Monday, September 12, 2011

KIUMBE MPYA KUBAINI ASILI YETU AGUNDULIWA A.KUSINI

Mabaki ya kale ya viumbe wawili waliopatikana huko Afrika ya kusini wanaofanana na binadamu yanaweza kubadili mtazamo wetu kuhusu asili yetu.
australopithecus sediba
Babu australopithecus sediba

Mabaki hayo yanayokadiriwa kuwa yamepatikana baada ya miaka milioni 1.9 yalielezewa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2010, na kupewa jina la kitaalamu Australopithecus sediba.
Tangu hapo kundi la wataalamu lililofanya ugunduzi wakati ule limerudi na uchambuzi wa kina zaidi.
Kundi hilo limelifahamisha jarida linalochapisha habari za Sayansi kua maumbile yaliyoshuhudiwa ya ubongo, miguu, mikono na mifupa ya nyongo yote yameonyesha kama viumbe hawa ni wa kwanza katika asili yetu -binadamu - ama kwa jina la kitaalamu - Homo sapiens.
Profesa Lee Berger wa Chuo kikuu cha Witwatersrand mjini Johannesburg anasema kuwa "wamechunguza sehemu muhimu za binadamu zinazoelezea umbo linalombainisha binadamu na viumbe wengine, na kuna uwezekano wa sehemu za binadamu kukuwa kwa nyakati tofauti na A.sediba anaonyesha kutimiza vigezo vya maumbile ya mwanadamu, kiongozi wa kundi la wataalamu aliifahamisha BBC.
Ni madai makubwa, na ikiwa yana ukweli, basi kuna uwezekano wa rekodi zilizokuepo kuhusu asili yetu kuwekwa kando.
Nadharia inashikilia msimamo kuwa binadamu wa sasa anaweza kudai urithi wake kutoka kwa kiumbe anayejulikana kama Homo erectus aliyeishi zaidi ya miaka milioni moja iliyopita.
homo erectus
kiumbe aliyekwenda kwa miguu miwili

Mnyama huyu, kwa mujibu wa wataalamu wa anthropolojia, huenda naye alikua na asili ya aina ya kiumbe ambaye hakustaarabika ajulikanaye kama hominin, mfano ni Homo habilis au Homo rudolfensis.
Jambo la kuridhisha kuhusu madai juu ya A. sediba ni kwamba ingawa ni wa kale kuliko wenzake , baadhi ya maumbile yake na uwezo wake yanaonyesha kuwa alikuwa na uwezo zaidi kuliko wenzake wa baadaye.
Kwa kifupi inaaminika A.sediba yuko karibu zaidi na babu wa mwanadamu Homo erectus.
babu wa miguu miwili
homo erectus

Mabaki ya sediba yalifukuliwa huko Malapa katika eneo maarufu la asili ya mwanadamu , nje kidogo na kaskazini magharibi mwa Johanesburg.
Viumbe hawa waliotambuliwa kama mwanamke my mzima na mvulana kijana, wametambuliwa kuwa mama na mwana. Kilichobainika ni kuwa walifariki kwa pamoja kufuatia ajali iliyowasababisha kudondoka ndani ya mfumo huo wa shimo kuu au walikwama humo ndani.
Baada ya kufariki, miili yao ilisukumwa ndani ya shimo lenye tope na kuganda humo kwa mda mrefu kama mabaki ya wanyama wengine yaliyokwama humo.

No comments:

Post a Comment