimua Jairo siku nyingi angekuwa amerudi kijijini kwao kufuga kuku.
Sasa ni wakati wa mtukufu Rais kuzungumzia swala hili kwani watendaji wako wanajikanganya sasa ukiacha waendelee kulumbana na Bunge ambalo ndio wananchi watakufikisha pabaya maana inaonekana wengi wao bado sio wakomavu na wamekosa busara za kuwa viongozi.
Shukurani za pekee zimwendee Mh Zitto Kabwe kwa kuongoza vyema mjadala huo na wabunge wote wa Bunge letu tukufu isipokuwa Ngeleja. Pia napenda nimpongeze Mh Waziri mkuu Mizengo Pinda, ninachoweza kusema kwa hili wanajaribu kukukatisha tamaa lakini usife moyo tupiganie wakulima walalahoi wenzio wewe ndio kiongozi wa pekee mwenye kuwajali wanyonge. Wanafanya haya kwa kujua kuwa wewe unaweza kuwa kikwazo kikubwa katika UFISADI wao, kwa maana mara nyingi umeonekana ukichukizwa na vitendo vya viongozi kufuja mali za umma.
No comments:
Post a Comment