Emmanuel Okwi
KATIKA kile kinachoonekana kuwa ni kutaka kuwakomoa mahasimu wao wa jadi, Yanga, klabu ya Simba imetangaza kuwa tayari kumuuza straika wao Emmanuel Okwi kwa dau kufuru la dola za Marekani milioni 2, ambazo ni sawa na Sh. bilioni 3.
Bei hiyo ya
Okwi kwa Yanga inazidi mara 13 ya kiasi cha pesa walichokihitaji Simba wakati
wakimuuza straika wao Mbwana Samatta kwenda klabu tajiri ya TP Mazembe ya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambayo ilikuwa ni dola za Marekani 150,000 tu,
sawa na Sh. milioni 230!
Mwenyekiti
wa Simba, Ismail Aden Rage, ndiye aliyetangaza dau hilo linaloonekana wazi kuwa
na dhamira ya kufuta ndoto za Yanga kumtwaa Okwi wakati akizungumza kwenye
mkutano wa klabu hiyo ya Msimbazi uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Bwalo la
Mafisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage akizungumza katika mkutano uliofanyika kwenye bwalo la Polisi Oysterbay jijini Dar.
Aidha, dau
hilo la Okwi pia linazidi takriban mara mbili ya bajeti ya Simba kwa mwaka ujao
wa fedha ambayo ilisomwa jana kwenye mkutano huo na kukadiriwa kuwa haitazidi
Sh. bilioni 1.6.
Rage alisema
kuwa Okwi bado ni mchezaji halali wa klabu yao na kama Yanga wanamuhitaji kweli,
basi watoe fedha taslim kiasi cha dola za Marekani milioni 2 (Sh. bilioni
3).
Hata hivyo,
inakumbukwa kwamba ni wiki iliyopita tu, Simba ilisema kuwa inatarajia kumuuza
Okwi kwa euro 600,000 (sawa na Sh. bilioni 1.1) kwa mabingwa wa Austria, klabu
ya Redbull Salzburg ambayo ilishiriki hivi karibuni ilitoka kushiriki hatua ya
awali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Viwango
tofauti vya bei ya mchezaji huyo, vinamaanisha kwamba Simba iko tayari kumuuza
Okwi kwa bei poa Ulaya kuliko kumuona anajiunga na Yanga; na kwamba thamani ya
straika huyo wa kimataifa wa Uganda ni mara 13 ya Mbwana Samatta waliyemuuza kwa
TP Mazembe.
Akieleza
zaidi kwenye mkutano huo uliohudhuriwa na wanachama zaidi ya 700, Rage alisema
kuwa kwa vyovyote vile, Okwi hawezi kukataa ofa ya mshahara wa euro 30,000 (sawa
na Sh. milioni 57) kwa mwezi nchini Austria na kujiunga na watani zao, Yanga
ambao wanasemekana wako tayari kumlipa mshahara wa Sh. milioni 2.5 kwa mwezi
endapo atakubali kujiunga nao.
No comments:
Post a Comment