Tuesday, August 23, 2011

Upinzani washinda urais Cape Verde

Mgombea wa upinzani Jorge Carlos Fonseca ameshinda katika uchaguzi wa urais wa Cape Verde, akimshinda mpinzani wake Manuel Inocencio Sousa kutoka chama tawala.


Wananchi wakishangilia ushindi wa Fonseca

Bw Fonseca alipata takriban aslimia 55 ya kura zote katika duru ya pili ya uchaguzi siku ya Jumapili, ukilinganisha na mwenzake Bw Sousa aliyepata asilimia 45.

Viongozi hao wawili wamewania nafasi hiyo baada ya Rais Pedro Pires kung'atuka kufuatia kumaliza vipindi vyake viwili.

Wachambuzi wanasema, Cape Verde ni moja ya nchi zenye demokrasia thabit barani Afrika.

Bw Fonseca, mwenye umri wa miaka 60, alisema atalenga zaidi kuujenga uchumi wa Cape Verde.

Amenukuliwa na shirika la habari la AFP akisema, "ushindi wangu ni wa kidemokrasia, kwa heshima ya watu wa Cape Verde walioamini mipango yangu."

No comments:

Post a Comment