Wednesday, July 25, 2012

KOMBE LA KAGAME, MNYAMA ALAMBA LAMBALAMBA YENYE SUMU KALI UWANJA WA TAIFA


Wachezaji wa Azam wakishangilia bao lililotupiwa na John Bocco "Adebayor/Boko Haramu" aliekaa chini.

Vilabu vya Azam na Vita vimefanikiwa kuingia nusu fainali ya michuano ya soka ya Cecafa.

John Bocco alikuwa shujaa pale timu yake ya Azam ya Tanzania, ilipofanikiwa kuingia nusu fainali ya mashindano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati baada ya kuwafunga mabingwa wa Tanzania, Simba, mabao 3-1.

Katika mechi hiyo ya robo fainali iliyochezwa Jumanne mjini Dar es Salaam, Bocco alitupiamo kambanio mabao yote dakika ya 17, 46 na 73, wakati bao la kufutia machozi la Simba likitupiwa na Shomari Kapombe dakika ya 53.

Timu hiyo sasa itapambana na Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kwenye nusu fainali itakayochezwa Alhamisi.

Vita Club walifuzu baada ya kushinda kwa mambao 2-1 dhidi ya Atletico ya Burundi kwenye mechi nyingine iliyochezwa Jumanne. Mabao ya Vita yalifungwa na Taddy Etekiama na Basilua Makola wakati bao la Atletico lilifungwa na Pierre Kwizera.

Matokeo hayo yamekuwa ya kushangaza hasa ikizingatiwa kuwa Simba ni timu kongwe ambayo imeshinda kombe hili la ukanda mara sita.

Nayo Azam, iliyoanzishwa mwaka 2007, haya ni mashindano yao ya kwanza kimataifa tangu timu ianzishwe na ilipata tiketi ya kushiriki baada ya kumaliza ligi msimu uliopita ikiwa nafasi ya pili.

Mafanikio ya Azam yanakuja baada ya kusajili wachezaji kutoka Ivory Coast na Kenya na kumwajiri kocha kutoka Uingereza.

Mechi zote za nusu fainali zitachezwa Alhamisi kufuatia kuondoshwa Simba kwenye mashindano.

Timu nyingine zitakazokutana kwenye hatua hiyo ni bingwa mtetezi Yanga ya Tanzania na APR ya Rwanda.

Fainali itachezwa Jumamosi na bingwa atapewa zawadi ya dola 30,000 na mshindi wa pili 20,000, na atakayemaliza katika nafasi ya tatu ataondoka na kitita cha dola 10,000.

Katika mchezo wa huo, kikosi cha Azam kilikuwa; Deo Munishi, Ibrahim Shikanda, Erasto Nyoni, Said Mourad, Aggrey Morris, Kipre Michael Balou/Ramadhan Chombo, Kipre Herman Tcheche/George Odhiambo ‘Blackberry’, Salum Abubakar, John Bocco, Ibrahim Mwaipopo na Khamis Mcha ‘Vialli’/Jabir Aziz.

Simba SC; Juma Kaseja, Haruna Shamte, Shomary Kapombe, Lino Masombo, Juma Nyosso, Mussa Mudde, Uhuru Suleiman/Kiggi Makassy, Mwinyi Kazimoto, Felix Sunzu, Haruna Moshi na Jonas Mkude/Amri Kiemba.

Mrisho Ngassa akiwa ubaoni


Kocha wa Simba Milovan Cirkovic akiwa amelowana kwa kichapo.


Kocha wa Yanga Tom Saintfiet ,Felix Minziro naMfaume athumani wakifuatilia mtanange kati ya Simba na Azam


Benchi la Simba haliamini kilichotokea katika mechi yao dhidi ya Azam

Mashabiki wa Azam F.C


Mashabiki wa Simba S.C


John Bocco "Boko Haramu" akijaribu kuiponyoka ngome ya Simba


Felix Sunzu akiwa amerudi nyuma kusaidia kuokoa jahazi wakati mpira wa kona ukielekezwa lango la Simba


Kipre Cheche wa Azam akitiririka kuelekea kumsalimu Juma Kaseja


John Bocco "Boko Haram" akishangilia bao la pili


John Bocco 'Boko Haram" na Abubakar Saalum 'Sure Boy' wakishangilia kwa mtindo wa aina yake.

Nazi hii ilivunjwa na kamati ya ufundi ya Simba S.C lakini haikufua dafu!


Kikosi cha Simba




Kikosi Cha Azam F.C

No comments:

Post a Comment