Friday, June 24, 2011

MANUEL JURADO ATAJWA KUMRITHI CSEC FABREGAS.

Klabu ya AS Roma ya Italy ipo katika mpango wa kumnasa chipukizi wa Barcelona Bojan Krkic kwa kitita cha euro milioni 10. Hii ina maana kwa Barcelona kuweza kutumia pesa hizo na kuongeza zingine ili kumnasa Kiungo wa Arsenal Csec Fabregas. Wenger ili kujiandaa na maisha bila ya Fabregas tayari ameshaweka malengo ya kumnasa kiungo mchezeshaji wa Schalke 04 Juan Manuel Jurado, ambapo mpango wa Wenger ni kutumia paundi za Uingereza milioni 7.5, Jurado aling'ara zaidi katika fainali za ligi ya mabingwa ulaya 2010-2011 ambapo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 aliiwezesha Schalke 04 kufika nusu fainali.

WENGER AJIPANGA KUMNASA DIARRA

Mahamadou Diarra
Meneja wa timu ya Arsenal ya Uingereza Arsene Wenger anajipanga kumnasa nyota wa Real Madrid Mahamadou Diarra. Habari zinasema Wenger anajipanga kumpa Diarra mkataba wa mwaka mmoja na kumtengea mshahara wa paundi za Uingereza 50,000 kwa wiki.

MELLO ACHUKIZWA KUBADILISHWA NA MEIRELES

Felipe Mello

Raul Meireles
Kiungo wa Juventus Fellipe Mello amekasirishwa na hafurahii kitendo cha cha uongozi wa Juventus kumtoa "kafara" na pesa kidogo ili kumnasa mchezaji wa Timu ya Liverpool mreno Raul Meireles. Juventus wapo tayari kumtoa Mello na kitita cha paundi za Uingereza milioni 13 ili kumnasa Meireles.Akiwa hajatimiza hata mwaka tangu asajiliwe na Liverpool akitokea Porto kwa ada ya paundi za Uingereza milioni 10,Meireles sasa anahitajiwa na Juventus kwa udi na uvumba. "Kwa hiyo tuseme Juve hawaniheshimu,hicho ndio nachoweza kusema" Mello aliliambia gazeti la Daily Mirror, "Yaani mi si lolote?,mi sio wa kujadiliana kwa bei nafuu" aliongeza Mello.

BARCELONA WATAJA DAU KUMNG'OA FABREGAS.

Csec Fabregas
Habari ya kweli ambayo imeripotiwa na magazeti mengi ya leo asubuhi ni kwamba Timu ya Barcelona ya Uhispania imetaja kuwa inataka kumsajili kiungo wa Arsenal ya Uingereza Csec Fabregas kwa kitita cha Paundi za Uingereza milioni 27.