Frank Ribbery akiipatia Bayern bao la kuongoza kwa shuti kali
Bao lililofungwa katika dakika za mwisho na Mario Gomez iliiweka Bayern Munich kifua mbele kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Real Madrid katika dimba la Allianz Arena mjini Munich Ujerumani ambapo ndipo kipute cha fainali cha ligi ya mabingwa kitarindimishwa.
Ushindi huo ni katika duru ya kwanza ya mechi ya nusu fainali ya kombe la mabingwa bara ulaya.
Mshambuliaji matata Franck Ribery alikuwa wa kwanza kutupia langoni mwa Real Madrid pale alipofumua mkwaju mkali wa chinichini na kumuacha kipa Iker Casillas akiwa hoi bin taaban.
Katika kipindi cha pili iliwachukua dakika 10 tu Real kurudisha matumaini ya kurudi tena Allianz Arena katika fainali pale Mesut Ozil akiwa hauta chache toka langoni aliipatia bao lake mnamo dakika ya 55.
Ozil na Ronaldo wakishangilia goli la kusawazisha
Wakati watazamaji wakidhania mpambano huo mkali ungeishia kwa sare, hamad! Gomez akachafua hali ya hewa kwa Real Madrid pale alipotupia kambani msumari wa mwisho na wa uchungu kwa Real katika dakika za mwisho.
Gomez akipigilia msumari wa pili
Kabla ya kufunga bao hilo Gomez alipoteza nafasi nyingi za kufunga,huku Webb refa wa mchezo huo akimnyima penati ya dhahiri baada ya Gomez kuangushwa na wachezaji watatu ndani ya eneo la hatari la Real Madrid.
Christian Ronaldo akiwa hoi bin taaban kwa kichapo
Hata hivyo mwamba wa Real Madrid Cristiano Ronaldo hakua na siku njema kwani hakuna kubwa alilofanya akiwa uwanjani bali alikuwa anambwelambwela tu na mpaka kipyenga cha mwisho Bayern 2-1 Real Madrid.
Jinsi Gomez alivyoangushwa eneo la hatari lakini Webb akaipotezea.
BAYERN 2-1 REAL MADRID
No comments:
Post a Comment