Thursday, June 21, 2012

WALIOONGOZA KWA KUTUPIA KAMBANI KATIKA HATUA YA MAKUNDI EURO 2012


1-(3)  Alan Dzagoev wa Urusi ameshatupia kambani mara mpaka kumalizika kwa hatua ya makundi, amekwishapoteza matumaini ya kunyakua daruga la dhahabu kwani Urusi haikufanikiwa kufuzu katika hatua ya robo fainali katika kundi A.


2-(3) Mario Gomez wa Ujerumani amekwisha kutupia kambani mara tatu na ana matumaini makubwa ya kuibuka kidedea kwa kutupia kambani katika michuano ya EURO 2012 baada ya Ujerumani kufuzu katika hatua ya robo fainali baada ya kuibuka namba moja katika kundi B ikijikusanyia pointi zote 9 ikifuatiwa na Ureno iliyomaliza kwa pointi 6.


3-(2) Andriy Shevchenko nahodha wa Ukraine ambao ndio wenyeji wenza wa michuano ya EURO 2012 ametupia kambani mara 2 na kwa bahati mbaya wenyeji hao wametupwa nje ya michuano hiyo baada ya kumaliza katika nafasi ya 3 katika kundi D, Uingereza na Ufaransa zikipenya kwa hatua ya robo fainali. 


4-(2) Christian Ronaldo wa Ureno amekwisha tupia mara 2 na ana matumaini makubwa ya kuwa kinara wa mabao katika mashindano hayo baada ya Ureno kufuzu robo fainali baada ya kushika nafasi ya pili katika kundi B nyuma ya Ujerumani.


5-(2) Fernando Torres wa Uhispania ametupia mara 2 na anaweza kuendelea kutupia baada ya timu yake ya Uhispania kufuzu kwa hatua ya robo fainali baada ya kuongoza kundi C.


6-(2) Francesc Fabregas wa Uhispania amekwishatupia kambani mara 2 matumaini ya kuendelea kutupia yanabaki baada ya timu yake kutinga katika hatua ya robo fainali ikiongoza kundi C na sasa atachuana na mhispania mwenzake Fernando Torres katika mbio za kuvaa daluga la dhahabu.


7-(2) Mario Mandzukic wa Croatia ametupia mara 2 na ndio mwisho baada ya Croatia kushindwa kuvuka hatua ya makundi kuelekea robo fainali za michuano ya EURO 2012 ikimaliza katika nafasi ya 3 kundi C


8-(2) Michael Krohn-Dehli wa Denmark ametupia kambani mara 2 na matumaini ya kuvaa daluga la dhahabu yaliyeyuka pale Denmark waliposhindwa kufuzu kwa hatua ya robo fainali baada ya kushika nafasi ya 3 kundi B


9-(2) Nicklas Bendtner wa Denmark ametupia mara 2 na ndio amemaliza hapo baada ya Denmark kuburuzwa nje ya michuano hiyo katika kundi B


10-(2) Olof Mellberg wa Sweden nae amefanikiwa kutupia kambani mara 2 na kutokana na ukweli kwamba Sweden haijafuzu kwa hatua za robo fainali matumaini yake ya kunyakua kiatu cha dhahabu yamezikwa rasmi.


11-(2) Petr Jiracek wa Jamhuri ya Czech ametupia mara mbili na itambidi asubiri miaka minne ijayo ili aendelee kuwania ufungaji bora kwasababu Timu yake imeshindwa kufuzu kwa hatua ya robo fainali za EURO 2012.


12-(2) Vaclav Pilar wa Jamhuri ya Czech nae ametupia kambani mara 2 lakini kutokana na timu yake kushindwa kufuzu kwa hatua ya robo fainali sasa matumaini yake ya kutwaa daluga la dhahabu yameishia hapo.


13-(2) Zlatan Ibrahimovic mshambuliaji wa Sweden ametupia kambani mara 2 na ki ukweli kabisa kama Sweden ingesonga katika hatua ya robo fainali basi huenda angetupia mara nyingi zaidi kutokana na uwezo alionao, lakini sasa ndio basi tena Sweden wameshatupwa nje baada ya kushika mkia katika kundi D.

No comments:

Post a Comment