Friday, June 10, 2011
PICHA YA LEO
Familia moja nchini Scotland kama inavyoonekana picha ambapo kila mtu katika familia hiyo anamiliki mnyama ampendae, tofauti kabisa na sehemu zingine tumezoea kuona watu wakimiliki vitu kama magari,baiskeli, pikipiki na vitu vingine...haya ukistaajabu ya Mussa utaona ya firauni.
Thursday, June 9, 2011
KULIKONI WATANZANIA BIGBROTHER AFRICA?
Katika ushiriki wa Tanzania hii miaka ya karibuni tumeonesha kupoteza dira kabisa na kila washiriki wanapoenda wanazidi kufanya vituko ambavyo vinaishushia hadhi Tanzania kutokana na ukweli kwamba mataifa ya nje yanahubiri ukarimu,upendo na tabia njema tulizonazo wa-TZ.
Miaka ya mwanzo washiriki wetu walianza vizuri sana na tukajisifu katika hilo lakini miaka hii hakuna mtanzania anaetamani hata kuiangalia Bigbrother kutokana na madudu yanayofanywa na washiriki wetu.Kwa mara ya kwanza alipoingia Mwisho Mwampamba mjengoni alifanya vizuri sana na akawa mshindi wa pili na kuipa shavu kubwa sana Tanzania japo alikuwa na mapungufu ya hapa na pale lakini sio ishu, akaja Richard na yeye akafanya vizuri hatimae kuibuka kidedea katika mashindano hayo na hakika hapo ndipo watanzania tukasema hakuna anaetuweza katika mashindano ya Bigbrother Africa.
Aliyekuwa mshiriki wa TZ na mshindi wa pili katika shindano la Bigbrother Africa I, Mwisho Mwampamba.
Aliyekuwa mshiriki wa Tanzania na kuibuka mshindi katika shindano la BigbrotherAfrica II,Richard Beduizenhout.
Latoya.
Baada ya washiriki waliotangulia kufanya vizuri, waliofuatia wakavimba vichwa na kujiona kwa kuwa wametoka Tanzania basi wao ndio wao au niseme washiriki wetu walipatwa na ule msemo usemao "Mgema ukimsifia Tembo hulitia maji"? kiukweli kabisa ndivyo ilivyo...sasa basi tukaona ngoja tutupe karata na kwa wadada..mama yangu tunajuuuta kuwafahamu na kuwapeleka mjengoni, hakika bora tungekaza uzi wa kupeleka vidume hata wakifanya madudu mwisho wa siku ni kuchanganya mataifa tofauti na madada zetu wanaomwegwa kisela.
Mwaka huu kichefuchefu kimetutokea mdomoni sio puani,tumepeleka wadada wawili..jamani mimi nawalaumu waliowachagua bila kuchanganya na kidume pale mjengoni, hakuna asiejua yaliyotokea baada ya kuwapeleka Bhoke na Lotus..mhhhhh, mmoja mapemaaaa kisa ngumi mkononi halafu bora angekuwa Bhoke tungesema ni walewale vita ni vita mura, lakini hapana ni Lotus kamchapa mshiriki mwenzake Luclay kavukavu mwisho wa siku Out.
Lotus
Akabaki Bhoke..mama yangu akagawa uroda kama biskuti..Ernest akamega kisela live bila chenga kila mtu kajionea kasoro vipofu tu ila na waop minong'ono watakuwa wameisikia. Bhoke nae mwisho wa siku kafungasha mapemaaa yupo home, sasa hatujui jamaa ataendelea kumega au ndio walikutana kimjinimjini?
Bhoke
Sasa watanzania wenzangu washiriki wetu ndio wameshatuangusha sasa tufanye nini ili miaka ijayo turudishe heshima yetu? Mimi nianze kutoa maoni yangu,Moja kuna haja tunapochagua washiriki tupate tabia za mtu tangu utotoni na hivi sasa kuwa anaishi vipi, ili kupata watu wenye maadili ya kitanzania na tusiendelee kujitia aibu, Pili mshiriki aingie mkataba na akubali akirudi tunamuadhibu kulingana na sheria za nchi pale itakapodhihirika ameitia nchi aibu na kuwafedhehesha watanzania kipindi chote alichokuwa ndani ya mjengo. Toeni maoni yenu kupitia Bog hii au mnicheki jiffjeff@yahoo.com .

NIONAVYO LEO HII.
Mtu yeyote yule ambaye hajawahi kufanya makosa inamaanisha kuwa hajawahi kujaribu kitu kipya katika maisha yake kwani mtu hujifunza kutokana na makosa.
Wednesday, June 8, 2011
WANYAMA NI RAFIKI WAZURI KWA BINADAMU.
Hapa duniani kiumbe ambaye amepewa akili ya kuweza kuufahamu ulimwengu na kuutawala ni Binaadamu, Pamoja na hilo maisha ya Binaadamu yanategemea viumbe wengine waliomzunguka kwa asilimia kubwa,mfano binaadamu wanategemea wanyama kwa kupata chakula mfano,Ng'ombe,mbuzi,nguruwe,kondoo na wengineo wengi. Binaadamu anategemea wanyama wengine kwa kazi za kila siku mfano,Punda kubeba mizigo, Ng'ombe kulimia na hata ubebaji wa mizigo. vilevile Binaadamu anategemea wanyama kwa ulinzi kwa mfano Mbwa.
Lakini baadhi ya wanyama wametokea kuwa adui wakubwa kwa Binaadamu kwa mfano Simba,Chui,Nyoka,na wengineo wengi. Lakini nimegundua kuwa Binaadamu na wanyama wanaogopana kwasababu hawajajuana, lakini pindi Mnyama anapokuwa karibu na akawa na mazoea na Binaadamu basi huwa rafiki mzuri sana wa Binaadamu kwa mfano Simba,Chui,Mbwa,Dubu ,Nyoka na wengineo wengi.angalia picha zifuatazo kwa ushahidi zaidi.

Samaki aina ya DOLPHIN wakicheza na watoto.
Chui wakijiachia kitandani na mlezi wao.
Pamoja na kuwa na urafiki na Binaadamu hata wao kwa wao ni marafiki.
Tuesday, June 7, 2011
PICHA YA LEO
Ni kama huyu mtoto anasema " Aaah mzee...unanipa pipi? shuka uone home tulivyo majalala..hapa nilipo sina hata sare za shule, home hatujala tokea jana mchana".
WAJUE 10 WANAOWANIWA NA ARSENE WENGER.
Meneja wa timu ya Arsenal ya uingereza Arsene Wenger amnahusishwa na nia ya kuhitaji wachezaji ambao atawatumia kujenga kikosi cha timu ya Arsenal ambacho kimemaliza ligi na hali mbaya japokuwa kilikuwa kikiwania ubingwa kwa karibu zaidi, wachezaji ambao wapo kichwani mwa Wenger ni hawa wafuatao.
1-Gervinho, mshambuliaji wa Lille ya ufaransa raia wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 24 ambaye anauzwa kwa dau la paundi za uingereza milioni 12-15.
2-Borjan Kric,Mshambuliaji wa Barcelona na raia wa uhispania mwenye umri wa miaka 20 dau lake ni paundi za uingereza milioni 16-18.
3-Mamadou Sakho,mlinzi wa kati wa PSG na raia wa ufaransa mwenye umri wa miaka 21 dau lake ni paundi za uingereza milioni 12-18.
4-Jan Vertonghen,Mlinzi wa kati wa Ajax na raia wa ubelgiji, umri miaka 24,dau lake ni paundi za uingereza milioni 12-15.
5-Gary Cahill, Mlinzi wa kati wa Bolton na raia wa uingereza, umri miaka 25,dau lake ni paundi za uingereza milioni 15-20.
6-Phil Jones, Mlinzi wa kati wa Blackburn na raia wa uingereza, umri miaka 19, dau lake ni paundi za uingereza milioni 15-18.
7-Karim Benzema, Mshambuliaji wa Real Madrid na raia wa Ufaransa,umri miaka 23, dau lake ni paundi za uingereza milioni 20-26.
8-Christopher Samba, Mlinzi wa kati wa Blackburn na raia wa Congo, umri miaka 27, dau lake ni paundi za uingereza Milioni 8-12.
9-Radamel Falcao,Mshambuliaji wa Porto na raia wa Colombia, umri miaka 25, dau lake ni paundi za uingereza milioni 26.
10-Ricardo Alvarez, mshambuliaji wa pembeni wa Velez Sasfield na raia wa Argentina, umri miaka 23, dau lake paundi za uingereza milioni 6-12.
ARSENE WENGER
wakati huo huo wenger anatafuta mrithi wa Niclas Bendtner mbali na hao kumi katika kumrithi Bendtner wengine ni Jeremy Menez wa Roma ya italy, Hugo Rodallega waWigan Athletic,Hulk wa Porto F.C, Gonzalo Higuian wa Real Madrid na Eden Hazard wa Lille.
BURRESS AMALIZA KIFUNGO CHA MIAKA MIWILI.
Hatimaye mchezaji mashuhuri wa NEW YORK GIANTS siku ya jumatatu tarehe 6 mida ya saa tatu asubuhi aliachiliwa huru kutoka gerezani ikiwa ni miezi mitatu kabla ya kifungo chake kukamilika kutokana na kuonesha tabia njema akiwa gerezani na kurudi nyumbani kwake Florida baada ya kutumikia kifungo cha miaka miwili jela kwa kosa la kukutwa na silaha, ambapo siku ya tukio novemba 2008 akiwa katika klabu ya usiku jijini New York kwa bahati mbaya risasi aliyoiweka kiunoni ilifyatuka na kumpiga katika mguu na kusababisha kukamatwa kwake na silaha kinyume na sheria.
Plaxico Burress akitoka Gerezani.
Plaxico Burress akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoka gerezani.
Plaxico Burress akiwa amembeba mwanae Elijah Burress baada ya kutoka gerezani.
Plaxico Burress uwanjani kabla ya kukamatwa kwake.
Akiwa amevalia mavazi meusi,sweater jeusi,t-shirt nyeupe na pale chini ametupia sneakers nyeusi akiwa peke yake kutoka gerezani na kuangaza huku na huko na kumuona meneja wake Drew Rosenhaus na kumrukia kwa furaha."Napenda kumshukuru mungu kwa kunipa moja ya mitihani maishani mwangu" alisema burress, "Napenda niwashukuru wote kwa maombi na maneno ya kunitia nguvu nikiwa gerezani" aliongeza Burress. Burress ambaye mwezi wa nane anatimiza miaka 34 alijitupia ndani ya Range Rover na kuungana na mkewe tayari kwenda nyumbani kufungua ukurasa mpya wa maisha baada ya kifungo.
Burress alitoka gerezani akiwa amevalia kofia ya Philadelphia Phillies na inasemekana kuna uwezekano mkubwa akarudi kuichezea tena na wakati huohuo kuna uwezekano wa timu ya New York Jets wakamchukua ili kuziba pengo la Braylon Edwards aliyestaafu.

Subscribe to:
Posts (Atom)