Wednesday, July 20, 2011

JENNIFER LOPEZ,MARC ANTHONY WAACHANA

KISA NI WIVU,KUKOSA UAMINIFU

Walipotangaza kuachana julai 15, Jennifer na Marc Antony waliweka wazi kuwa tayari wameshaweka mambo sawa na kila kitu ni shwari. watu wanaowafahamu wawili hao si ajabu wakashangazwa na kauli hiyo na kuuita huu ndio mwisho wa ndoa yao iliyodumu kwa miaka saba. Uamuzi wa kuachana umekuja baada ya ugomvi uliodumu kwa miezi kadhaa. Taarifa kutoka kwa mtu wa karibu wa wawili hao anasema chanzo kimeanzia katika maandalizi ya filamu, wivu katika steji ya American idol na Lopez (41) akimshutumu Marc Anthony kutokuwa mwaminifu.

Zifuatazo ni picha za familia hiyo kabla ya kuachana wakila bata

Lopez akiwa na mapacha wake Max na Emme










SONG OF THE DAY

RIHHANa-California King Bed

NGASSA USO KWA MACHO NA MAN UNITED

Mrisho Ngassa katika moja ya mechi akiwa na timu ya Taifa

Mshambuliaji wa Azam f.c na timu ya Taifa stars Mrisho Ngassa leo anapata nafasi ya kuivaa Man United ya Uingereza ambayo ipo Marekani katika mechi za majaribio. Ngassa atakuwa na timu yake ya Seattle Sounders ya Marekani ambapo Ngassa anafanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa,kipute hicho kitapigwa katika dimba lenye nyasi bandia la Century Link. Jana Ngassa alionekana katika uwanja wa Seattle Sounders wa Starfire wakijiandaa dhidi ya mechi yao na Man United leo.
Wakati Ngassa akiivaa Man United mtanzania mwingine Nizar Khalfan akiwa na Vancouver White Caps amecheza mechi dhidi ya Man City na kupokea kipigo cha mabao 2-0.

Tuesday, July 19, 2011

MFALME ANAPOCHAGUA KIFAA SWAZILAND MAMBO HUWA HIVI

Agosti 31, nchi ndogo ya Swaziland iliyopo katikati ya Afrika ya kusini hufanya sherehe ya mwaka kumtafuta malkia. Wasichana 50,000 hukusanyika karibu na ikulu, wasichana hawa huwa watupu kama walivyozaliwa isipokuwa baadhi tu ya sehemu za mwili huwa zimezibwa huku wakiimba na kupigiza miguu kwa kishindo katika ardhi yenye vumbi jekundu, wakati huo mfalme wa Zulu akiwa amekaa kivulini kwenye hema akiangalia wasichana hao kwa tabasamu la kuopoa kifaa kipya. Sherehe hizi zimejizolea umaarufu kwa wasichana wa kizulu ambao baadhi hutoka mile kadhaa,mfano Durban ili kuja kucheza katika sherehe hiyo ya heshima. Zifuatazo ni picha za sherehe hizo zinavyokuwa.

Wasichana wa kizulu wakipita mbele ya mfalme

Wakiimba na kucheza kwa furaha



Wakipita kwa mbwembwe

Hatime wamesimama mfalme apate kuchagua kifaa chake



FASHION MPYA KWA VIATU VYA KIKE








UAE’s Awana Diab attempts insane penalty kick (and it works)

Monday, July 18, 2011

SIKU YA MATOPE U.S.A

Kila mwaka taifa la marekani watu husherehekea siku ya matope ambayo huazimishwa Nankin Mills kila tarehe 12 julai ndani ya jiji la Westland,Michigan. Katika sherehe hizo galoni za maji zipatazo 20,000 huchanganywa na udongo tani 200 ili kutengeneza tope tayari kusherehekea. zifuatazo ni picha katika sherehe hiyo ijulikanayo kama "MUD DAY"